Kwanini tudai katiba mpya sasa

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
Tanzania ni nchi huru inayokatiba iliyoidhinishwa mwaka 1977 na kurekebisha kila kipindi inapobidi. Kwanini tusiendelee kuirekebisha kama ilivyokua mwanzo. nini hoja ya msingi ya kutaka katiba mpya sasa na sio marekebisho. :bump::msela:
 
Join Date : Sun Jan 2011
Posts : 1
Thanks0Thanked 0 Times in 0 Posts

Rep Power : 0

Piga hodi kwanza na usalimie uliowakuta humu jamvini, nachukua nafasi hii kukukaribisha, japo unaingia kikushotokushoto
 
katiba mpya kabisa ni lazima,
>kwanza kwa sababu taifa limekosa mwelekeo, tunataka taifa jipya lenye mwelekeo mpya unaoendana na watu wa sasa, hususani vijana(tukumbuke katiba mpya ni kwa ajili ya vijana wa tanzania na watoto ambao ni taifa la kesho)
>pili ijaze utupu uliopo kwakuwa kwa sasa katiba haitamki ni vipi tutambana kiongozi mzembe na mlarushwa, pia katiba haiweki wazi kiongozi wa serekali anatkiwa awe na sifa gani(kielimu na kimaadili) na je akikiuka maadili hayo tumfanyaje?
>katiba ambayo itatamka wazi vipi muungano wa tz na zbr utakuwa, kwa nini tangu 1961 marais wa tz 3 wametoka bara na 1 ndio katoka zanzibar?
>sababu ni nyingi sana na zinaendelea
tanzania mpya katiba mpya,
kanyaga twende.
 
Tanzania ni nchi huru inayokatiba iliyoidhinishwa mwaka 1977 na kurekebisha kila kipindi inapobidi. Kwanini tusiendelee kuirekebisha kama ilivyokua mwanzo. nini hoja ya msingi ya kutaka katiba mpya sasa na sio marekebisho. :bump::msela:

Nani kakutuma?Umeingia tu na kioja juu.Tulishajadili hapa.Unataka kuturudisha nyuma?
 
Nani kakutuma?Umeingia tu na kioja juu.Tulishajadili hapa.Unataka kuturudisha nyuma?

mtu aliyetoa kauli hii nadhani anafikiri JamiiForums ni kwa ajili ya kutoa maoni anayopenda yeye tu. Ukweli ni kwamba hatuhitaji katiba mpya, labda muungano ukishavunjika. Ila kama nchi hii ya Tanzania itaendelea kuwepo basi ni suala la kufanya mabadiliko machache na nyongeza za msingi tu katika katiba yetu.

Tatizo watanzania wengi (ashukum si matusi, ambao ni wajinga*) wanarukia tu ki-ushabiki eti wanataka katiba mpya wakidhani ndio muarobaini wa kuwaletea maendeleo. Yaani watu wengine wanadiriki kusema bora damu imwagike ili katiba mpya ije. Kama mtanzania una uchungu na nchi hii wahimize ndugu zako jasho za damu ziwatoke kwa kufanya kazi ili nchi iendelee. Kama kiongozi hawajibiki na katiba inamlinda basi turekebishe katiba ili isimlinde. Pale ambapo hawajibiki tumuwajibishe. Sio kupoteza nguvu na jasho kung'ang'ania katiba.
 
Back
Top Bottom