Kwanini Trump alisema Afrika inatakiwa kutawaliwa tena kama miaka 100?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nilisikia kauli ile ila sikujua hasa kwanini alisema kauli ile.Hata hivyo niliikubali sana.

Sababu kubwa ya kwanini niliikubali ni kwamba, wazungu wana aibu wanapofanya mambo mabaya dhidi ya binadamu au hata viumbe wengine. Hata kama watatutawala, naamini hawatatutesa kama nionavyo waafrika wakiteseka sasa chini ya waafrika wenzao.

Mzungu hata akifuga mbwa anatunzwa vizuri sana kwa daraja lake, lakini roho zetu waafrika ukitaka kuzijua vizuri angalia tusivyo wajali hata mifugo yetu. Utakuta mtu ana punda hadi katoka vidonda lakini ndo kwanza anabebeshwa mzigo mzito. Ndivyo zilivyo roho za wengi wa viongozi wetu. Hawajali watu madamu wao walishapata. Sababu za kumkubali Trump ni zangu,

Je, yeye alifikiri nini hasa hadi kutamani Afrika itawaliwe tena?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom