Kwanini TRA sasa hawatangazi mapato ya kikodi ya kila mwezi kama ulivyokuwa utaratibu?

We nae unaongea ujinga gani uliona mapato ya serikali yakaingia mfukoni mwa raia inamaana mpaka umri huo ulionao hujui matumizi ya kodi!!!??
Wewe ndo tatizo! Ni huduma gani imekwama kwa TRA kutotangaza mapato yake ktk miezi hii 2? Afterall ilikuwa inasaidia nini kutangaziwa makusanyo wakati matumizi huambiwi? CAG akijaribu kudadavua matumizi inakuwa bifu kuanzia kwa Spika wa Bunge hadi Ikulu?
 
Ukisikiliza bajeti bungeni na ukisoma ripoti za BoT na CAG utafahamu vizuri sana
Nchi yetu sio zile miongoni mwa zilizoendelea wale walioendelea waacheni na utaratibu wao wakutokutangaza ila sisi masikini nivizuri tukitangaziwa ili tujue kama tunapanda au tunashuka
 
Mazoea yana tabu na ukikosa kitu ama jambo ulilolizoea pia huja maswali.

Mimi jitombashisho nataka kujuzwa na TRA ni kwanini takribani miezi miwili sasa hamtoi taarifa juu ya mapato ya kila mwezi?!
Nani alianzisha huo utaratibu? Lengo lake lilikua nini? Deni la Taifa kutoka 2015 hadi sasa limekua kwa kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mazoea yana tabu na ukikosa kitu ama jambo ulilolizoea pia huja maswali.

Mimi jitombashisho nataka kujuzwa na TRA ni kwanini takribani miezi miwili sasa hamtoi taarifa juu ya mapato ya kila mwezi?!
Mara ya mwisho TRA kutangaza mapato ya nchi ilikuwa mwezi gani? Na nini kilisababisha tangu wakati huo yasitangazwe?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Fanya uchunguzi ni wafanyabiashara wangapi wamenyang'anywa hela zao benk, ndio utajua kwa nini TRA wanakwama kutangaza mapato.
 
Nilikuwa nashangaa sana. Labda kama kulikuwa na lengo mahsusi ila kama ni sababu za kisiasa basi tulikosea sana.
Hata sisi raia wa kawaida tu, total earnings zetu ni siri yetu, halafu tunaibuka kutangaza mapato yote ya nchi? Hata pale kwenye website yao waondoe. Kuwe na taarifa za jumla jumla tu. Detailed reports za mapato kwa nchi sio kabisa. Mapato ya nchi hayana tofauti na military budget or capability.
Umetokea wapi?? Mars au??
 
Sababu ni ushamba, na mshamba namba 1 tushafukia, kaenda na mambo yake ya kishamba ya kupika data na kupora hela wafanyabiashara na kuziingiza kwenye mapato ya kila mwezi.
 
Mazoea yana tabu na ukikosa kitu ama jambo ulilolizoea pia huja maswali.

Mimi jitombashisho nataka kujuzwa na TRA ni kwanini takribani miezi miwili sasa hamtoi taarifa juu ya mapato ya kila mwezi?!
Ni aibu maana wafanyabiashara wengi siku hizi wanakwepa kodi, risiti wanaandika za vitabu ukiwauliza EFD wapi wanakujibu mashine mbovu kumbe wamezificha. Zitto Kabwe alikuwa bingwa wa kutoa takwimu za makusanyo ya mwezi toka TRA lakini siku hizi hatumsikii. Nina wasiwasi kama makusanyo yanafikia hata trilioni moja
 
Nilikuwa nashangaa sana. Labda kama kulikuwa na lengo mahsusi ila kama ni sababu za kisiasa basi tulikosea sana.
Hata sisi raia wa kawaida tu, total earnings zetu ni siri yetu, halafu tunaibuka kutangaza mapato yote ya nchi? Hata pale kwenye website yao waondoe. Kuwe na taarifa za jumla jumla tu. Detailed reports za mapato kwa nchi sio kabisa. Mapato ya nchi hayana tofauti na military budget or capability.
Wala sio vibaya hiyo si ndiyo tunasema uwazi? Pesa hizo si za umma? Ata kule Serikali z Mitaa Wenyeviti wanasisitizwa kutangaza mapato na matumizi, kwenye NGo's ndiyo kabisa unaambiwa kwenye ubao wa matangazo wabandike kabisa sasa leo hatutaki kusikia tulichokusanya mwa miezi mitatu..!! Sina hakika kama Watanzania wanajua wanataka nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndo tatizo! Ni huduma gani imekwama kwa TRA kutotangaza mapato yake ktk miezi hii 2? Afterall ilikuwa inasaidia nini kutangaziwa makusanyo wakati matumizi huambiwi? CAG akijaribu kudadavua matumizi inakuwa bifu kuanzia kwa Spika wa Bunge hadi Ikulu?
Matumizi Bajeti ilishipitishwa mzee mwisho wa mwaka wa fedha tunaweza kujumlisha wenyewe tulichokusanya kutokana na makusanyo ya kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom