Kwanini Tiketi za UDART/MaxMalipo hazioneshi kiasi cha nauli kilicholipwa?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,796
5,509
Nimeshangazwa sana na tiketi za mabasi ya haraka ya UDART ambazo zinatolewa na MaxMalipo kuwa hazionyeshi kiasi cha nauli anayolipa abiria.

Hakuna mahali hapa nchini na duniani ambapo mnunuzi analipia huduma au bidhaa na kupewa stakabadhi ambayo hazionyeshi thamani ya pesa aliyolipa.

Hawa UDART na MaxMalipo kutoa stakabadhi isiyoonesha kiasi cha nauli tuliyolipa inaashiria nini, tuwaeleweje?

Wanawasilisha malipo ya kodi TRA kwa kutumia kigezo gani? Iwapo abiria anatakiwa kuwasilisha kazini kwake ili arejeshewe nauli na mwajiri wake au anatakiwa kufanya retirement, Mhasibu ataelewaje?

Wahusika walifanyie kazi hili.
 
Piga utume , na kituo ulichokatia pia useme. ...otherwise tutaona ni story za kutuchangamsha humu.
 
Barbarosa
Duh, wewe unaonaje? Je, ni sawa tiketi kutoonyesha kiasi cha pesa ambacho mtumaji amelipa? Hilo limekaa sawa? Mbona inaonekana kama vile umekwazwa? Kama unayo maslahi mahususi ktk hizi tiketi yakupasa urekebishe sio ubeue!

Salute!
 
Lingine ambalo limeshtua leo hii ni hili;

Ukikata tiketi na kwenda kupita kwenye vile vyuma kuna mtu una mkuta anachukua na kuipitisha/ana scan kuonesha umepita, lkn isipo_scan anakwambia pitia upande huu, akimaanisha upande usio na vyuma vya kukuruhusu kupita.

Sasa basi, moja kwa moja uki_scan inaonekana kwenye system na isipo_scan inaonekana kuharibika hivyo kuna nini kinachopelejea hizo tikiti zengine zisisome?

Au ndio kutengeneza pesa mapema kabla hawajastuka?

**Binafsi nilikataa a_scan nika_scan mwenyewe na ikakubali!!.

NOTED.
 
Vv

Mimi naona ni mapungufu na sehemu ya changamoto tu, mradi ndiyo kwanza umeanza hata mwezi hauna hivyo tulipaswa tuwaache DART wafanye kazi yao angalau baada ya kuanzia miezi 3-6 ndiyo tuanze kukosoa, kwani watu wenyewe bado wako kwenye majaribio na sidhani kama wewe peke yako ndiyo utakuwa umeliona hilo!

Hivyo wewe chill and relax rudi baada ya miezi 3 kwa sasa shukuru angalau hata mabasi yapo na yanafanya kazi!
 
Ndugu mradi bado uko kwenye majaribio hivyo kuna mambo mengi bado hayajakaa sawa kuweni na subira angalau mjaribu kukosoa baada ya miezi mitatu, watu kama ninyi sidhani kama mtakuja kufanikiwa maishani kwani mmejikita zaidi kwenye negativity klk positivity!
 
Piga utume , na kituo ulichokatia pia useme. ...otherwise tutaona ni story za kutuchangamsha humu.
Unataka ushahidi gani? U-fake wa hizo tiketi nimeuelezea kwa misingi ya sheria, lkn system zao zinazitambua hizo tiketi na mageti yao yanazikubali na kufunguka.

UDART na Max Malipo wenyewe ndio wamezitengeneza zikiwa na hizo discrepancies za makusudi.

Vv
 
Mimi naona ni mapungufu na sehemu ya changamoto tu, mradi ndiyo kwanza umeanza hata mwezi hauna hivyo tulipaswa tuwaache DART wafanye kazi yao angalau baada ya kuanzia miezi 3-6 ndiyo tuanze kukosoa, kwani watu wenyewe bado wako kwenye majaribio na sidhani kama wewe peke yako ndiyo utakuwa umeliona hilo!

Hivyo wewe chill and relax rudi baada ya miezi 3 kwa sasa shukuru angalau hata mabasi yapo na yanafanya kazi!
Naona una utoto tu, how can they improve if we consumers do not identify and tell them of their weakness? However, the raised concern is very sensitive to ignore and wait for weeks or months, they can correct it immediately.

Vv
 
Nimeshangazwa sana na tiketi za mabasi ya haraka ya UDART ambazo zinatolewa na Max Malipo kuwa hazionyeshi kiasi cha nauli anatoyolipa abiria.

Hakuna mahali hapa nchini na duniani ambapo mnunuzi analipia huduma au bidhaa na kupewa stakabadhi ambayo hazionyeshi thamani ya pesa aliyolipa.

Hawa UDART na Max Malipo kutoa stakabadhi isiyoonyesha kiasi cha nauli tuliyolipa inaashiria nini, tuwaeleweje?

Wanawasilisha malipo ya kodi TRA kwa kutumia kigezo gani? Iwapo abiria anatakiwa kuwasilisha kazini kwake ili arejeshewe nauli na mwajiri wake au anatakiwa kufanya retirement, Mhasibu ataelewaje?

Wahusika walifanyie kazi hili.

Vv
Usisahau kuna insurance wakati wa ajali nao ni wadau katika suala la tiketi. Ila tatizo lingine hizo tiketi hazioneshi sehemu ulipotoka na unapokwenda.
 
Naona una utoto tu, how can they improve if we consumers do not identify and tell them of their weakness? However, the raised concern is very sensitive to ignore and wait for weeks or months, they can correct it immediately.

Vv

Kwani ukiandika kiingereza ndiyo kuna kitu umebadilisha? Mabasi yako kwenye majaribio hata mwezi hayamaliza na hata DART wenyewe wamesema wako kwenye majaribio au hauelewi maana ya majaribio?

Kwani Wazungu wenu huwa kwanini wanafundisha Kiingereza chao lkn hawawapi akili zao?
Majaribio ni majaribio kila kitu kinajaribiwa kama kiko sawa au unafikri ktk DART yoote wewe tu ndiyo umeliona hilo??
 
Hili swala jana alilizungumzia mkurugenzi wa maxmalipo, wamesema wameshapata malalamiko na swala lipo mezani, linafanyiwa kazi. Hizo ni changamoto tu, kila ikija changamoto ni wajibu wao kuifanyia kazi coz wapo kwenye transition period.
 
Kuwa mradi ndio umeanza ndio tukae kimya hilo halikubaliki,tunatakiwa tuseme kasoro zilizopo from the begining,watajuaje kuwa wanakosea kama hataelezwa matatizo ambayo inawezekana kwa kukaa kimya wanaweza wasiyagundue.
 
Chamakimoja ooh sorry Vyamavingi hebu wape mfano huu hapa;
36af58590f4ed8e503eb330b5978464d.jpg
nauli imeoneshwa wapi?
 
_hivi wagonjwa wa akili nao mmo humu jf..!!

Ulifundishwa na wazazi wako watu wanaofanikiwa hawakosoi jambo?

Au shule uliyopitia umeambiwa ukianzisha biashara TRA watakupa machine na karatasi zake kwa ajili ya majaribio?
& na POLE SANA!!
Ndugu mradi bado uko kwenye majaribio hivyo kuna mambo mengi bado hayajakaa sawa kuweni na subira angalau mjaribu kukosoa baada ya miezi mitatu, watu kama ninyi sidhani kama mtakuja kufanikiwa maishani kwani mmejikita zaidi kwenye negativity klk positivity!
 
Kwani ukiandika kiingereza ndiyo kuna kitu umebadilisha? Mabasi yako kwenye majaribio hata mwezi hayamaliza na hata DART wenyewe wamesema wako kwenye majaribio au hauelewi maana ya majaribio?

Kwani Wazungu wenu huwa kwanini wanafundisha Kiingereza chao lkn hawawapi akili zao?
Majaribio ni majaribio kila kitu kinajaribiwa kama kiko sawa au unafikri ktk DART yoote wewe tu ndiyo umeliona hilo??
Mkuu Barbarosa mleta mada ana hoja ya msingi hao Dart et al..wanategemea mawazo na ushauri kutoka kwako na kwangu ili waboreshe huduma vizuri tafadhali usibeze ushauri wake ni wa muhimu.
 
Kwani ukiandika kiingereza ndiyo kuna kitu umebadilisha? Mabasi yako kwenye majaribio hata mwezi hayamaliza na hata DART wenyewe wamesema wako kwenye majaribio au hauelewi maana ya majaribio?

Kwani Wazungu wenu huwa kwanini wanafundisha Kiingereza chao lkn hawawapi akili zao?
Majaribio ni majaribio kila kitu kinajaribiwa kama kiko sawa au unafikri ktk DART yoote wewe tu ndiyo umeliona hilo??

Ktk thread niliyoanzisha nimehitimisha hivi, 'Wahusika waliangalie hilo', lkn wewe uko bize ku-defend unreasonably.

Nimechagua kukupuuza.

Vv
 
_hivi wagonjwa wa akili nao mmo humu jf..!!

Ulifundishwa na wazazi wako watu wanaofanikiwa hawakosoi jambo?

Au shule uliyopitia umeambiwa ukianzisha biashara TRA watakupa machine na karatasi zake kwa ajili ya majaribio?
& na POLE SANA!!

Watu wote waliofanikiwa maishani wana tabia moja ambayo huwatambulisha nayo ni
,,subira na uvumilivu"
sasa wewe umeshaambiwa kwamba mabasi yako kwenye majaribio na wala mwezi mmoja hayajamaliza kwanza hata nauli zenyewe ndiyo wameanza kutoza baada ya kuwa yanachukuwa watu bure na ni swala la muda tu kabla hawajalifanyia kazi, na ndiyo maana wamesema wako kwenye majaribio au hilo neno labda halieleweki maana yake?!

Sasa kama unashindwa kuwa na ,,subira na uvumilivu" kwa jambo ambalo tayari umekwisha ambiwa kwamba liko kwenye majaribio unawezaje kufanikiwa maishani?
Kwa maana mambo yote maishani yanafanana, na yanahitaji ,,subira na uvumulivu"
 
Nimechagua kukupuuza.

Vv

Siku nyingine jaribu kuwa na subira na uvumilivu hiyo ndiyo siri ya mafanikio maishani na siyo kutaka kila kitu kiende jinsi unavyotaka wewe kwa kuwa tu wewe unataka hivyo hata pale ambapo tayari umekwisha ambiwa kwamba wako kwenye majaribio!
 
Back
Top Bottom