Kwanini tech director wa atcl asifukuzwe kazi kwa hili!!!!!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,947
22,105
Kwenu wanandugu,
Habarini za kwenu,najua ni wengi wanaipenda ATCL na wengi wanaitakai mema kampuni hii ...tumekuwa tukipiga kelele kila siku hakuna pesa kwenye hii kampuni na pesa zimekuwa zikitolewa kila siku mahesabu yanaonyesha kati ya BILLION 7.1 wameshapewa BILLION 6.8...na kampuni bado inasheki kwa kweli inasikitisha lakini hakuna jinsi zaidi ya kuwaacha watawala wenyewe
Tumekuwa ATCL zaidi ya miaka 25 sasa lakini vituko vinavyotokea hapa kitengo cha techn ni hatari kwa kweli...na nina hakika hata waziri akifuatilia atakuwa wa kwanza kukimbilia hazina na kuwaambia wasimamishe hizo pesa wanazopewa kila siku....
Ndugu watanzania kama kichwa cha habari kinavyosema sisi kama mafundi tumeona imetosha na hakuna haja ya kuendelea na huyu mkurugenzi wa kitengo cha ufundi....,hakika hakuna atakaekubali aendelee na cheo hiki...tumekuwa tukilalamika kwa mkurugenzi mtendaji matokeo yake amekuwa akimngangania na kumkumbatia mpaka hapo vituko vinatokea hana wa kumuuliza mana alishaambiwa kabla...
Tunajjua serikali imekuwa ikitoa hela kwa ajili ya uendeshaji lakini inaonekana watu wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao....hapo nyuma unaweza kuamini yalitumwa matairi 4 kutoka london ,,,na kabla ya kufika hapa nchini ndge kubwa ya AIRBUS ilikuwa chini kwa zaidi ya mwezi....lakini yalipofika na kuwekwa kwenye ndege ati yamekutwa saizi ni tofauti!!!
Jamani hata kama pesa ipo..mzigo wa matairi umelipiwa cargo kutoka uingereza umefika ukalipiwa tax kutolewa jamani inaingia akilini kukuta matairi hayaendani na size yalipo kwenye ndege.....tumellalamika tukaomba wahusika washurutiwe kuwajibika hakuna aliekuwa wa kwanza kufanya hivyo zaidi ya kulindana....sasa majuzi tumepata billion 2.4,
Baada ya hapo..kuna ndege mbovu moja kati ya hizo zilizopo...ilikuwa ina tatizo la radar...tukashauri wawe makini katika kuagiza...ndege ikasimama siku zaidi ya 6.bila kuangali sh ngapi wamepoteza kulaza ndege...ikaagizwa spare
gafla ikaja kituko cha matairi ya AIRBUS...mi nafikiri mh waziri kuna umuhimu wa kuwafanyia kazi moja kwa moja kwa maslahi ya tanzania...viongozi kama hawa...wanaamua kulindana na hata katika kuchaguana wanapeana wenyewe wakiamini hata wakiaribu hakuna atakaewagusa..je kuna umuhimu wa kuendelea kutoa hela kwenye kampuni hii???

MH WAZIRI: WA MIUNDO MBINU

Tunaomba kama rais alivyosema kwa TPA majina atawakilisha na kama mkurugenzi akishindwa apewe waziri akishindwa waziri aambiwe yeye imeshindakana awafanyie kazi...tunaomba mh waziri wa miundo mbinu embu rekebisha hiki kitengo wawe na heshima na kampuni hii.....na kama utashindwa kumwagiza mkurugenzi mkuu basi tunaomba upeleke matatizo haya kwa mh RAIS awaondoe watu wanaochezea pesa kama hawa
BAYA ZAIDI
Pamoja na kuleta vifaa tofauti,,pamoja na kulipia kodi kutoa..kulipia usafiri mpaka leo hii aijulikani hivyo vifaa yaani hayo matairi yako wapi..na hiko kifaa tofauti kiko wapi..na hivi sasa wameagiza kingine tena kama walicholeta lakini ilabda watafaikiwa kuagiza kinachotakiwa

Watanzania tuwe na uchungu na nchi yetu..tuache kulndana kwenye ujinga na kuifanya serikali kukataa tamaa ya kuisaidia kampuni hii...mh mkurugenzi mkuu tunarudia tena kama utaendeleza kulindana wakati watu wanaharibu pesa ovyo hivyo tunakupa mwezi wa nne hakika yanarudi yaliotukumba december

kila la kheri
 
Matatizo kama hayo ndio yanayo yaua mashirika yote ua Umma, hakuna uwajibikaji! simpo, wa Tanzania hatujajuwa maana ya kuwajibika na yule ambae anawajibika ipasavyo kazini, huambiwa ''lione hilo lina jidai ujanja''.

Watu ambao hawa wajibiki na wamo katika kututia hasara wananchi (kwani hizo pesa wanazo hasarisha ni zetu walipa kodi), waufungwe milele. Na wale mafisadi, wauliwe, kwani huo ufisadi wao ndio unasababisha vifo vingi vya waTanzania, Kwa mwenye kufikiri ataelewa nasema nini.
 
kuna umuhimu wa watu kuwajibishwa ili mashirika ya umma yawe na uhakika wa kuendelea kusurvive,vinginevyo JK atuambie haya mashirika ameweka kwa ajili ya wafuasi wake kujinufaisha
 
Back
Top Bottom