Jamaa_Mbishi

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
8,071
2,000
Radio Tanzania/ TBC FM wao ndio Wana archive kubwa kabisa ya nyimbo za zamani, kwani bendi zote za muziki, vikundi vya taarab na kwaya vilirekodi kwenye studio za RTD.

Kuna nyimbo nyingi sana hazipatikani YouTube wala sehemu yoyote Ile, hivyo Basi wapenzi wa muziki ya kwetu hatuna pa kulipata muziki Ile.

Kipindi Kama Tuimbe Sote cha kwaya, kila asubuhi. Tumbuizo asilia, kipindi cha Michael Karembo cha nyimbo za asili. Kipindi cha mashairi cha Malenga Wetu, kipindi cha Mama na Mwana cha Debora Mwenda, Muziki wa Mwambao na vingine vingi tulivipenda, ila Leo hatuna namna Tena ya kujikumbusha.

Namshauri mkurugenzi wa TBC alifanyie kazi Jambo hili.

Bujibuji Ngosha Jasu
Naunga mkono hoja
 

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
62,561
2,000
Pamoja na nyimbo za zamani wana pia hotuba na matukio ya zamani ambayo kwa sasa ya atafutwa sana na sisi vijana ili kuweza kujifunza na kujua nini kilicho kuwa kinatokea na kuendelea kipindi hiko tuweze kulinganisha na sasa ili kwenye na kukosea tujisahihishe.

Nimejaribi sana kutafuta hotuba za all hasani mwinyi lakini hakuna kama sio chache sana, ila TBC wanazo .

Kwa hiyo naunga mkono hoja, huyo mkurugenzi wa TBC anapaswa kuliangalia hili kwa jicho lingine.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa hawatundei haki. Wao ni hazina ya Taifa, lakini wamelala, wanadhani wapo ili walipwe mishahara tu
 

Insigne

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
2,668
2,000
Mimi naomba nyimbo zetu za mchiriku za zamani, Aisee napata shida sana kuzipata

Hata hizi za juzi tu za Genarali Lupozi(Juma Mpogo) na zenyewe sijui ziko wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom