Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
62,561
2,000
Radio Tanzania/ TBC FM wao ndio Wana archive kubwa kabisa ya nyimbo za zamani, kwani bendi zote za muziki, vikundi vya taarab na kwaya vilirekodi kwenye studio za RTD.

Kuna nyimbo nyingi sana hazipatikani YouTube wala sehemu yoyote Ile, hivyo Basi wapenzi wa muziki ya kwetu hatuna pa kulipata muziki Ile.

Kipindi Kama Tuimbe Sote cha kwaya, kila asubuhi. Tumbuizo asilia, kipindi cha Michael Karembo cha nyimbo za asili. Kipindi cha mashairi cha Malenga Wetu, kipindi cha Mama na Mwana cha Debora Mwenda, Muziki wa Mwambao na vingine vingi tulivipenda, ila Leo hatuna namna Tena ya kujikumbusha.

Pia kuna hotuba za viongozi mbalimbali, tunahitaji kusikiliza.

Namshauri mkurugenzi wa TBC alifanyie kazi Jambo hili.

Bujibuji Ngosha Jasu
 
Percy

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
6,398
2,000
Kwa sababu wao sio wamiliki halali wa hizo nyimbo. Haki zote zinabaki kwa watunzi na waimbaji, wenye hizo nyimbo wana haki ya kuwashtaki hao tbc kwa pesa ndeefu tu endapo watafanya hivo bila makubaliano.

Wataishia kuzicheza tu kwenye media ila kuzisambaza kwenye digital platforms sahau!

Hata ITV wamefanya productions nyingi tu za wasanii ila kuziweka mitandaoni hawathubutu.
 
Kwe kipindi kile hatukuwa na sheria ya haki miliki. Hivyo Basi mmiliki wa hizo kazi ni Radio Tanzania
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,359
2,000
Mpaka leo sielewi kwanini TBC Radio hawarudishi kile kipindi cha Tuimbe Sote ili watu wa Kwaya nao waweze kupata jukwaa na fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Sasa hivi kuna mtangazaji anaitwa Mbazigwa Hassan anakipindi cha kama dakika kumi anakiita "Tuimbe pamoja" kisha anaweka kanyimbo kake kamoja basi kipindi kimeisha!!!

Nakumbuka kipindi cha "Tuimbe Sote" kilikua kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi kuanzia saa nne na robo asubuhi mara baada ya taarifa ya habari na matangazo ya vifo

Pale ndio watu waliweza kuwajua Kapten John Komba na mwenzie Gasper Mapunda. Wakati huo wakiwa na Kwaya ya JWT. Sauti zao za ujana zilikua zinapanda sana na walitoa nyimbo nzuri mno

Nyimbo zao kama "Tuyahifadhi mazingira", "Mawe ndio msingi wa nyumba," Awamu ya Kwanza na ya Pili, Mabadiliko Ulaya ya Mashariki, Tumpambe Ali Mwinyi na nyingine nyingi

Pia alikuwepo Mwalimu mmoja wa shule ya Msingi Kange kule Tanga kisha baadae akahamia Mkono wa Mara Morogoro jina nimemsahau kidogo. Huyu Mwalimua alirekodi nyimbo na wanafunzi wake zilizobamba na kutamba katika ulimwengu wa kwaya hapa nchini

Nyimbo zake ni kama ile Mtama wa baba waliwa mtama wa baba ni nini, Mtaje mtaje kijana aliyekupa mimba Sakina dada nk

Kuondoa kile kipindi kwa kiasi kikubwa kimepoteza vipaji vya watunzi na waimbaji wa nyimbo za kwaya. Sasa hivi kwaya imebaki kua kama muziki wa dini tu. Hata mashuleni ni kama wameacha kufundisha nyimbo hizi
 
Afadhali JamiiForums imetupa jukwaa, tuna sehemu japo kwa kiasi twaweza kuweka kumbukumbu za kale
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,359
2,000
Afadhali JamiiForums imetupa jukwaa, tuna sehemu japo kwa kiasi twaweza kuweka kumbukumbu za kale
Kabisa kabisa mkuu. JF ni faraja yetu

Tena jina lako(hapo ulipoongezea ubini) limenikumbusha jamaa mmoja alikua ripota wa RTD kutokea wilaya mojawapo za Arusha. Jamaa alikua akiitwa Simba Nyamaume Simba na akiunguruma sana kwenye kipindi cha "Majira" asubuhi au kile cha saa tatu usiku
 
Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
2,742
2,000
Radio Tanzania/ TBC FM wao ndio Wana archive kubwa kabisa ya nyimbo za zamani, kwani bendi zote za muziki, vikundi vya taarab na kwaya vilirekodi kwenye studio za RTD.

Kuna nyimbo nyingi sana hazipatikani YouTube wala sehemu yoyote Ile, hivyo Basi wapenzi wa muziki ya kwetu hatuna pa kulipata muziki Ile.

Kipindi Kama Tuimbe Sote cha kwaya, kila asubuhi. Tumbuizo asilia, kipindi cha Michael Karembo cha nyimbo za asili. Kipindi cha mashairi cha Malenga Wetu, kipindi cha Mama na Mwana cha Debora Mwenda, Muziki wa Mwambao na vingine vingi tulivipenda, ila Leo hatuna namna Tena ya kujikumbusha.

Namshauri mkurugenzi wa TBC alifanyie kazi Jambo hili.

Bujibuji Ngosha Jasu
P.Mayala anafaa kuwa mjumbe kulipeleka hili wazo kwa mamlaka husika
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,880
2,000
Radio Tanzania/ TBC FM wao ndio Wana archive kubwa kabisa ya nyimbo za zamani, kwani bendi zote za muziki, vikundi vya taarab na kwaya vilirekodi kwenye studio za RTD.

Kuna nyimbo nyingi sana hazipatikani YouTube wala sehemu yoyote Ile, hivyo Basi wapenzi wa muziki ya kwetu hatuna pa kulipata muziki Ile.

Kipindi Kama Tuimbe Sote cha kwaya, kila asubuhi. Tumbuizo asilia, kipindi cha Michael Karembo cha nyimbo za asili. Kipindi cha mashairi cha Malenga Wetu, kipindi cha Mama na Mwana cha Debora Mwenda, Muziki wa Mwambao na vingine vingi tulivipenda, ila Leo hatuna namna Tena ya kujikumbusha.

Namshauri mkurugenzi wa TBC alifanyie kazi Jambo hili.

Bujibuji Ngosha Jasu
Naunga mkono hoja
P
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,851

Tangu ameondoka Tido Muhando,
Hili shirika limekuwa kama limekufa.
Walimtoa Tido ambaye ana uzoefu kwenye media,wakamuweka Profesa kutoka UD ambaye anauzoefu katika kufundisha,matokeo yake,shirika limeshuka kwa ubora kuliko hata ilivyokuwa TVT,hakuna mada Wala vipindi vya maana,limebaki kama shirika la propaganda za ccm
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,763

Idea nzuri sana ,watapiga pesa sana za Youtube! Sema ndiyo hivyo TBC wamejaa wazee ambao hawajui chochote kuhusu digital labda kina GANGANA wawasaidie.
 
Hahaha Ayoub Ryoba analiingiza chaka Shirika la Utangazaji.
 
Kiby79

Member
Feb 1, 2021
64
125
Radio Tanzania/ TBC FM wao ndio Wana archive kubwa kabisa ya nyimbo za zamani, kwani bendi zote za muziki, vikundi vya taarab na kwaya vilirekodi kwenye studio za RTD.

Kuna nyimbo nyingi sana hazipatikani YouTube wala sehemu yoyote Ile, hivyo Basi wapenzi wa muziki ya kwetu hatuna pa kulipata muziki Ile.

Kipindi Kama Tuimbe Sote cha kwaya, kila asubuhi. Tumbuizo asilia, kipindi cha Michael Karembo cha nyimbo za asili. Kipindi cha mashairi cha Malenga Wetu, kipindi cha Mama na Mwana cha Debora Mwenda, Muziki wa Mwambao na vingine vingi tulivipenda, ila Leo hatuna namna Tena ya kujikumbusha.

Namshauri mkurugenzi wa TBC alifanyie kazi Jambo hili.

Bujibuji Ngosha Jasu
Wanachofanya ni kuziuza kupitia CD, siku moja nilikwenda kwenye banda lao la maonyesho pale 77, cd yenye nyimbo 10 inauzwa tsh.5000!!!
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,359
2,000
Idea nzuri sana ,watapiga pesa sana za Youtube! Sema ndiyo hivyo TBC wamejaa wazee ambao hawajui chochote kuhusu digital labda kina GANGANA wawasaidie.
Wapo wazee wenye kujua muziki na biashara ya muziki. Masoud Masoud kwa mfano. Huyu jamaa anajua muziki na nahisi TBC wana mu under utilize

Maktaba ya TBC haina mpinzani kwa Tanzani kwa utajiri wa kumbukumbu za kila aina ikiwemo muziki. Nina wasiwasi kama vijana wengi wanaweza kwa faida ya shirika.

Uongozi wa TBC ni bora ungejipanga na kukaribisha uzoefu kutoka kwa human resources zake na hata nje ya shirika juu ya nini kifanyike kupata thamani ya urithi na utajiri wa maktaba yao
 
Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
62,561
2,000
Tangu ameondoka Tido Muhando,
Hili shirika limekuwa kama limekufa.
Walimtoa Tido ambaye ana uzoefu kwenye media,wakamuweka Profesa kutoka UD ambaye anauzoefu katika kufundisha,matokeo yake,shirika limeshuka kwa ubora kuliko hata ilivyokuwa TVT,hakuna mada Wala vipindi vya maana,limebaki kama shirika la propaganda za ccm
Kosa la kiufundi
 
Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
4,365
2,000
Pamoja na nyimbo za zamani wana pia hotuba na matukio ya zamani ambayo kwa sasa ya atafutwa sana na sisi vijana ili kuweza kujifunza na kujua nini kilicho kuwa kinatokea na kuendelea kipindi hiko tuweze kulinganisha na sasa ili kwenye na kukosea tujisahihishe.

Nimejaribi sana kutafuta hotuba za all hasani mwinyi lakini hakuna kama sio chache sana, ila TBC wanazo .

Kwa hiyo naunga mkono hoja, huyo mkurugenzi wa TBC anapaswa kuliangalia hili kwa jicho lingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom