Kwanini TBC haituhabarishi kesi ya Mbowe na wenzake?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wadau wote tunajua TBC ni televisheni ya serikali Watanzania wote kodi zao pamoja na kodi za Mbowe na wenzake zinatumiwa na TBC.

TBC imekuwa inatangaza kesi mbalimbali lakini toka mahakama ya uhujumu uchumi ianze kusikiliza kesi ya Mh. Mbowe na wenzake hakuna hata siku TBC imeripoti juu ya mwenendo wa kesi hiyo wakati ni haki ya wananchi kuhabarishwa na chombo wanachokichangia kodi wananchi.

Naipongeza ITV kwa kutuhabarisha watanzania mpaka tumejua kuwa Mh. Mbowe na wenzake wananyimwa chakula hakika ni ukatili na unyama uliopitiliza.

Wenye mamlaka kumbueni dunia ni mapito mbinguni kila mtu atajitetea kivyake hakuna kusema ulitumwa au uliagizwa.

Gen. Sabaya licha ya kusema aliagizwa na wakubwa miaka 30 anaitumikia pekee yake.
 
Tutulie mapungufu haya Rais na Nape watayarekebisha. Ninaamini hivyo, TBC itakuja kubadilika, na wasipofanya hivyo Mkurugenzi ataingia kwenye shida kuna reformation kubwa inakuja.
 
Wameona ni kesi ya mchongo,wameona wasiifedheheshe serikali kwa ushahidi feki wanaouleta mahakamani.
 
TBC falsafa yake ni "Ukweli na Uhakika" tofauti na "ITV Daima".

Muwe mnaelewa TBC ni wa kweli
 
Wadau wote tunajua TBC ni televisheni ya serikali Watanzania wote kodi zao pamoja na kodi za mbowe na wenzake zinatumiwa na TBC.

TBC imekuwa inatangaza kesi mbalimbali lakini toka mahakama ya uhujumu uchumi ianze kusikiliza kesi ya Mh. Mbowe na wenzake hakuna hata siku TBC imeripoti juu ya mwenendo wa kesi hiyo wakati ni haki ya wananchi kuhabarishwa na chombo wanachokichangia kodi wananchi.

Naipongeza ITV kwa kutuhabarisha watanzania mpaka tumejua kuwa Mh. Mbowe na wenzake wananyimwa chakula hakika ni ukatili na unyama uliopitiliza.

Wenye mamlaka kumbukeni dunia ni mapito mbinguni kila mtu atajitetea kivyake hakuna kusema ulitumwa au uliagizwa.

Gen. Sabaya licha ya kusema aliagizwa na wakubwa miaka 30 anaitumikia pekee yake.
TBC siyo Tv ya umma
 
Back
Top Bottom