Kwanini Tanzania wasomi wengi ila ICT tunaongozwa na Wahindi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Tanzania wasomi wengi ila ICT tunaongozwa na Wahindi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dungulee, Oct 23, 2008.

 1. D

  Dungulee Member

  #1
  Oct 23, 2008
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Enyi Watanzania wenzangu hebu niambieni,KWANINI ICT TUMETAWALIWA NA WAHINDI?Jaribuni kuangalia kampuni zote Tanzania zinazojihusisha na mambo ya IT.Je wao wananini cha zaidi ya kutushinda sisi wazawa?kwanini sisi tuwe wafanyakazi wao wakati Uwezo wakujiendesha tunao?Tushauriane jamani,Au nyinyi hamuoni hilo?
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi mkuu wa ict katika wizara inayohusiana hayo ni mswahili kwa jina la dr zaipuma yonah , alitokea ttcl ,na kuna vitengo vingi tu vinaendeshwa na waswahili kama wewe waswahili wako sehemu nyingi sema maduka mengi ndio yanaendeshwa na wahindi au watu kutoka asia ukiangalia kwa makini kama vile maduka yote haya outlet yake ni moja nenda mitsumi angalia laptop - model hiyo hiyo utaikuta prince , utaikuta orchards utaikuta qprint na ikiwa na shida usiende maduka yote hayo kwa sababu na zao zitakuwa na shida mambo kama hayo

  kuna kitu nyeti pia kama tanzania internet service providers association hiyo ngo nayo wengi ni wahindi mpaka mwenyekiji wake ni muhindi data flow inadhibitiwa na wahindi hichi ni kitu cha kuangalia pia

  hata jana tulikuwa katika mkutano wa ict governance kulikuwa na wahindi chini ya 4 wengine wote walikuwa ni wazawa halisi naamini katika majadiliano ya jana tutafika mahali sasa kila kitengo kila idara itashikiliwa na mzawa na kuanzia hapo tutaendesha mambo yetu kwa uwazi zaidi .
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Duh sikuangalia jina lako vizuri wewe dungulee si ndio ulikuwa kule nyerere road unauza bidhaa za mambo ya internet au sio wewe ? Habari za darhotwire ndugu , ynaaa na salmaa hawajambo
   
 4. D

  Dungulee Member

  #4
  Oct 23, 2008
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  shy isiwe sababu mkuu ilikua zamani ila salmaa hajambo kabisa na wote pia wazima.Nipo sehemu hapa nchi jirani najaribu kama maisha nitaweza mana TZ usanii umezidi
   
 5. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #5
  Oct 23, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi wamesoma lakini hawapendi kujiajiri na kuingia kwenye sekta binafsi.Wanapenda wafanye kazi za kuajiriwa na kutoa tenda kwa wahindi kwa kupewa ten percent za kifisadi za asante kwa kutoa tenda.

  Wahindi wakisoma sana wanawaza kujiajiri.

  Pia waswahili hawajui kujipanga kuanzisha kampuni kubwa lenye nguvu kwa kujiunga pamoja kivikundi cha wataalamu tofauti waliobobea kwenye ICT.Kila mswahili hutaka aanzishe kikampuni chake cha ICT kidogo na mkewe au hawara yake.

  Wahindi wao wakitaka kuanzisha kampuni ya ICT hawawazi kuanza na kikampuni kidogo cha kuganga njaa kwa kuuza diskette.Hujipanga.Vikao hufanyika.Havifanyiki kwenye mabaa kama vya waswahili huku wanakunywa pombe na kujadili.Wahindi hukutana katika maofisi wakiwa serious kujadili namna ya kuanzisha kampuni lenye nguvu.Hutafutana wataalamu tofauti tofauti waliosomea fani tofauti za ICT na kukubaliana kuunda kampuni ya pamoja yenye nguvu kubwa kiutaalamu n.k kuanzia mwanzo inapoanza.Kwa hiyo ukienda kwenye kampuni zao utashangaa kama ni duka la ICT karibu kila unachotafuta kipo.Kama ni kampuni ya Software utashangaa ilivyo na wataalamu wengi maeneo kibao.

   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu, nilihisi kuwa unafahamu sababu... kumbe kweli.

  Cha kusikitisha ni kwamba, USANII huu umetapakaa kila kona na kila rika, katika kila uongozi na kila nyanja ya maisha. ..hapo sasa. The solution however lies within.
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ni kweli unachosema mfano mzuri ni maduka ya prince computers wao ndio wenye quantium computers , ndio wenye q print , ndio orchards , ndio vista computers ndio mzizima lazima wakushike
   
 8. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Kumbe hii tabia iko kwa waswahili wengi!
  .
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Si Tanzania tu ambako wahindi wamejazana kwenye IT.
  Hata hapa USA Computer Engineering wameishikilia wao wahindi, tena si wahindi waliosoma hapa wamesoma India, hapa walikuja kusoma PhD tu.

  Wenzetu walianza zamani kwenye hizi dulu wako masafa.
  Tofauti na sisi tunaopoteza muda kwa kuweka Mawaziri wapita njia kwenye wizara nyeti kama akina Mungai. Huwezi kuamka asubuhi na kuchukua mawazo ya mkeo na kwenda kugeuza mtaala wa elimu kana kwamba Wizara unayoiongoza ni kundi la Mistress wako!

  Si suala la kufundisha masomo sahihi kwa msisitizo tu, ni pamoja na kuwafundisha Watanzania kutafsiri elimu yao kwa vitendo katika level zote za kuhitimu.


  Sisi bado tupo nyuma mno.
  Si suala la watanzania kujiajiri kwenye hiyo IT ni suala la utamaduni wetu mzima. Somo la Entreprenear halituingii akilini kwa sababu ya jinsi tulivyolelewa sekondari na vyuoni.
  Mtaala wetu wa elimu ni ule wa kuelimika ili uajiriwe.
  Lakini hapo hapo utashangaa Ukisha hitimu Mijitu kibao yenye dhamana serikalini ndo inakutolea macho kwamba kazi hakuna ujiajiri.
  Kma vile tulivyokuwa tunalazimishwa kucrame majina ya mawaziri na kuwaimba kwenye nyimbo mahsiri na ngonjera, vivyo hivyo tunatakiwa kuimba kwa nguvu na juhudi zetu zote juu ya suala la kutafsiri elimu yetu kwa vitendo katika sekta binafsi.

  Tunahitaji JUHUDI ZA MAKUSUDI kujenga upya mtaala ukatao tutoa matongotongo ya kudhani kampuni ni lazima ziundwe na wageni kwani sisi waswahili ni watu wa kuajiriwa tu.
  Nijuacho mimi ni komja.
  Watanzania ni mabingwa wa kuanzisha Pet Business zisizo sajiliwa na zisizo na mwelekeo wa kukua.
  Bar, Saloon, Chips na Nyamachoma Vipanya nk.
  Hakuna tatizo lolote kwenye hizi Business tatizo lipo kwenye Vision na mission ya Business hizi. Hilo ndo tatizo tutakiwalo kulitatua kama taifa ,amii na mtu mmoja mmoja.
   
 10. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2008
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ICT tunaongozwa na wahindi kwa sababu ya lack of support from goverment for wazawa kwenye ICT sector, bangalore na cheap n' skilled indian labour kwenye ICT, 10% za mwindi kwenye kugombania tender, na mindset ya wasomi wetu kukimbilia kuajiriwa badala ya kujiajiri.... vile vile mwindi katupiga bao kwenye sector nyingi kuliko ICT pekee (manufacturing, pharmaceutical industry, trade, etc) so its not a big suprise that they also lead here, the solution lies in our leadership, with the government and it policies and the mindset of Tanzanians in the ICT sector. (WAtch Rwanda in the next coming years and you will see what i mean.)..
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wahindi nyie waacheni kama walivyo kuna watu wanaona wahindi kama hamnazo kwa kuangalia zile slum kule Mumbai......kweli walianza zamani na wanakimbia kwa kasi sekta ya It duniani kusema ukweli imeshikiliwa na whindi....

  Umemaliza kabisa mkuu......
  Mtaniwia radhi lakini watanzania wana utando wa kufikiria globally.....kila siku hizi ndio biashara wanazojua zitawalipa........kila mtu anataka kufungua bar
   
 13. M

  Mjasiliamali Member

  #13
  Oct 23, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lakini kumbuka kuwawatanzania wengi tuna kwendashule kwa ku cream, Ebuona MH.sana Karamagi anatamba amesoma lakini ukirudia. chini kabisa utakuta katika History, ya "O"Level, ime bainisha, kuwa wazee wetu kwa ushamba, ama elimuduni, ama kwakuogopa, na kudanganywa walisainishwa mikataba ya ajabu, lakini yeye Karamagi na wenzake. kwa kupanda majukwaani walijinadi kuwa wao wamesoma.na hatimaye wakasaini mikataba kamaile walio saini mababuzetu, je ali udhuria shule, au alipata elimu?
   
 14. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  The bigger, underlying question that begs to be asked here would be why is trade in Tanzania controlled by this particular small minority?

  One can invoke history and the lagacy of colonial favoritism but surely enough years have passed to redress that, and yet a proportionate equitability is not apparent. One must not ignore the genuine shrewd industriousness, frugality and sometimes sheer forcefulness if not damned crookedness -from unchaste political connections to the black market and piracy business- of many among the Indians.

  In a system as green as ours, maintaining the status quo and cycles of poverty and affluence may not turn out to be hard at all.When you couple this with a government that is shying away from empowering black Tanzanians (Iddi Simba and Uzawa anyone?) partly due to the complacency caused by a chummy assurance of support from the indian community, the reasons begin to mount.

  There are doubtlessly many more, but the above are apparent in a flash.
   
 15. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Swala la kusaini mikataba mibaya linaweza lisiwe na uhusiano na kusoma kwa sana kama lilivyo na uhusiano na rushwa.

  Mtu aliyesoma sana na aliyefaulu vizuri tu akiwa hana moral compass ya kukataa rushwa anaweza kusaini mikataba mibaya sana, ili mradi apate chake.

  Huyu utasema hajasoma?
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama hawa wahindi ni Watanzania tatizo liko wapi? Mwisho mtauliza kwanini wafanyabiashara wengi ni wachagga, kwanini sekta ina watu hawa au wale...? Ubaguzi una tabia mbaya sana.
   
 17. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  I get your point.

  I guess you will have no problem with a president and cabinet of "Tanzanians of Asian origin" right?

  I believe in the brotherhood of mankind and non-discrimination too, but if the Indians are locking everything, that would be discriminating (whether deliberately or inherently systemically) us non-Indians.

  There has to be a balance somewhere.
   
 18. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri sasa tunaelekea kwenye ubaguzi, kuna wahindi wengi tu ni wazawa. the issue here is not sisi or wao, the issue ni kwamba wewe hufikirii kuwa mjasiliamali ndiyo maana kila siku utakuwa unamuangalia successful indian origin entrepreneur na kumchukia. Let's think about starting our own ventures after graduations instead of serching employment from these indian origin entrepreneurs. Where are we going to get capital?, there is a lot of banks which can lend good business plans, lets be risk takers, use your fathers houses as collateral that will make you more careful not to fail the business. I think the argument here should be why most of educated people in Tanzania don't think of starting their own businesses?
   
 19. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #19
  Oct 24, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza siyo kweli kwamba Tanzania ina wasomi wengi katika fani ya ICT. Tanzania ina wababaishaji wengi. Ubabaishaji na usanii ndo umetawala sector ya ICT Tanzania. Watanzania wenye asili ya kihindi kidogo wako serious ingawa nao ni wababaishaji. wengi wamejikita katika kuuza bidhaa "commodities" tu ha hiyo inaweza kufanywa na mtu yeyote.
   
 20. D

  Dungulee Member

  #20
  Oct 24, 2008
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shy nimeona kashfa moja inakuhusu kwenye Story ya dada mmoja ameoitoa kwenye Blog ya issamichuzi.Hebu isome hiyo story ipo kwenye page ya kwanza kabisa Then nijibu kama nikweli ama noo mana watoto wote hao nawafahamu
   
Loading...