Kwanini Tanzania wanauza kwa 'dollar' sio 'shillings'?

Natalia

JF-Expert Member
Jul 3, 2011
4,324
1,892
Bunge linafanya nini kwa swala hili na wizara ya fedha inasemaje? Na wanamchi wana mpango gani na swala hili?
 
Nadhani wanaifananisha na dola, ndio maana kutumia dollar ni sawa tuna mazoea ya kutumia sana dola

mkuu serikali imelala wafanyabiashara wako kazini
 
Bunge linafanya nini kwa swala hili na wizara ya fedha inasemaje? Na wanamchi wana mpango gani na swala hili?

Ni ulofa tu, tumepiga kelele we wenzetu wameziba masikio. Tusubiri awamu ya Fisadi papa ipite.

BTW ... ... Yoyo huwa unawatetea sana hawa mafisadi kulikoni?
 
Basi tufunge BoT na tutumie Federal Reserve Bank, kwani hali hii haipaswi kuruhusiwa inaifanya fedha yetu kukosa thamani zaidi. Wakati fulani serikali ilizuia nadhani iko sheria inayokataza ndiyo maana hata makampuni ya simu na DSTv yalikubali na sasa yanapokea Tsh. Tatizo ni lile lile serikali imelala
 
Nch hii haina sheria. Kila mmoja anafanya anachohisi kwake ni sahih. Nakir hatuna serikal.
 
Bunge linafanya nini kwa swala hili na wizara ya fedha inasemaje? Na wanamchi wana mpango gani na swala hili?
wengine wanasema ni soko huria.........kumbe ni holela........kutumia dola nayo ni sababu inayoifanya thamani ya shilingi kushuka.....
 
Hivi ni wakati gani........nchi ina-declare KUFILISIKA?..........naomba kuelimishwa.........
 
Hivi ni wakati gani........nchi ina-declare KUFILISIKA?..........naomba kuelimishwa.........
Iki default kwenye madeni yake nadhani na ikiwa wameshindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi,bajeti nk.I stand to be corrected.
 
Ni kinyume cha sheria.Hii hutokana na kushuka thamani ya shilingi.Inflation ya Tsh ni very high ingawa serikali inalazimisha shilingi isishuke thamani.
 
Kiufupi ni kwamba Shillingi letu limekosa thamani ya kuitwa sarafu kwa thamani halisi ndio maana wafanyabiashara na watu wengine wanafanya transactions in US dollar na bado hadi itakapofika thamani ya dollar ya marekani moja ni sawa Tshs milioni moja ndio tutatia akili kwani tukisema we watu hawatusikilizi wacha mambo yakorogeke vizuri ndio tutatia akili sawa sawa.
 
350-million-dollars.jpg

Wee Faizafoxy acha kutudanganya usidhani sisi ni watoto kihivyo. Ona, kazi kucopy and paste tu, sijui huo mkaratasi umeuokotea wapi, maana hata sio bongo. hamna lolote upuuzi tuu.
 
Wanauza vitu kutumia dola u wanaset bei kutumia dola?
Hakuna tofauti kama wanaset bei kutumia dola tena ndo inaongeza ufanisi, kwa sababu dola iko stable kama nikiweka bei ya $10 kisha nikatumia exchange rate kukupa bei in shillings nakuwa ninaepuka kubadili bei daily kufuatana na up and down za shillingi.

Kubadili bei kuna cost zake, hasa katika packaging na advertising, kwa vile dola iko stable nakuwa naepuka cost hizo.
 
Wee Faizafoxy acha kutudanganya usidhani sisi ni watoto kihivyo. Ona, kazi kucopy and paste tu, sijui huo mkaratasi umeuokotea wapi, maana hata sio bongo. hamna lolote upuuzi tuu.
Huna hata haya, wala hujui vibaya. Ni wapi ulipoona nimesema hiyo ni bongo au Tanzania?

Hata Victoria Falls huijui iko wapi? Mnhhh, halafu wewe ndio great thinker? Unanshangaza!
 
Back
Top Bottom