Kwanini Tanzania tunaingiza (Import) samaki kutoka nje?

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,873
"Shehena ya samaki wenye sumu kutoka nchini China wateketezwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi Jijini Dar Es Salaam.

Zoezi hilo lilofanyika Machi 11, 2019 limesimamiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina.

Samaki walioteketezwa wanafikia Tani 11 ambapo inaelezwa thamani yake ni zaidi ya TSh Milioni 60 milioni, ni baada ya kubainika kuwa samaki hao wana kemikali ya Zebaki yenye madhara kwa jamii na inaweza sababisha Saratani na kuharibu uzazi."

Nilipona hii taarifa nilianza kufuatilia kwanini tunaingiza samaki kutoka nje ,changamoto nini ikiwa tuna Bahari,Maziwa na Mabwaya yenye samaki wazuri na wengi.

Mh.Luhanga mpina akiwa bungeni wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya uvuvi 2018/2019 alisema " Maji ya Tanzania yaani mito ,maziwa na bahari wana samaki walioivaa (Harvestable fish) tayari kwa kuvuliwa takribani tani 2,736,248 (Milioni mbili laki saba na elf thelathini na sita ,mia mbili na arobaini na nane).

Hapo hapo Gazeti la "The citizen" liliwahi muhoji katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi Mh.Yohana Budeba ,akasema kuwa Tanzania,Tunavua samaki tani 336,821(laki tatu na elfu thelathini sita ,mia nane na ishirini na moja),Kwa mwaka.

Ambapo akasema ni pungufu sana, tani hizi hadhikidhi mahitaji ya samaki wanaohitajika kwa matumizi ya ndani ambao ni tani (730,000) laki saba na elfu thelathini .

Huku kukiwa na upungufu wa tani (480,886 ) laki nne na elf themanini ,mia nane themanini na sita).

Hii ina maana sio kwamba tuna uhaba wa samaki nchini ,tuna maziwa ,Bahari, na mabwawa yana samaki wa kutosha ambao ni harvestable fish takribani tani 2,736,248 (Milioni mbili laki saba na elf thelathini na sita ,mia mbili na arobaini na nane).kauli hii iliwahi zungumzwa pia Naibu waziri wa Uvuvi Abdallah Ulega.

Kinachofanya sisi kuendelea kuvua samaki wachache wasio kidhi mahitaji nini ?

Ukisoma taarifa ya ofisi ya Takwimu (NBS-National Bureau of statistics ) na ukisikia kauli ya Naibu Waziri wa uvuvi Mh.Abdallah Ulega na waziri wa uvuvi pia Mpina wanasema bado tuna njia za uvuvi wa zamani na kienyeji,uhaba wa vifaa vya kisasa vya uvuvi ,uhaba wa fedha kwa wavuvi kuvua kisasa,ukosefu wa elimu na mafunzo .

Unapata jibu kuwa sio kwamba hatuna samaki wa kutosha ,tunao wengi sana ila njia ya uvuvi tunaotumia ndio sio bora na ya kisasa !

Utatuzi wa changamoto hii nini ?

Utatuzi wa changamoto hii kwa maoni yangu,ili kuwezesha upatikanaji wa samaki wa kutosha wenye kukidhi mahataji ya soko la nje na ndani ni kutatua hizo changamoto, wavuvi wapewe elimu ,tujenge vyuo vingi vya uvuvi, tutafute vifaa vya kisasa vya uvuvi,(Mfano,tununue Meli yetu ya uvuvi), tujenge vituo vingi vya uvuvi wa kisasa ,wavuvi wadogo wadogo wapewe mafunzo na njia bora za uvuvi ,wasiishie kunyanganywa nyavu tuu ,waoneshwe nyavu zipi zinafaa kwa uvuvi (wakopeshwe hizo nyavu bora).

Ila jambo la kushangaza sana! Kitakwimu Tanzania tunaingiza (Import) samaki tani 24000 za samaki kwa mwezi kutoka China,Vietnam na India ili kuweza kukidhi mahitaji ya ndani .Mfano ,2016 Tanzania tulilazimika kuingiza samaki kilo.million 13.2 ,kukidhi mahitaji!

Kupitia Gazeti la "The citizens" Dec 19/2017 katibu mkuu wa wizara ya uvuvi na mifugo ,yohana Madebe ,alisema Tanzania inanufaika na kuingiza samaki kutoka nje katika njia tofauti tofauti ,kwanza uingizaji wa samaki huongeza mapato kupitia Lesensi zinazotolewa,Mrabaha wa uingizaji (Import royalties) na pia husaidia kuziba upungufu wa samaki ( fill fish deficient gap), kutokana kuwa Tanzania tunavua kidogo tofauti na mahitaji ya ndani na nje.

Hatuwezi kuendelea zaidi kwa kutegemea tozo kwa uingizaji wa samaki ambazo tunazo na tunauweza na sisi kusafirisha zaidi nje kuwauzia kama tutakubali kuumia kidogo tutatue changamoto zilizopo hasa kuwa na meli yetu ya uvuvi na kusaidia hawa wavuvi wadogo wadogo kuvua kisasa.

Tutafaidika zaidi mfano.Taarifa ya NBS inasema 2016 Tanzania ilisafirisha kiasi cha kilo million 39.691 cha samaki na nchi ilipata mapato ya nje kiasi cha $257.257 million ,sawa na shilingi billion 526.228 za kitanzania (2016).

Ambapo kwa taarifa ya BOT wanasema mwaka 2016 samaki iliingiza fedha za kigeni kushinda mazao yote ya pamba,chai,katani, karafuu ambayo yaliingiza sh.billion 337.44 .

Taarifa ya NESR National environment statistic report ya 2017 ,inasema kuanzia 2001 hadi 2016 ,Tanzania imeingiza kiasi cha trillion 5.8 kwa kuuza samaki nje !

Hii ina maana kuwa kama tutakuwa serious kama taifa ,tukafumba macho tukanunua meli ya kisasa ya uvuvi ,kwa kuwa tuna akiba ya samaki takribani tani million 2 na laki 7 katika maji yetu nchini ,meli hiyo inaweza kuongeza kiwango cha upatikanaji wa samaki chenye kutosha ndani na nje na kuingizia Taifa kipato zaidi ya hivi tunvyoingiza.

Samaki wanaweza kuwa ndio bidhaa inayoingiza fedha za kigeni sana kushinda bidhaa nyingi tukichukua mfano wa mwaka 2016 ,kwa mujibu wa BOT.

Shukrani,Mungu ajalie tupate meli yetu,Mungu ajalie tufunze na kuwasaidia wavuvi wetu wadogo wadogo.

Abdul Nondo.

abdulnondo10@gmail.com.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nondo, jiangalie sasa hivi nguo ulizovaa - kwa nini umevaa mtumba toka Taiwan wakati Morogoro kuna vitenge ambavyo ungeshona shati zuri sana - kwa nini umevaa sandle za uchina wakati Dar kuna sandle nyingi nzuri za kimasai

Badilika kwanza kisha kosoa wenzako
 
Nondo, jiangalie sasa hivi nguo ulizovaa - kwa nini umevaa mtumba toka Taiwan wakati Morogoro kuna vitenge ambavyo ungeshona shati zuri sana - kwa nini umevaa sandle za uchina wakati Dar kuna sandle nyingi nzuri za kimasai

Badilika kwanza kisha kosoa wenzako
Dogo akujiangalia wakati anaandika UZI mkuu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maziwa, mabwawa sijui mito sijui bahar tunavyo na vyote vina samaki! inakuaje mnaagiza nje? waacheni wale wenyewe kweli Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu. Tusha zoe kuagiza wacha tuletewe sumu tule tufe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe dogo sasa unataka kuharibika. Tuko wengi tunaku admire kwa ujasiri wako wa kutetea haki, tafadhali usianzishe mada kwa kusoma theory kwenye vijitabu. Kuna mada ziko far above your grasp! Mada za mambo ya uchumi sio zako. Hakuna nchi inayojitosheleza. China wana import mpaka soy beans kutoka USA na wao ni wazalishaji wakubwa wa hiyo kitu. Supply ya bidhaa nyingi Tanzania hazikizi demand. Jiulize wewe mwenyewe kama una familia, kwa nini unaenda kununuwa vitumbua au mkate wakati mchele na unga wa ngano unao ndani?
 
Nondo, jiangalie sasa hivi nguo ulizovaa - kwa nini umevaa mtumba toka Taiwan wakati Morogoro kuna vitenge ambavyo ungeshona shati zuri sana - kwa nini umevaa sandle za uchina wakati Dar kuna sandle nyingi nzuri za kimasai

Badilika kwanza kisha kosoa wenzako
Ninyi buku 7 hamshauriki kwa vyovyote vile.nondo abadilike kivipi ???
Badala ya kumwambia rais na mawaziri wake wabadilike sasa unamwambia abdul nondo abadilike !!!
Tatizo lililopo serikali ya awamu ya tano haishauriki .
Ukiishauri unaambiwa ,wewe ni mpinzani.
Abdul nondo ashawahi kusema yeye si mwanachama wa chama chochote cha siasa.lakin ninyi maccm mnalazimisha eti anatumiwa na viongozi wa upinzani.
Nondo ni mwanaharakati wa kisiasa na ataendelea kuikosoa na kuishauri serikali kwa mstakabali wa taifa whether you agree or not.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utamu wa Sera bora kabisa za chama cha kijani miaka 57 ya Uhuru ,wameshindwa hata hili la samaki .
 
Bongo nguo bado sanaa. Hata nguo za kushona asilimia 99 vitambaa vyatoka nje.

Pia hata uwekezaji kwenye Hilo eneo ni sifuri.fikilia hata vyuo vyetu vikuu havina hizo kozi.najua ni UD pekeee hivi karibuni ndio wameanza kufundisha kozi ya textile technology (Sina kumbukumbu nzuri,na jina la hiyo kozi.

Mtu anaweza jibu nguo watu wanaangalia ubora ! Na samaki unaangalia nini ? Hadi unanunua wa China ambao wanasumu ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abdul nondo ashawahi kusema yeye si mwanachama wa chama chochote cha siasa.lakin ninyi maccm mnalazimisha eti anatumiwa na viongozi wa upinzani.
Nondo ni mwanaharakati wa kisiasa na ataendelea kuikosoa na kuishauri serikali kwa mstakabali wa taifa whether you agree or not.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe naye nyumbu kweli - ni wapi kati ya maneno niliyoandika nimesema Nondo yuko chama fulani? Niliandika hivi "Nondo, jiangalie sasa hivi nguo ulizovaa - kwa nini umevaa mtumba toka Taiwan wakati Morogoro kuna vitenge ambavyo ungeshona shati zuri sana - kwa nini umevaa sandle za uchina wakati Dar kuna sandle nyingi nzuri za kimasai

Badilika kwanza kisha kosoa wenzako


Fikiri kwa kutumia akili, kazi ya tumbo inajulikana!
 
Hakuna nchi inayojitosheleza. China wana import mpaka soy beans kutoka USA na wao ni wazalishaji wakubwa wa hiyo kitu. Supply ya bidhaa nyingi Tanzania hazikizi demand. Jiulize wewe mwenyewe kama una familia, kwa nini unaenda kununuwa vitumbua au mkate wakati mchele na unga wa ngano unao ndani?

Hoja yako ingeanzia hapa ingependeza......
Abdul Nondo Kuitwa Nondo Muachie Nondo na wenzake....
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom