Kwanini tanzania tuna viongozi wasiojua wanachokifanya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tanzania tuna viongozi wasiojua wanachokifanya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicazius, May 8, 2011.

 1. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa sana la viongozi wa serikali wasiojua nini wanafanya na wala hawana upeo na nini kifanyike kuleta maendeleo badala yake wamekuwa ni watu wa kulalamika kila kukicha bila kujenga hoja.

  Mfano: Mbunge mmoja ametoa comment hii kwenye facebook:

  Nanukuu

  "Hivi ni kweli CHADEMA hawajui sababu za ukweli za mfumuko wa bei Tanzania? Kwa nini wameamua kuzunguka nchi nzima wakitafuta umaarufu wa bei chee kwa ku-take advantage ya uchumi mbovu wa kidunia? Napata wasiwasi kama watu hawa hawajui sababu na miongoni mwao kuna wabunge 'makini! ' Au wamekumbwa na upofu wa kutafuta umaarufu kwa gharama yoyote ile?"

  Mwisho wa kunukuu.

  Hivi mtu kama huyu, tena mbuge aliyesoma anaweza kulisaidia vipi jimbo lake kuleta maendeleo ikiwa kama upeo wake wa kufikiria na kiasi hiki, na kama wabunge wasomi ndiyo wapo hivi Je wale ambao hawajasoma kabisa watakuwa vipi na ndiyo wanatuwakirisha katika chombo muhimu kama bunge, nashindwa kuelewa nabaki nachanganyikiwa kabisa.

  Ndugu zangu JF hebu nisaidieni kumsaidia Mhe. wetu ili aweze kubadirika na kuwasaidia wananchi wake.
   
 2. O

  Omr JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna wengine wamesema Rais apigwe mawe, na huyo unamuonaje??
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  ndugu..usiogope kuweka link,kama yy (MB) kaimwaga facebuk nadhani tuwekee hapa tumwendee hukohuko....habari za kiintelegensia zinaonesha kwamba Wabunge/viongozi wasio na hoja wala mashiko wengi hukimbilia facebuk...tunataka tuwaendee hukohuko kuwapa-sure!! so tuwekee link plzeee!!tumjue ni nani huyo,usiogope!!
   
 4. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Omr: hiyo habari nimeisoma hapa JF na mpaka sasa hakuna source ya ukweli, Pls nipe link au source inayoonyesha kama Mhe. amesema kauli hiyo... Kama ni ukweli Mhe amesema hakika hayupo sawa hata kidogo na tunahitaji kumweleza kama Watanzania, lakini siwezi kutoa any comment mpaka nipate source ya uhakika, naamini javini tupo wengi ukweli utajulikana.

  Bila kutoka nje ya mada, wewe unasemaje kuhusu huyu Mhe kutoa kauli kama hii, tena msomi kuliko mamillioni ya Watanzania... unategemea lolote kutoka kwake kwa kauli kama hizi...
   
 5. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sizinga: Sina haja ya kuogopa, kwani sina ugovi naye, ila huu ni ukweli na lazima usemwe. Huyu hapo chini:

  Dokta Hamisi Kigwangalla
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hamisi anafahamika ni mbunge aliyeingia bungeni kwa mchakakto wa kuomba mkataba wa mgodi jimboni kwake kwa mbwembwe kubwa,na alionekana kuwa na hoja yenye nguvu na ni mwelewa kwa kile akifanyacho
  Lakini ktk hili la uchumi nadhani nae amelichukulia kisiasa zaidi kwa kuingia ktk kukemea CDM kutafuta umaarufu,lakini kwa upande wangu ninge mweleza Mh Hamisi kuwa umefika wakati sasa wa Wabunge wasomi kama wao kuwa washauri wazuri wa Mwenyekiti wa chama ili kuweza kufanikisha nchi na serikali yake kuondoka ktk dhahama ya kulaumiwa na wapiga kura wake
  Kwa mfano kwa sasa bei za mafuta machafu USA ZIMESHUKA KWA 10%,Na hata bei ya mazo kama kakao na mengine pia yameshuka kwa kasi ile ya ajabu,na imefikia wakati sasa viongozi wa nchi husika wanajiuluza kwa nini hili limetokea na pia wanajiuliza watumie njia ipi kutatua

  Tatizo tulilo nalo TZ hatuna hata njia mbadala ya kupambana na huo mfumuko wa bei kwa kuwa watawala wengi wapo ktk biashara na wanafurahia mfumuko wa bei kwani ndio unao wapa utajiliu

  Angalia kenya serikali iliamua kupunguza hata bei za mafuta ya taa na nyingine angalau hilo linawapa moyo wapigakura kuwa kuna kazi inafanyika na kwa watawala wetu
  Lakini kwa upande wetu hatuna majibu yaliyo sahihi na hata wawakilishi wetu nao wapo ktk kulalamika kana kwamba hawaweza na hawana njia mbadala ya hata kupunguza tatizo

  Nilitegemea Mh Hamisi angekuja na hoja ya nini kifanyike ktk kuondokana ama hata kulipunguza hili tatizo tulilonalo,lakini nae na Usomi wake amekuwa mpiga ngoma na mwimbaji amesahahu hata kazi tuliyo mtuma ya kutuwakilisha juu ya kushauri nini kifanyike

  Mh mbunge angalia Mbunge wa kagera juzi alikuwa ktk wakati mgumu jimboni kwake si kwa kuwa wapiga kura wanachuki nae la hasha ni kutokana na Kauli zake awali sasa sinamla yeye mwenyewe,ubabaishaji,na longolongo nyingi kuliko vitendo,hivyo vyote vinasababisha wapiga kura wakutolee uvivu na kukueleza kinaga ubaga

  Nakuasa Mh jitahidi kuwa na majibu mazuri pindi ukutanapo na wapigakura wako juu ya swala hili la ugumu wa maisha kwani wapiga kura wasasa wanatambuwa mbichi na mbivu,ukileta longolongo na kujifanya kuwa ni mshabiki wa uchumi na sio mtatuwaji wa matatizo ya kiuchumi jiandae kukupambana na nguvu ya maswali ya umma yasiyo vumilika mbele ya macho yako

  Mungu ibariki TZ
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Siyo kila anayeitwa kiongozi ni kiongozi. Wengi ni watawala. Mtawala hahitaji kujua matatizo ya watu anaowatawala bali anachotakiwa kujua ni mbinu za kuwatiisha.
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Tupe maelezo yanayojitosheleza,ni mbunge gani alietamka kwamba RAISI apingwe mawe.
   
Loading...