figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Heshima kwenu wakuu,
Ili Tanzania na watanzania tufanikiwe lazima tujenge utamaduni wa kutoa. Vinginevyo tutasikia maendeleo kwenye TV. Nchi ya Tanzania haina Taasisi ya kiserikali hata moja ya kutoa misaada. Hata maandiko yamesema.
Ukweli ni kwamba Watanzania walio wengi hata kwa umoja wao kama nchi, hawana roho ya hisani. Yaani kutoa msaada na kujitolea.
Kwanini hatuna utashi wa kutoa misaada pale kwenye matatizo. Kidogo tunajitahidi kwenye misiba kwenda kuzika wapendwa wetu. Je, msaada lazima utoe kwa mtu unaye mfahamu?
Mfano:
Tanzania kulitokea tetemeko kule Kagera, lakini Serikali iligoma kuwasaidia wahanga lakini kenya waliweza saidia kwa kuleta mahindi ambayo sijui yaligawiwaje.
Kuna sehemu kuna ukame wananchi hawana chakula lakini serikali haisaidii.
Tuna watoto yatima wengi lakini ukiacha watu wa dini, na taasisi mbalimbali, huwezi kuona mtanzania wa kawaida anapeleka mchicha, maharage, mahindi nk. Anadai hana kitu.
Ombaomba barabarani Tanzania ukiangalia unakuta wanarushiwa mia mia mbovu hadi mia mbili. Halafu anatoka hapo anaenda kunywa bia za elfu 50.
Mtaani Tanzania kuna wasomi wengi, wanashinda wamekaa vijiweni. Huwezi kusikia wanaenda kujitolea sehemu ambazo elimu yao inahitajika.
Kuna watu wana nguvu, lakini hawawezi kwenda kujitolea kujenga, kutengeneza miundombinu ya kijamii.
Hii roho mbaya ya Watanzaniabna Serikali yao inatoka wapi?
Wamarekani wanashika nafasi ya pili kama watu wenye kuongoza katika kutoa misaada kwa wenzao. Mtu anayehesabika hutoa misaada ni yule anayesadia mtu mwenye shida ambaye mtoa msaada hamfahamu, anayechangia pesa za hisani, au anayejitolea kufanya kazi bila malipo. Nafasi ya kwanza ulimwenguni inashikwa na raia wa Myanmar.
Kwenye orodha niliyoipitia ambayo ni matokeo ya utafiti ya kampuni ya Gallup, Kenya inashika nafasi ya 12, Uganda ya 26, na Tanzania inashika nafasi ya 57 kwa matokeo ya utafiti wa mwaka 2016.
Ni rahisi kusema kuwa Wamarekani wana uwezo mkubwa wa fedha kuliko Watanzania, kwa hiyo ukweli kwamba pesa za hisani zipo nyingi zaidi nchini Marekani si suala la kushangaza.
Lakini hoja ya aina hiyo inapuuzia ukweli kwamba moyo wa kutoa au wa kujitolea hauna uhusiano wowote na utajiri. Moyo wa kujitolea ni uamuzi unaoongozwa na jinsi gani mtu mmoja amepima tatizo lililopo mbele yake na kuamua kuchukua hatua kupunguza tatizo hilo kwake au kwa jamii inayomzunguka.
Kila mara tunafikiwa na maombi ya kuwa miongoni mwa wale wanaochangia kumaliza matatizo kadha wa kadha. Na, hali inaporuhusu, kila mara tunafanya uamuzi wa kusaidia au kutosaidia.
Mara kwa mara napokea kadi ya kuchangia sherehe ya aina moja au nyingine, na tabia iliyojengeka miongoni mwetu ni kuwa asiyechangia sherehe hizo anajipambanua kama mtu ambaye hapendi kushirikiana na wanajamii wenzake.
Kwa hiyo baadhi ya Watanzania tunachangishana mamilioni ya pesa kwa madhumuni ya kuandaa sherehe kubwa na karamu za vyakula, vinywaji, na muziki kwa siku moja.
Na kwa siku zilizosalia ndani ya mwaka tunaitisha vikao kujadili matatizo mbalimbali ambayo yanatukabili ndani ya jamii zetu.
Kwenye sensa ijayo ingefaa kuwauliza Watanzania wanachangia kiasi gani cha pesa kwenye sherehe kila mwaka ili tukae kutafakari kama hayo mabilioni ya pesa yasingeweza kuleta manufaa makubwa zaidi kama yangeelekezwa kwenye kuboresha elimu, au afya zetu, au kwenye miradi ya kutunza na kuhifadhi mazingira.
Wapo watakaosema kuwa ni serikali ndiyo inayopaswa kuhakikisha kuwa raia wake wanapata huduma zote za jamii. Kinadharia utaratibu ni huo, lakini ukichunguza hali halisi utabaini kuwa hata kwenye nchi tajiri serikali inahitaji mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikina nayo kuziba mapengo ya huduma mbalimbali za jamii.
Watu wenye asilia ya India ndo wanatuokoa katika kutoa misaada na kujitolea. Wanasiasa wanatoa misaada lakini nia kubwa inakuwa nibkwa manufaa yao ya kisiasa ndo maana hawatoi misaada kimya kimya.