Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Tenga? Tunakwama wapi kama taifa?

W
Huyo tenga na mbwana ilitokea tu kama kunguru kumnyea binaadamu. si kana kwamba eti enzi hizo kulikuwa na vipanga kunako soka. Na ili kulithibitisha hili ebu nitajie graduate wengine japo watatu mbali na hao wawili! Siku zote mpira wake masela😀 haruna moshi,kelvin yondani,juma nyoso etc.
walikuwepo wengi tuu, kina marehemu Mwalusako, kina Mtemi Ramadhani, Kina Tenende , nk
 
Huyo tenga na mbwana ilitokea tu kama kunguru kumnyea binaadamu. si kana kwamba eti enzi hizo kulikuwa na vipanga kunako soka. Na ili kulithibitisha hili ebu nitajie graduate wengine japo watatu mbali na hao wawili! Siku zote mpira wake masela😀 haruna moshi,kelvin yondani,juma nyoso etc.
Stamili Mbonde,Mohammed Banka nk.
 
Tangu zamani na hata sasa kulikuwa na wapo wachezaji wenye elimu ya kutosha. Mfano mbali ya Leodgar Tenga kuna Denis Mdoe aliyekuwa anachezea Red Star ya Dsm, Mtemi Ramadhani, Ibrahim Malekano wa Simba, Lawrence Mwalusako aliyekuwa beki wa Yanga.
Madundo Mtambo nk
Ni wengi
Chuo cha ushirika Moshi kilikuwa na timu ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wanafunzi wa chuo hicho.
Hata hivyo mtu kama amekosa elimu kwa sababu ya mpira basi aongeze juhudi mara dufu kujiweka vema kimaisha na ikibidi ajiendeleze kielimu.
 
Back
Top Bottom