Kwanini Tanzania inakimbilia nyasi bandia wakati nchi zilizoendela zimekataa kuzitumia viwanjani

Yusuf Kashaju

Member
Oct 20, 2019
57
89
Wasalaam,

Nimeshangaa kuona kupitia bajeti ya 2021/22 serikaliri inaondoa kodi kwenye nyasi bandia ili kuhamasisha matumizi yake nchini, cha kushangaza sera hii imeungwa mkono na wabunge kama kwamba hawana uelewa wa masuala ya kimataifa ya mpira, hata TFF sikuwasikia wakitia neno wakati wanajua FIFA na mataifa ya Magharibi wamekataa kutumia nyasi hizo kwenye viwanja vya mpira wa miguu.

Kuna wakati fifa ilitaka zitumike wakati wa mishindano ya wanawake, nao wakakaa kuwa FIFA isiwafanyie majaribio. Sasa sisi Tanzania tumefanya utafiti ili kujua kwa nini FIFA hawazitumii na mataifa ya magharibi kwanini hawakubali kutumiwa kwa nyasi hizo bandia ktk viwanja vyao?
 
Nyasi bandia zinaleta majeruhi sana kwa wachezaji. Na ndiyo maana baadhi ya vilabu barani ulaya wanaziondoa na kuweka nyasi asilia au kuweka mchanganyiko yaani asilia na bandia.
 
Nyasi bandia inachubua sana ngozi za wachezaji. Hasa ukiteleza unaweza acha ngozi chini
 
Ni sababu za kiafya zaidi kwa wanamichezo kuliko za kimazingira.

TFF hawawezi kupinga matakwa ya serikali kwa sababu bado ktk nchi hii michezo huchanganywa na siasa.

Wale akina Karia sio muda mrefu tutawaona wakichangamkia fomu za ubunge kwa tiketi ya ccm kwani kwao mpira wanatumia kama ngazi tu ya kwenda huko.
 
Wasalaam,

Nimeshangaa kuona kupitia bajeti ya 2021/22 serikaliri inaondoa kodi kwenye nyasi bandia ili kuhamasisha matumizi yake nchini, cha kushangaza sera hii imeungwa mkono na wabunge kama kwamba hawana uelewa wa masuala ya kimataifa ya mpira, hata TFF sikuwasikia wakitia neno wakati wanajua FIFA na mataifa ya Magharibi wamekataa kutumia nyasi hizo kwenye viwanja vya mpira wa miguu.

Kuna wakati fifa ilitaka zitumike wakati wa mishindano ya wanawake, nao wakakaa kuwa FIFA isiwafanyie majaribio. Sasa sisi Tanzania tumefanya utafiti ili kujua kwa nini FIFA hawazitumii na mataifa ya magharibi kwanini hawakubali kutumiwa kwa nyasi hizo bandia ktk viwanja vyao?
Kwa Sababu itapunguza Athari ya kuwapo kwa viwanja Vingi vyenye pitch mbovu, hata hao wazungu walipambana na ubovu wa pitch kwa kubuni hizo nyasi bandia.Tofauti ni Nyakati, itafika Nyakati tutaziacha kama wanavyoziacha wao sasa, hilo lisikutishe.

Uendeshaji wa Nyasi Asili ni Gharama sana, ushawahi kuwa na kabustani tu home ukaona bill ya maji inavyopanda?Sasa fikiria liuwanja loooote ulimwagie Maji, wamiliki kwao inakuwa changamoto
 
yusuph Kashuja umeuliza swali fikirishi sana,hata waandishi wa habari za michezo,wachambuzi nimewasikia wakisifia serikali kuondoa tozo ilhali wanajua kabisa kinachoendelea kuhusu nyasi bandia.
 
Kwa Sababu itapunguza Athari ya kuwapo kwa viwanja Vingi vyenye pitch mbovu, hata hao wazungu walipambana na ubovu wa pitch kwa kubuni hizo nyasi bandia.Tofauti ni Nyakati, itafika Nyakati tutaziacha kama wanavyoziacha wao sasa, hilo lisikutishe.

Uendeshaji wa Nyasi Asili ni Gharama sana, ushawahi kuwa na kabustani tu home ukaona bill ya maji inavyopanda?Sasa fikiria liuwanja loooote ulimwagie Maji, wamiliki kwao inakuwa changamoto
Hivi nyasi bandia zinazui magugu na nyasi nyingine kuota chini, je hapo suala la ajira umeifikiria kwa vijana wetu maana siyo kupunguza gharama peke yake. Je majerui kwa wachezaji, maana udongo mchezaji anapokita udongo na nyasi ni rahisi kusambaa, sio rahisi kwa nyasi bandia maana zimesukwa kama mkeka.
Je athari kwa mazingira umeyangalia, maana zinatengezwa katakana plastics, je zitaoza au ndiyo tunatafuta balaa lingine la mazingira kama mifuko ya plastics
 
loftus check aliwahi vunjika mguu kwenye nyasi bandia
Ni ajali tuu, embu tuambieni ni wachezaji wangapi wamejeruhika Kaitaba, uhuru ,Azam comlpex na Nyamagana kutokana na uwepo wa hizo nyasi bandia, mtueleze na athari za kimazingira zilizoletwa na uwepo wa hizo nyasi kwenye viwanja husika hapo juu
 
Back
Top Bottom