Nchi nyingi za kiafrika ikiwemo Tanzania zinaitwa ni nchi za dunia ya tatu au zisizoendelea kwa sababu zifuatazo:.
- Rais kushindwa uchaguzi kwa kupata kura chache,lakin yeye ndio anakuwa Rais wa nchi.
- Mtu mwenye akili timamu kuendesha gari au pikipiki au baiskeli usiku bila kuwasha taa.
- Kufaulu mitihani darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika.
- Kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mbunge bila kujua kusoma na kuandika.
- Kuua watu kwa pistol au bunduki hadharani ,lakin unaachiwa huru kuwa huna hatia.
- Rais kuteua watoto wote , ambao baba zao walishawahi kuwa viongoz na kuwapa uwazir bila kuzingatia uwezo wao.
- Mtu mwenye akili timamu kusimamisha gari yake barabarani na kujisaidia haja ndogo bila wasiwasi.
- Mabinti au vijana wengi kumaliza vyuo huku hawajui walichosomea.
- Ukijuana tu na Rais au wazir mkuu au makamo wa Rais unateuliwa kuwa mkuu wa mkoa au wazir bila kuzingatia weledi wako.
- Ajali kuwa nyingi barabarani na kugharimu maisha ya watu wengi huku wakuu wa Polisi wakizidi kupandishwa vyeo.
- Watumishi wote waliofukuzwa kwa kuwa na vyeti fake ,kulipwa mafao yao.
- Wazir wa nishati kusimama bila aibu na kutaja sababu za uongo za kukatika kwa umeme kila siku.