Kwanini Tanzania inahujumu undugu Afrika ya Mashariki?

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,528
47,774

Sambamba na sakata ya ‘Brexit’ ya Uingereza kujitenga jumuiya ya Ulaya ‘European Union’ (EU) yamkini Tanzania inajitia katika mwiba huo wanaojichoma waingereza.

Tukitathmini kwa kina mwenendo wa Tanzania katika swala zima la uwiano, umoja na maendeleo ya watu wa kanda hii ya Afrika Mashariki tunaona imekuwa kikwazo kikubwa kwa lengo hili nyeti.


Cha kushangaza ni kwamba mmoja wa waanzilishi wa jumuiya hii ni baba wa taifa hili yaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Zaidi ya yote makao makuu ya jumuiya ya Afrika mashariki yalianzishwa mjini Arusha kule kule Tanzania na kudumu hadi leo. Akiwa na baba wa taifa la Kenya marehemu Mzee Jomo Kenyatta sambamba na Rais Milton Obote walianzisha umoja huu wa kanda.


Hatahivyo ndoto ya muungano thabiti wa Afrika mashariki umetatizwa na majirani wabongo kaka blaza kwa sababu tutakazobainisha hapa.


SEE ALSO :Dar revokes licences of forex bureaus

Kizungumkuti ni kwa Tanzania kuwa na woga na Kenya kwa kuona kuwa watamezwa kiuchumi na jirani alopiga hatua


kubwa za uchumi na siasa. Kimsingi ni wivu wa kuona maendeleo ya Kenya unaowazuzua watanzania.Tatizo hili lilianzishwa na Nyerere mwenyewe aloshindwa kuinuwa taifa lake kiuchumi alivyofanya Jomo.


Kivipi?


Nyerere alisoma na kupata elimu ya juu ya chuo kikuu maarufu kule Scotland cha Edinbourgh katika masomo ya siasa na uchumi. Sasa badala ya kutilia mkazo elimu na kuanzisha msingi kwa wananchi wake alipiga


mbiyu ya kuendeleza Kiswahili kwa umoja wa nchi.


SEE ALSO :Ex-CEO of Bank M charged with fraud, money laundering

Changamoto ya maendeleo


Je, itawezekana vipi kuboresha watu wasio na elimu hususan kiuchumi? Ni kweli Kiswahili kimeondosha ukabila na


kuleta mshikamano wa mtanzania lakini bado wamesalia ujingani katika karne hii ya teknolojia.


Nyerere wa kabila la kizanaki kutoka kijiji cha Butiama kule Bukoba, alisomeshwa na wamishonari kidini na kielimu.Mbona hakutaka watanzania wasome kama yeye? Kunapofuka moshi kuna moto. Nyerere alihofu watanzania


wakisoma wataerevuka na kutisha uongozi wake.Alitaka wawe wajinga ili awatawale na kuwazuzuwa Nyerere alifaulu kwani watanzania mpaka leo wanamuenzi.


SEE ALSO :An escape that shouldn't cost you much

Twakumbuka nyimbo fulani ya kale kule bongo inayojumuisha mapenzi mazito ya wabongo kwa Nyerere. Mistari ni hii:-


“Ndugu Juliasi Kambarage Nyerere si kwamba yeye tu….ni kiongozi halisi…bali pia ni mwalimu.. alo na kipaji cha ukarimu…. Na hakuna asiye mfahamu…anayeshirikiana nasi katika shidana raha...”


Kimsingi Nyerere aliwateka akili watanzania kifikra akitumia masomo ya kifalsafa na siasaalosoma kule Edinbourgh.


Nyerere mjanja alianzisha siasa za ujamaa na kujitegemea na kuwarundika watanzania katika ufukara wa ukulima wa


kikale. Aliogopa kukuza wasomi bali alitaka wajinga kuwaongoza. Aghalabu alizinduwa azimio la Arusha kama sheria kuu ya kikatiba.Akifuata siasa za kidikteta na za kiimla za Mao Tse Tung wa China, Nyerere alisuta ubepari kabisa asijuwe kuna nukta fulani nyeti katika mfumo huu ambao Kenya walifata.


SEE ALSO :Traders say quality of Tanzanian tea improves

Malumbano


Nyerere katika kilele cha uhasama na Kenya alitaja Kenya kuwa jamii ya mtu kula mtu mwenzake. Akimjibu Kenyatta kwa kuiita Tanzania nchi ya mtu asiyekula chochote! Nyerere mwenywe alikiri mwishoni mwa awamu yake kuwa ujamaa haukuleta ufanisi kama kwanza alofikiria.Alijidanganya kuwa Tanzania ingekua ama Uchina asijuwe uchanga wa taifa lake ukilinganisha na China pevu.


Matokeo yake watanzania walifukarika wakawa madutu na washamba wakiwa ndani ya nchi tajiri ya raslimali sufufu lakini bila ya wasomi na watalamu wakugunduwa na kukuza. Huku Nyerere akilemaza watanzania Jomo Kenyatta aliendeleza elimu kwa wakenya akisisitiza matumizi ya kiingereza kama lugha ya kimataifa na kiuchumi.


Kenya ilpiga hatuwa huku vijana wakisoma kwa bidii wakati watanzania wakipepeta kiswahili kule katika vijiji vya ujamaa na kujitegemea.


Nyerere aliboresha udikteta wa chama kimoja cha TANU kisha cha mapinduzi (CCM) ikifata mfumo wa Uchina.


Wakiwa bila ilimu ya fikra watanzania walimuabudu Mwalimu aliyekuwa akiwachekesha kwa hotuba zake za mahanjam na uchali zilojaa inadi, sitiazai na hekaya za Abunuasi. Kenya ilipiga hatua kubwa kiuchumi na


Nyerere alifahamu hili na hata kuitambuwa Kenya kama nyota ya jaha na hata kujisahau na kuitaja katika hotuba zake.


Mfano dhahiri ni pale vijana wengi wa Tanzania walivyotaka kwenda nje ya nchi kule Ulaya na Marekani kwa masomo na makazi kama wenzao wakenya walivyosaidiwa na serikali yao. Nyerere alipochoka na kerohili aliwaambia watanzania hao hivi (nukuu):-


Ulaya iliyo Afrika


‘Uraya (ulaya) yanini? na uraya iko hapa hapa jirani (Nairobi)!.. nendeni hapa uraya !’alisema huku kama kawaida


yake akishangiliwa kwa nderemo na vifijo naye akihitimisha kwa kicheko chake kirefu cha gugumizi’ hee..hee..heee!’


Nyerere ambaye alibarikiwa kwa kuzungumza kwa haraka kama cherehani ya stima aliheshimiwa kupita kiasi na jibulake kwa swali lolote lilichukuliwa ukweli mtupu na hakuna wakupinga kwani baba kasema!


Viongozi wa chama tawala cha CCM kama Ngumbare Mwiro, Rashid Kawawa na kina Abeid Jumbe walishikilia sera za mwalimu kikamilifu na kuzitekeleza. Marais waliofuata kama Benjamin Mkapa, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Mrisho Kikwete na kwa kiasi fulani wa sasa John Pombe Magufuli walifata sera za Mwalimu. Aghalabu mfano wa m’buyu mkongwe ilikuwa kazi kung’owa kabisa mizizi ya ujamaa alozika Nyerere katika ardhi ya Tanzania.


Twaweza kusema Kikwete ambaye alikuwa kiongozi kijana wakati wa Nyerere alifuzu sera na hata tabia za babu yake huyo.


Alipokuwa Rais Kikwete alitawala kama Nyerere na kuzidi kulemaza Tanzania hususan kiuchumi


kwani ufisadi ulizidi kukithiri huku yeye akichekacheka tu! Kikwete alipenda sana kusafirinje ya nchi kwa kigezo cha kusoma mambo ya nchi ziloendelea.


Kuna wakati alitembelea Uhispania na kwende katika uwanja wa timu maarufu ya soka Barcelona kule Camp Nou. Aliporudi Tanzania aliisifu uwanja huo wa mpira ulivyopendeza eti ni mzuri!


Ni wakati wa Kikwete Tanzania ilipojitenga kwa muda na jumuiya ya Afrika mashariki na kujiunga na umoja wa kusini


mwa Afrika yaani SADEC.



 
Hivi kati ya Tanzania na Kenya wapi kuna mafukara wa kutupwa au majengo ya kina Kenyatta na baadhi ya wanasiasa na wazungu wote mnajiona tayari matajiri.
Tanzania imejaa mafukara. Watanzania wengi huishi katika nyumba za tope zilizoezekwa na nyasi. Sidhani kama wengine wamewahi ona bati maishani mwao. Very ugly houses in the villages
 
Ebu tutolee uchafu huu hapa. Kwanza kiswahili kilichoandikwa ni kibovu. Mpangilio wa muundo, maudhui na muktadha ni mbovu kupindukia. Pia herufi za maneno zimekosewa. Mfano, badala la kuandika suala anaandika swala.

Inaonekana muandishi hata historia ya Afrika Mashariki haijui... eti KIKWETE aliamua kujitoa jumuiya ya Afrika Mashariki na kujiunga na nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Huyu mpumbavu hajui kuwa sisi ni founding members wa SADC. Kama ilivyo kwa EAC kuwa founding members, ndivyo ilivyo kwa SADC. Hatujajiunga na SADC kama Rwanda walivyojiunga EAC. Mpumbavu tu ndiye atakayefuatilia maandishi yaliyokosa mashiko na ueledi kama gazeti hili.

Lingine ni kuwa no matter WHAT sisi tutamuenzi Nyerere daima, kwa kuwa hakutuuza au kuiuza NCHI YETU kwa wanyonyaji kama baba YENU Kenyatta alivyofanya. Amewatupa kwenye utumwa. Mnalia lia lkn hakuna la kufanya.
 
Mk254...umeandika maada ndeefu ila hukuongozwa kwa utashi wako na weredi..ila umeongozwa na ubinafsi plus chuki zidi ya Tanzania...hulaumiwi sana na wakosoaji wa maada yako kwasababu hayo yote mmerithi toka kwa mwasisi wa Taifa lenu..(kenya)
Naamini ingawa sina uhakika sana Mk254 pamoja na umri wako kua mkubwa hivyo huna kibanda wala mahali pa kujenga kibanda..maanake utakufa ukiacha familia yako ikiishi kwenye nyumba za kupanga huku ukijisifu kwa majirani wako wa tz kua umejengewa nyumba nzuri na wazungu...na unathubutu kuwadharau wenzio kwa nyumba zao na aridhi yao..
Hapa namaanisha asilimia kubwa ya aridhi ya kenya ipo mikononi mwa wakenya wachache...asilimia kubwa ya wakenya hamna chenu na kama raia hunauwezo wa kumiliki aridhi katika taifa unaloitwa ni taifa lako basi jua utaifa wako upo mashakani..in short ulisha uzwa bila ww kujijua au ww ni mzamiaji katika taifa hilo
Kenya ni kweli inauchumi mkubwa kwa kulinganisha nchi zote za EA..swali wakenya kama wakenya mnaufaidi..yaani Cake ya taifa mnakula sawa....
Au nyinyi mnapiga vigele gele tu walaji ni wengine?
So MK254 niwashauri wakenya masikini kama ww mpiganie aridhi kwanza na sio mtake muungano wa East africa mkitegemea mtapata aridhi tz..
Nakukumbusha tu Uraia bila kuwa na haki ya kumiliki aridhi na sawa na kukaa kwenye nyumba ya kupanga then ukajiona na ww ni mwenye nyumba..
 
Mimi nilisoma shule ya kwanza ya Sekondari kujengwa baada ya Tanganyika kupata uhuru. Ni shule ambayo ilikua na kila kitu ambacho shule bora inatakiwa iwe nacho. sasa sijui mtoa mada anamaanisha nini anaposema Nyerere aliwanyima wananchi wake Elimu. Kusoma shule wakati wa Nyerere ilikua bora kuliko sasa ingawa nafasi zilikua chache. Nyerere alitaifisha shule nyingi za makanisa kama Pugu(St Francis ) , Minaki(St Andrews), Alliance(mazengo ), St benedicto (Kigonsera ) n.k ili ziwe za serikali na watu wa dini zote wasome maana serikali ya kikoloni iliacha shule chache za serikali.

Wahadhiri wangu wengi walikua ni wanufaika wa scholarship za serikali, na wengi walienda Urusi, Ujerumani na Uingereza. Baba yangu mdogo alifaidika na hii program ingawa hajaifanyia chochote Tanzania iliyomsomesha, kaishia kubaki huko nje hata baada ya kustaafu.

Sera ya ujamaa ilikua lazima ifeli kwa sababu mbalimbali. Ukitoa Nyerere ni watu wachache sana walikua wanaelewa nini maana ya ujamaa, kuuamini na kuuishi. Kwahiyo kufeli kwake kusifanye tumwone kuwa hakua na nia njema na Tanzania. Nadhani Nyerere alikua anaamini katika regional integration kuliko kiongozi yeyote Afrika mashariki maana umoja ndio msingi wa ujamaa.
 
Mada imeandikwa kwa kiswahili kibovu na mwandishi hajui vitu vingi anaandika kwa mihemko na research za social media, mfano nyerere katokea Bukoba,kweli jamani?
 
Mk254...umeandika maada ndeefu ila hukuongozwa kwa utashi wako na weredi..ila umeongozwa na ubinafsi plus chuki zidi ya Tanzania...hulaumiwi sana na wakosoaji wa maada yako kwasababu hayo yote mmerithi toka kwa mwasisi wa Taifa lenu..(kenya)
Naamini ingawa sina uhakika sana Mk254 pamoja na umri wako kua mkubwa hivyo huna kibanda wala mahali pa kujenga kibanda..maanake utakufa ukiacha familia yako ikiishi kwenye nyumba za kupanga huku ukijisifu kwa majirani wako wa tz kua umejengewa nyumba nzuri na wazungu...na unathubutu kuwadharau wenzio kwa nyumba zao na aridhi yao..
Hapa namaanisha asilimia kubwa ya aridhi ya kenya ipo mikononi mwa wakenya wachache...asilimia kubwa ya wakenya hamna chenu na kama raia hunauwezo wa kumiliki aridhi katika taifa unaloitwa ni taifa lako basi jua utaifa wako upo mashakani..in short ulisha uzwa bila ww kujijua au ww ni mzamiaji katika taifa hilo
Kenya ni kweli inauchumi mkubwa kwa kulinganisha nchi zote za EA..swali wakenya kama wakenya mnaufaidi..yaani Cake ya taifa mnakula sawa....
Au nyinyi mnapiga vigele gele tu walaji ni wengine?
So MK254 niwashauri wakenya masikini kama ww mpiganie aridhi kwanza na sio mtake muungano wa East africa mkitegemea mtapata aridhi tz..
Nakukumbusha tu Uraia bila kuwa na haki ya kumiliki aridhi na sawa na kukaa kwenye nyumba ya kupanga then ukajiona na ww ni mwenye nyumba..

Mbona unateseka kunijibu mimi, nimeleta bandiko la gazeti wacha kunijadili, jadili kilichoandikwa kwenye gazeti, mimi siye mwandishi wala sio mwandishi wa habari.
Jifunze kutumia muda wako vizuri.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom