Kwanini Tanzania hatuzingatii FANI aliyosomea Mtu katika ajira?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Ni kawaida kabisa hapa Tanzania kukuta watu wameajiriwa/teuliwa kwa kazi ambazo hawajazisomea eti kwamba watapata uzoefu kazini,Mfano wakurugenzi wa Taasisi za umma hata za binafsi.Daktari wa kutibu watu kuwa Mkuu wa Wilaya/Mkoa.Ili kuleta ufanisi si ni vyema mtu apewe kazi aliyosomea ili aweze kutimia ujuzi wake kwa maendeleo ya Taifa?Wana JF mnaonaje hili?
 
Nchi zingine wanajali sana FANI ya mtu katika AJIRA kwanini hapa Tanzania ni vigumu kufuata utaratibu?
 
Ni kawaida kabisa hapa Tanzania kukuta watu wameajiriwa/teuliwa kwa kazi ambazo hawajazisomea eti kwamba watapata uzoefu kazini,Mfano wakurugenzi wa Taasisi za umma hata za binafsi.Daktari wa kutibu watu kuwa Mkuu wa Wilaya/Mkoa.Ili kuleta ufanisi si ni vyema mtu apewe kazi aliyosomea ili aweze kutimia ujuzi wake kwa maendeleo ya Taifa?Wana JF mnaonaje hili?

Unataka ukuu wa wilaya/mkoa apewe nani? Kwani kuna mtu anasomea fani ya ukuu wa wilaya/mkoa? Na kuna some fields zinaingiliana na zingine.
 
At least asiwe somebody very technical!asiwe engineer,q.s,medical doctor.

kuna kitu kinaitwa 'MAN'S MISSLOCATION OF SKILLS'huwa inafika mahala tunahire wataalamu wakati tunao ila wamejiingiza kwenye siasa,au uongozi.

Walau asome hata sociology,pspa,hrm,na maungwine ungwine fulani hivi
 
Kujuana, undugu, makulaji, ufisadi, uchoyo, tamaa, n.k n.k n.k ndo jibu la swali lako!

NB; Nadhani hata kutothamini wataalam inaweza kuchangia, ila sina uhakika sana
 
Ni kawaida kabisa hapa Tanzania kukuta watu wameajiriwa/teuliwa kwa kazi ambazo hawajazisomea eti kwamba watapata uzoefu kazini,Mfano wakurugenzi wa Taasisi za umma hata za binafsi.Daktari wa kutibu watu kuwa Mkuu wa Wilaya/Mkoa.Ili kuleta ufanisi si ni vyema mtu apewe kazi aliyosomea ili aweze kutimia ujuzi wake kwa maendeleo ya Taifa?Wana JF mnaonaje hili?

MMARORO,
Ni kwasababu ya siasa, undugu, ukabila, n.k.
 
Ni kawaida kabisa hapa Tanzania kukuta watu wameajiriwa/teuliwa kwa kazi ambazo hawajazisomea eti kwamba watapata uzoefu kazini,Mfano wakurugenzi wa Taasisi za umma hata za binafsi.Daktari wa kutibu watu kuwa Mkuu wa Wilaya/Mkoa.Ili kuleta ufanisi si ni vyema mtu apewe kazi aliyosomea ili aweze kutimia ujuzi wake kwa maendeleo ya Taifa?Wana JF mnaonaje hili?

Tatizo liko kwa wasomi wenyewe wanapoanza kujifanya wanasiasa.... wakaacha kutenda taaluma zao na kutafuta vyeo vya kisiasa.Unategemea nini pale ambapo, Mhandisi anapotafuta ubunge au kuingia kwenye kupigania nafasi za juu katika vyama vya siasa?Kuna mtaalamu mmoja yeye aliteuliwa kushika wadhifa mkubwa sana ilhali tayari alikuwa kwenye eneo linalomruhusu kutumia taaluma yake.Alichokifanya ni kukataa kwa heshima ule uteuzi pamoja na kuwa angepata cheo, jina, marupurupu n.k.Lakini watu kama hawa ni wachache sana wenye kuthubutu kukataa.
 
Mimi sioni tatizo kwa sababu kazi hizo wanazopewa nyingi haziitaji taaluma bali skills za kuongoza/kutawala ambazo kmsingi mtu yoyote anaweza kuwa nazo. Ingekuwa tatizo kama Engineer unampeleka akawe Medical doctor or vice versa!
 
HIVI ni kweli skills hizi mtu yeyote anaweza kuwa nazo?
 
Chanzo kimoja ya hali hii ni mfumo wa promotion.Mfano Mwalimu mzuri wa fizikia tunamtunuku uheadmaster .Tatizo:in hierachy every employee tends to rise to his/her level of incompetence,habari ndo hio.
 
tatizo lawasomi wengi wa Tanzania linaanzia tangu mwanzo kwenye msingi, sio siri kama kuna wasomi ambao tangu wako Olevel walikuwa wanajua watakuwa kwenye field gani ni wachache sana, 95% ya watu mnaokutana chuo mnakuta mmengia kwenye kozi fulani just accidentaly, yaani kwa kifupi mtu anakuwa anataka degree tu alafu mambo ya kazi mbele kwa mbele, kwa hiyo wasomi wanaotoaka chuo kwa sababu ya misingi mibovu waliojiwekea kwenye taaluma wanakuwa tayari kwa kazi yoyote bila kujali taaluma yake na muda wake aliopoteza,
ni sawa mambo ya siasa ni ya kila mtu octor, injinia etc, lakini sidhani kwa nchi kama zetu za kimaskini ambazo wasomi wazuri wanapatikana kwa shida na kisha hao hao tunaamua kuwapoteza kwenye siasa, amfano angalia mtu kama Prof Sarungi, alikuwa ni mtu wa muhimu nsana kwenye sekta ya afya na kama serikali ilikuwa inataka kumtumia basi atleast wangemuweka kwenye angalau ushauri au kitu kama hicho kwenye wizara yake usika(afya)
wasomi wengi sana tanzania walioaribiwa na serikali, maghembe, Kapuya, mbilinyi, magufuli, mwandosya nk
sasa kwa sababu wasomi wa kweli ndio wanaingia kwenye siasa hata na wale wasiokuwa wasomi wameanza kununua ndegree na phd ili nao wafanane na wasomi wa kweli
ni mawazo yangu tu
 
lakini hili jambo liko wazi kwanini kulikuwa na chuo cha uongozi mzumbe wako watu wenye fani za utawala na uongozi hao wengepewa kipaumbele kwenye eneo kam hilo la wakuu wa wilaya kuliko kumpa daktari wakati wajua kabisa hata hao tulionao leo hawatoshi au mpang wa kuwapa wanajeshi wastaafu matokeo yake watu wanachapwa viboko nafikiri kuna umuhimu wa kuangalia taaluma za watu wapo walishasoma na bado wanasoma
 
Tatizo liko kwa wasomi wenyewe wanapoanza kujifanya wanasiasa.... wakaacha kutenda taaluma zao na kutafuta vyeo vya kisiasa.Unategemea nini pale ambapo, Mhandisi anapotafuta ubunge au kuingia kwenye kupigania nafasi za juu katika vyama vya siasa?Kuna mtaalamu mmoja yeye aliteuliwa kushika wadhifa mkubwa sana ilhali tayari alikuwa kwenye eneo linalomruhusu kutumia taaluma yake.Alichokifanya ni kukataa kwa heshima ule uteuzi pamoja na kuwa angepata cheo, jina, marupurupu n.k.Lakini watu kama hawa ni wachache sana wenye kuthubutu kukataa.

Mtu akikuuliza swali wewe unasoma ili iweje?. Kuacha longolongo na kujifanya mzalendo jibu la msingi litakuwa ni kujijengea misingi ya kuishi maisha bora. Sasa maisha bora yanapatikanaje?, jibu ni kuwa na shughuli inayolipa vizuri either ya kuajiriwa au ya kujiajiri. Ni kazi gani ya kitaalam Tanzania inayolipa zaidi ya Siasa? jibu unalo wewe.

Kitu cha msingi hapa si tamaa ya wasomi bali ni ubinafsi wa wanasiasa kujilimbikizia wao malipo ya kila aina na kuwasahau wataalam where "Rubbers hit the road" katika maendeleo. Kwa kuwa lengo la watu kusoma nimelifafanua hapo juu basi kinachofuata ni kwamba ukiona sahani hazikufikii na wewe unaingia jikoni labla waweza pata hata makoko au kuambulia uliomwagwamwagwa na wanasiasa.

What next na wewe ukiingia hutoki unalia hukohuko na kusahau kuwa nje umeacha watu wanasubiri sahani zitoke kama ulivyokuwa unasubiri wewe. Hawa ndiyo wanasiasa wetu. na kuona nani unamjua ili umvute ndani na yeye aje ale matunda ya wewe kuwepo jikoni, kwa kufanya hivyo huwezi kuangalia unayemvuta ana utaalamu gani bali je ni nani? "Nepotism"

Cha kufanya: Ili kuondoa utata huu, ni sharti kupunguza malipo ya wanasiasa yaendane na kazi wanazofanya na si kuwa na titles nyingi. Utakuta mtu ana title 10 na kila title inalipa kweli kweli, kama uwaziri, ubunge, ukuu wa mkoa, uenyekiti au ujumbe wa board n.k.

Tufanye kuwa waziri ni lazima asiwe mbunge, mkuu wa mkoa ni lazima asiwe mbunge au mwenye nafasi nyingine kwenye taasisi yoyote. Unajua Tanzania tunalalamikia ajira ngumu, ila tunashindwa jua kuwa ajira zipo ila watu wamezikalia tu kwa kujilimbikizia titles kibao.

Kama waziri anateuliwa toka nje ya wabunge ni dhahiri tusingeshuhudia wasomi kibao wakiingia kwenye vinyang'anyiro vya ubunge.
 
Last edited:
Ni kawaida kabisa hapa Tanzania kukuta watu wameajiriwa/teuliwa kwa kazi ambazo hawajazisomea eti kwamba watapata uzoefu kazini,Mfano wakurugenzi wa Taasisi za umma hata za binafsi.Daktari wa kutibu watu kuwa Mkuu wa Wilaya/Mkoa.Ili kuleta ufanisi si ni vyema mtu apewe kazi aliyosomea ili aweze kutimia ujuzi wake kwa maendeleo ya Taifa?Wana JF mnaonaje hili?

Maana ya kuwa na Degree ni kuwa na analytical thinking. Hakuna tatizo lolote kwa Dr. kuwa Mkuu wa mkoa. Kinachotakiwa ni kuwa na elimu. Kwa Dr. kuwa Mkuu wa mkoa, huyo Dr. ataweza kusaidia kutatua matatizo mengi ya afya ya wananchi wake wa Mkoa. However, kuna sehemu nyingine za kazi lazima mtu awe na elimu ya kile alichokisomea.
 
Back
Top Bottom