Kwanini Tanzania hatutengenezi magari?

Gari hizo zitanunulika tu hapana shaka ingawa kwa gharama za kuendesha kiwanda inatakiwa watu waweze kununua gari walau 100 kila mwaka.

Kibongo bongo kuna watu wanaendesha mpaka gari za million 600 barabarani tena private achilia mbali wenye gari za million 70-150 (prado,jeep cherokee,touareg,discovery series,land cruiser VX,LX) ni wengi mno na hio ni kwa dar tu achilia mwanza na Arusha.

Hivyo hilo swala la kudai kuwa watu hawatamudu gharama za kununua siliafiki kama kutakuwa na gari zinazoendana na vipato tofauti vya wananchi.

Wakiwa na plans nzuri mbona yanawezekana, unanunua gari mpya 0 kms under warranty safi kabisa. Nikupe mfano kwa hizi economical cars (gari pendwa) kama passo, swift cheap kabisa hata ukifanya evaluation ya kodi na gharama na manunuzi ya used kwa 2017 model haitozidi million 18 ushaitia mkononi na ni toleo la mwaka jana import kutoka japan.

Kodi ya passo.
View attachment 741947

Kodi ya suzuki swift.
View attachment 741948
Ni kweli kabisa mkuu, tatizo letu hua tunakosa uthubutu katika kuwekeza. kama raisi kathubutu kutumia trilioni mbili kasoro kwenye kipande cha Dar Moro nadhani pia itakua vyema kama taifa tukaingia ubia na kampuni yeyote tukaanza uzalishaji mkubwa.
Tunaweza kuanzisha kiwanda cha magari ya 650cc baadaye tukaja kwenye magari makubwa zaidi. Kinachotakiwa ni commitment tu. kama ni mtaji hisa tutanunua hata kama hisa moja itakua ni 50,000 tutajichanga hivyohivyo.
 
Gari mpya 0 km ni watu wachache sana wanaweza mudu.Hapa mbeya sijaona gari zaidi ya 10 new models za watu binafsi.
kuna watu wengi wanaendesha 0 km, ila siwezi kuwataja sababu ni kinyume na maadili kutoa taarifa binafsi za watu. lakini tukiamua tunaweza kutengeneza gari ndogo classic kwa bei ya milioni 30.
 
Ni kweli kabisa mkuu, tatizo letu hua tunakosa uthubutu katika kuwekeza. kama raisi kathubutu kutumia trilioni mbili kasoro kwenye kipande cha Dar Moro nadhani pia itakua vyema kama taifa tukaingia ubia na kampuni yeyote tukaanza uzalishaji mkubwa.
Tunaweza kuanzisha kiwanda cha magari ya 650cc baadaye tukaja kwenye magari makubwa zaidi. Kinachotakiwa ni commitment tu. kama ni mtaji hisa tutanunua hata kama hisa moja itakua ni 50,000 tutajichanga hivyohivyo.
Inawezekana kabisa na focus iwe kwa mauzo ya ndani ya nchi tu kwa kuanzia na badae target kuipeleka East Africa kulingana na ubora wa magari husika.
 
Jiulize ni nani anatakiwa kujenga hicho kiwanda,na yeye anapata ushirikiano upi?
 
Mpk tuwe na kundi kubwa la middle incone earners ndipo tutaweza kupata wananchi wengi watakao afford hizo gari tunazozitengeneza.
 
Nyumbu hujaziona gari zao tanzania tunatengeneza magari

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyumbu uwezo wao ni mdogo mkuu, angalia TATA walizindua kiwanda cha kuassemble nagari yao sijui ni nini kimezuia...wakati huohuo Rwanda inaassemble gari za Volkswagen.
How comes nchi ndogo kama Rwanda wanaassemble gari za kampuni kubwa kama Volkswagen lakini sisi tunashindwa kukomaa ata na TATA ambaye gari zake ni cheap.
 
Back
Top Bottom