Kwanini Tanzania haina uwekezaji wenye tija kama Mataifa mengine yaliyoendelea

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,912
Ukiangalia mataifa mengine utaona kwamba yamepiga hatua kubwa mno kimaendeleo kutokana na matumizi sahihi ya Rasilimali zao.

Botswana na Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE) especially Dubai au hata Libya utaona namna uwekezaji sahihi ulivyobadili kabisa maisha ya wananchi toka ufukara mpaka kuwa na hali njema kiuchumi.

Kabla ya kugundulika kwa mafuta 1950 UAE ilikua ni nchi inayotegemea mapato ya Uvuvi na bidhaa za baharini.

Lakini baada ya kugundulika tu kwa mafuta historia ya Taifa hilo ikabadilika na kuwa moja ya mataifa Tajiri.

Tanzania ukiachana na madini ya Tanzanite ambayo hayapatikani mahali kwingine popote duniani tuna madini na rasilimali nyingine ambazo kama zingetumika ipasavyo maisha ya watanzania yangekuwa bora.

Kwa miaka kadhaa sasa toka tunapata uhuru Taifa letu limekua likipokea wawekezaji katika sekta mbali mbali ambazo ukiachana na mapato kiduchu tunayoambulia kutokana na faida wanayopata maisha ya watanzania yameendelea kuwa duni na nchi bado ikitegemea mikopo na misaada mbali mbali kujiendesha.

Kwa muda mrefu tu dhahabu, almasi na Tanzanite vimekuwa vikichumwa bila ya kutunufaisha.

Inashangaza kwamba ukiachana na mali zote hizo bado sisi ni maskini.

Unabaki kujiuliza je sisi labda hatuna viongozi wenye uwezo na wazalendo??

Je, hatuna sera nzuri na pia hatuna watu wenye nia ya kuona Taifa likiondokana na umaskini??

Kwakweli majibu yanakuwa machache kwa maana Tangu Uhuru tumeshuhudia wawekezaji lukuki lakini hali ya maisha ya mtanzania haijawahi kuwa bora.

Kipato cha mtu mmoja mmona, ubora wa huduma za afya, elimu na miundombinu bado tu duni sana.

Kwanini uwekezaji haujawahi kubadili maisha ya mtanzania kama mataifa mengine?
 
Tofauti ni kwamba hapa Tz siasa zetu hazitabiliki. Kila Raisi anakuja na sera zake. Hamna muendelezo wa sera
 
Tofauti ni kwamba hapa Tz siasa zetu hazitabiliki. Kila Raisi anakuja na sera zake. Hamna muendelezo wa sera
Hili ni tatizo kubwa mkuu.

Maana ukiangali wenzetu huko wana viongozi ambao wanapigania haswa maslahi ya Mataifa yao ila kwa hapa kwetu naona kama viongozi wetu hawana uzalendo wanaangalia maslahi binafsi tu na wanaowazunguka.
 
Kwa sababu ya sera zinazobadilika badilika sana na mfumo mbovu wa kodi.
Wawekezaji wakubwa huwa wanahitaji utulivu na uhakika wa mitaji yao kwa muda mrefu.
 
Hapa kwetu Tanzania viongozi hawana vision na matamanio ya kuona watanzania wanakuwa na hali nzuri ya maisha.

Sana Sana wanaendeshwa na tamaa za matumbo yao na familia zao. Na hiyo 10% ndiyo inavuruga vichwa vya viongozi wengi sana. Wako tayari kusiani mikataba hata mahotelini bila hata ya kusomwa na wanasheria.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukiomba mikataba ipite bungeni lkn wapi. Sababu kubwa ni uroho. Wanaona wabunge wanaweza kuweka kauzibe.
 
Back
Top Bottom