Kwanini Tanzania haina Presidential Debate (Mjadala wa Wagombea Rais)?

Kessy Wa Kilimanjaro

JF-Expert Member
Jan 23, 2016
327
208
Leo nina swali tu: Kwanini Tanzania hatuna Presidential debate (Mjadala wa wagombea Raisi) kwenye uchaguzi tangia tupate uhuru.
 
Jibu ni kuwa hapa Tanzania au tuseme nchi nyingi za kiafrika hazina viongozi bali zina watawala....sasa ukitazama mtawala hana muda wa kujadili na mtawaliwa isipokuwa anaangalia au kubuni mbinu za kuendelea kumtawala mtumwa wake......
Na ndio maana hata maigizo ya uchaguzi yanapofanyika lazima kunakuwa na nguvu nyingi sana za kijeshi dhidi ya raia wanaoonekana wanataka viongozi na sio watawala....

Watawala siku zote wanaishi kwa wasi wasi kwani wanajua ubaya wanaoufanya kwa watawaliwa....na kila penye safari zao lazima ushuhudie wingi wa magari ya polisi yanayokwenda kasi.......

Huyu rais wa uruguay ndio mfano wa kiongozi na sio mtawala....
4f290e0ce1aae2f4dbcf357addb3e9e9.jpg
 
Mwaka 1995 Ulifanyika Mdahalo Kati ya Mkapa, Lipumba na Mrema, Mkapa na Lipumba walifanya Vizuri sana lakini kwa wakati ule kwa Ushabiki watu walidhani Mrema alikuwa Ni kiongozi mzuri, Mbona kama Kidogo tuingie choo cha kike akia mama!

Nashauri 2020 Uwepo Mdahalo, Kisha Uwepo na Mwingine special kwa Lugha ya Kiingereza (Official Languages Tanzania ni English and Swahili) Ambapo wagombea watazungumzia maswala ya nje na Uhusiano wa Kimataifa.
 
I strongly agree the debate should be both in English & Swahili
 
Leo nina swali tu: Kwanini Tanzania hatuna Presidential debate (Mjadala wa wagombea Raisi) kwenye uchaguzi tangia tupate uhuru.
Kwa sababu mwisho wa siku kura huwa zinaibiwa na matokeo kuchakachuliwa kwa ulinzi wa Bunduki, sasa hapo debate ya nini, ili hali Rais atapatikana kwa lazima.
 
Leo nina swali tu: Kwanini Tanzania hatuna Presidential debate (Mjadala wa wagombea Raisi) kwenye uchaguzi tangia tupate uhuru.

1995 kwny Uchaguzi Mkuu ilikuwa na Umri gani?

Mdahalo ulifanyika Kilimanjaro hotel na Benjamin Mkapa na Ibrahim Lipumba walionesha uwezo mkubwa wa kujieleza. Augustine Mrema alikataa kufuata ushauri na maelekezo ya kipi cha kuzungumza muda wote akawa anazungumzia Mashamba ya Chavda na Dhahabu alizokamata Airport. John Cheyo alikuja kishatangwa Kitwanga kadhaa.
Mdahalo hauna nguvu kwa sababu upigaji kura Tanzania hauongozwi na hoja za Maendeleo watu wanapiga kura kwa Mkumbo, ukabila,udini n.k hivyo mdahalo has nothing to do with kura.

Wagombea wetu hawana uwezo kabisa wa kujieleza wengi wao wanategemea WAPAMBE wao na vijembe vya majukwaani sio hoja kitu ambacho hakipo kwny mdahalo
 
Sababu vyama njaa.
Havina Wagombea wenye uwezo wa kufikili, kujadili, Kuongea, na hata Nguvu ya kuvumilia Debate mwanzo mwisho, ama wamesimamisha Wagombea Wagonjwa hivyo kuogopwa na Media.
Wao wamepata nafasi ya kugombea kwa kunuanua chama, hela nyingi za kifisadi kuhonga vijana not uwezo/ Ushawishi/kuaminiwa kwao kuja kuongoza
 
Waomb
Mwaka 1995 Ulifanyika Mdahalo Kati ya Mkapa, Lipumba na Mrema, Mkapa na Lipumba walifanya Vizuri sana lakini kwa wakati ule kwa Ushabiki watu walidhani Mrema alikuwa Ni kiongozi mzuri, Mbona kama Kidogo tuingie choo cha kike akia mama!

Nashauri 2020 Uwepo Mdahalo, Kisha Uwepo na Mwingine special kwa Lugha ya Kiingereza (Official Languages Tanzania ni English and Swahili) Ambapo wagombea watazungumzia maswala ya nje na Uhusiano wa Kimataifa.
Muombe DG wa TBC ndugu Ayoub Ryoba aweke hicho kipreamble wakati ukifika na mimi nitaangali pia na hakuna ulazima wa kutumia lugha za wenzetu acha tulie kikwetu
 
Kama mdahalo ni muhimu na ushuke mpaka kwenye ngazi ya ubunge na udiwani kama wanavyofanya mataifa makubwa yenye demokrasia iliyokomaa.
Ndio maana ya nchi kuwa changa, bado elimu ni kikwazo cha maendeleo mengine.
Marekani au Russia huwezi kuona habari ya kujengwa daraja ikipewa nafasi kwenye taarifa ya habari ya siku nzima, madaraja yalishajengwa.
Huwezi kuwadanganyia pipi watu walioelimika, sisi bado hatujaelimika ikiwa mwenye division four anaweza kwenda chuo kikuu.
 
Sababu vyama njaa.
Havina Wagombea wenye uwezo wa kufikili, kujadili, Kuongea, na hata Nguvu ya kuvumilia Debate mwanzo mwisho, ama wamesimamisha Wagombea Wagonjwa hivyo kuogopwa na Media.
Wao wamepata nafasi ya kugombea kwa kunuanua chama, hela nyingi za kifisadi kuhonga vijana not uwezo/ Ushawishi/kuaminiwa kwao kuja kuongoza
Jina tu limeshakudisqulify kuchangia mada, nyamaza tu mkuu
 
Mwaka 1995 Ulifanyika Mdahalo Kati ya Mkapa, Lipumba na Mrema, Mkapa na Lipumba walifanya Vizuri sana lakini kwa wakati ule kwa Ushabiki watu walidhani Mrema alikuwa Ni kiongozi mzuri, Mbona kama Kidogo tuingie choo cha kike akia mama!

Nashauri 2020 Uwepo Mdahalo, Kisha Uwepo na Mwingine special kwa Lugha ya Kiingereza (Official Languages Tanzania ni English and Swahili) Ambapo wagombea watazungumzia maswala ya nje na Uhusiano wa Kimataifa.
Hapo kwenye masuala ya uhusiano wa kimataifa utasikia Sasa Hussein alikuwa Rais wa.......... Ama kweli Tanzania raisi anaweza Kuwa yeyote.
 
Nchi hii ni ya vilaza, hakuna utamaduni wa kujali mambo ya msingi ndio maana waziri anaona bora akazindue Wema Sepetu App kwa vile ndio vitu watu wanapenda ni IQ ndogo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom