Kwanini Tanzania haina Income Tax Treaty na Marekani (USA)?

Ni kwa sababu wengi walio Tanzania bado hawako kwenye mfumo rasmi wa ulipaji kodi. Hiyo ni tofauti na wale walioko Marekani.

Labda useme ugumu wa kisiasa itakapoonekana tunajaribu kuenforce sheria kwa Watanzania walioko nje huku walioko ndani tunasuasua? Mbona hiyo itaipa nguvu ya kisiasa serikali kuweza kuanza kuenforce sheria hizo kwa walio ndani. Umeone jinsi vitambulisho vya Wamachinga vilivyoleta kashkash? Ku declare siyo lazima kuwa utatakiwa kulipa kodi mfano kama kipato chako kiko chini ya kiwango fulani.

Mwisho wa siku hii haimuongezei Mtanzania aliye nje mzigo wowote zaidi wa kodi.
Mtuanzania akifanya kazi Marekani na kulipa kodi Marekani, halafu umtake alipe kodi upya Tanzania, hiyo si double taxation?
 
Kuna biashara kubwa inafanyika kati ya nchi hizi mbili na hasa toka kipindi cha Urais wa Kikwete tumekuwa kwenye msukumo wa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani. Mfano ni hivi majuzi tu kuna kundi la wafanyabiashara wa Marekani walifanya mkutano na wafanyabiashara na mamlaka mbalimbali mjini Dar es Salaam.

Cha kushangaza mpaka leo hakuna Income Tax Treaty kati ya Tanzania na Marekani.

Kwa mtazamo wangu, hili jambo linaweza kuwa na faida kubwa sana kwetu. Kwa mfano, hii itawalazimu Watanzania waishio Marekani ambao bado hawajaukana Utanzania kulazimika kudeclare kipato chao kila mwaka kwa TRA na pia kulipa kodi ndani ya Tanzania kila mwaka. Tunaweza kuamua labda hii hela iende katika mfuko maalumu kwa ajili ya kazi fulani mfano elimu ya juu au ya msingi.

Hata Wamarekani wanaoishi nje ya Marekani wanalazimika kila mwaka wajaze fomu kusema wameingiza kiasi gani na wanalipa kodi huko Marekani hata kama wameishi mwaka mzima nje ya nchi yao.

Kuna masuala ya malipo ya royalty mfano kwenye shughuli kama za sanaa. Itakuwa rahisi sana kwa wasanii wa Tanzania kufaidika na kazi zao zinapotumika nchini Marekani. Sasa hivi sijui ni utaratibu gani unatumika kwenye suala kama hili. Badala ya kila siku kuja na sheria za kubana watu, embu mara moja moja tuje na sheria za kumfaidisha Mtanzania.

Pia itasaidia kujua takwimu sahihi zinazowahusu Watanzania walioko huko Marekani kitu ambacho kwa sasa hatuna. Tumekuwa tunafanya makongamano mbalimbali ya Diaspora kila mwaka tukiongelea fursa za uwekezaji na jinsi gani tunaweza kuwatumia Watanzania walioko nje kwa fursa za kiuchumi zilizoko Tanzania.

Takwimu ni zaidi ya kujua tu kuna watanzania wangapi walioko nje ya nchi. Inabidi kujua kipato chao, kazi wanazofanya, elimu yao, nk. Hatuwezi kuja na sera sahihi bila kuwa na takwimu sahihi.

Kwa haraka haraka hizo ni faida za kuwa na hiyo Income Tax Treaty lakini kuna faida nyingi zaidi zilizo direct na indirect ya kuwa na hii kitu.
Marekani haina "tax treaty" na Tanzania, lakini Sheria zao za Kodi zinataka US Citzens and Greencard Holders wanaoishi nje ya Marekani zaidi ya siku 330 wa file taxes na IRS.
 
Naunga mkono hoja, miongoni mwa mikataba tulio ingia na Marekani ni mkataba wa Anga Huria uliosainiwa na Mkapa na Bush ambao unaruhusu ndege za Marekani kuingia kwenye anga la Tanzania wakati wowote na sisi ndege zetu kuingia Marekani anytime, wakati huo Tanzania tulikuwa hatuna ndege zenye uwezo huo, sasa tunazo, tuzitumie kwa wafabiashara wa Tanzania kuzichangamkia fursa za Marekani kama ambavyo tumechamkia fursa za China. Kwa mkataba huu, Marekani is just like a next door neighbor, tunafanya safari za non stop Dar-NY-Dar, wenzetu KQ wanafanya.
P.

Utalii ni njia nzuri ya kuimarisha mapato.
 
Mtuanzania akifanya kazi Marekani na kulipa kodi Marekani, halafu umtake alipe kodi upya Tanzania, hiyo si double taxation?

Ni double taxation kama atatakiwa kulipa kodi hiyo hiyo. Inavyofanya kazi ni kuwa Mtanzania atasamehewa kabisa au kupunguziwa kodi fulani za mapato ndani ya Marekani halafu hizo kodi zikalipwa Tanzania.

Kwa mtazamo wangu kama tutafikia kufanya treaty hiyo, IRS na TRA watafanya kazi kwa pamoja kwa mfumo huu. IRS itakusanya kodi yote ya Mtanzania kama kawaida halafu itailipa TRA kilicho chake kulingana na wale Watanzania watakao declare TRA.

Hii inamaana kwa wale watanzania ambao hawatafile TRA kwa mwaka fulani, Tanzania haitapata mgao wake kutoka IRS kutokana na kutofile kwao.

Hapo hamna double taxation. Zaidi ni kuwa na sisi Wamarekani wanaofanya kazi na kulipa kodi Tanzania itabidi tusamehe au kupunguza kodi zao za mapato.

Swali ni je, tukifunga mahesabu itakuwa faida au hasara kwetu?
 
Unachekesha sana.

Kwa hesabu gani wanazojua kupiga TRA?

Umeona kodi wanayolipishwa watu kwa kuingiza magari yaliyotumika Tanzania?

Inawezekana kabisa kuna vigezo fulani vya standards za kufikia ili kuwa na taxation treaty na Marekani ambavyo Tanzania hawajavifikia bado.

Nchi haina hata kitambulisho cha taifa kinachoeleweka na kilichokuwa widely adopted na diaspora, utamkata kodi Mtanzania aliyepo nje kwa kitambulisho gani?
 
Unachekesha sana.

Kwa hesabu gani wanazojua kupiga TRA?

Umeona kodi wanayolipishwa watu kwa kuingiza magari yaliyotumika Tanzania?

Ingia website ya IRS kuna nchi zaidi ya 60 zilizo na income tax treaty na Marekani. Kila kitu kinakuwa wazi, hakuna nafasi ya hesabu za kutunga.

Labda kuna kitu namiss katika utaratibu mzima kinachofanya huu utaratibu usiwezekane au usiwe na faida kwetu.
 
Ingia website ya IRS kuna nchi zaidi ya 30 kama sikosei zilizo na income tax treaty na Marekani. Kila kitu kinakuwa wazi, hakuna nafasi ya hesabu za kutunga.

Labda kuna kitu namiss katika utaratibu mzima kinachofanya huu utaratibu usiwezekane au usiwe na faida kwetu.
Tax Regime yetu bado haijaakaa vizuri, nchi zote duniani mtu unalipa tax pale unapoishi except diplomats.

Nimekaa US hata diplomats wa Tanzania wana tax exemptions, lakini nimefanya kazi FCO ya UK, wafanyakazi wao wote wakiwemo Watanzania, hatukuwajibika kulipa kodi, na kwa sera yao, income tax ni personal affairs kwa sababu pesa ya FCO sio pesa ya Tanzania, ni British money, hivyo UK citizens tuu ndio walikuwa wanalipa kodi kwao, sisi local staff wa Tanzania, tulipaswa kulipa income tax TRA, kwa sababu japo ni pesa ya Mwingereza, sisi Wabongo we made that money Tanzania, hivyo tulipaswa kulipa kodi Tanzania, na ilipaswa Watanzania wote popote walipo, whatever the money they make, pesa yoyote wanayoituma Tanzania ilipaswa kukutwa kodi.

Wenzetu wanajisikia very proud kulipa kodi, miongoni mwa sifa za kuchaguliwa kuwa a public office, your tax clearance certificate ni moja ya sifa. Hadi Trump kule kwao analipa kodi, Obama analipa kodi, kila mtu analipa kodi.

Hata wanamuziki ma stars wao, na wana michezo wa kimataifa fedha wanazo make popote duniani, kodi inapaswa kulipwa nchini kwao, kuwa na off shore account is illegal kwa baadhi ya nchi.

Huku kwetu kwenye tax affairs tuna double standard kubwa. Kuna nafasi fulani za uongozi wana tax exemptions, then kiongozi ambaye yeye halipi kodi anaweza vipi kuuhamashisha ulipaji kodi?.

Niliwahi kushauri humu

P
 
Ingia website ya IRS kuna nchi zaidi ya 60 zilizo na income tax treaty na Marekani. Kila kitu kinakuwa wazi, hakuna nafasi ya hesabu za kutunga.

Labda kuna kitu namiss katika utaratibu mzima kinachofanya huu utaratibu usiwezekane au usiwe na faida kwetu.
Kwani wapi nimesema hakuna nchi yenye tax treaty na Marekani?

Mbona unataka kujibu swali ambalo halijaulizwa wakati lililoulizwa hujibu?
 
Niliileta mada kwa mfumo wa swali ili tujadiliane na kuelimishana kwa nini na ni busara gani imetumika hadi kuamua kwamba kutokuwa na hii treaty ni jambo lenye manufaa zaidi kwa taifa.

Mpaka sasa kwa uchunguzi wa haraka nilioufanya naona ni jambo litakalokuwa na manufaa sana kwetu. Labda utuambie hasara itakuwa wapi au kikwazo ni nini.

Mtanzania yoyote aliye Marekani kihalali ana passport ya kumtambulisha ni Mtanzania na ana file tax kila mwaka kwa IRS. Jambo pekee la ziada atakalotakiwa kufanya ni kufile pia kwa TRA, na nasema kufile siyo kulipa. Shida iko wapi maana hilo ndiyo umetoa kama kikwazo pekee?
 
Tanzania haiwezi kuwa katika position ya kuwa na tax treaty na Marekani kama nchi haina mifumo ya kisheria, kiteknolojia na inayotekelezwa na kufuatiliwa na watu ambayo inaweza kufanya mambo yanayoafikiwa kwenye tax treaty yaweze kutekelezeka.

Wenzetu wanajua maana ya msemo "a law is as good as its enforceability".

Wanaweza kukubali kuingia treaty nasi, lakini je, treaty itabaki kwenye makaratasi au itatekelezeka?

Mtanzania akifanya kazi US, TRA itahakikishaje sehemu ya kodi yake inarudi Tanzania bila kuipa kazi ya ziada IRS?

Kuna reciprocity kati ya Tanzania na US hapo? Kuna Wamarekani wangapi wanafanya kazi Tanzania ambao IRS haiwezi kuwabana bila msaada wa TRA under this treaty? Sio tunaona wenzetu wanawatoza raia wao wanaofanya kazi Tanzania bila msaada wetu, halafu sisi tunataka mkataba nao ili wao watusaidie kuwatoza kodi raia wetu wanaofanya kazi kwao! No reciprocity there. A treaty is supposed to be reciprocal and mutually beneficial.

Is Tanzania a tax haven for Americans? Hardly!

IRS itajiridhishaje Tanzania haitumii sheria za kodi kubana watu ambao chama tawala hakikubaliani nao kisiasa tu? Marekani hawataki kuingia tax treaty na nchi ambayo kodi imetumika kama fimbo ya kisiasa kufunga mdomo watu fulani. Non-discrimination provisions za tax code Marekani ziko kali sana kuangalia kodi isitumike kisiasa. Tanzania tutaweza kukidhi viwango vyao wakati tax code yetu ina loopholes na discretionary clauses kibao?
 
Tax Regime yetu bado haijaakaa vizuri, nchi zote duniani mtu unalipa tax pale unapoishi except diplomats.

Nimekaa US hata diplomats wa Tanzania wana tax exemptions, lakini nimefanya kazi FCO ya UK, wafanyakazi wao wote wakiwemo Watanzania, hatukuwajibika kulipa kodi, na kwa sera yao, income tax ni personal affairs kwa sababu pesa ya FCO sio pesa ya Tanzania, ni British money, hivyo UK citizens tuu ndio walikuwa wanalipa kodi kwao, sisi local staff wa Tanzania, tulipaswa kulipa income tax TRA, kwa sababu japo ni pesa ya Mwingereza, sisi Wabongo we made that money Tanzania, hivyo tulipaswa kulipa kodi Tanzania, na ilipaswa Watanzania wote popote walipo, whatever the money they make, pesa yoyote wanayoituma Tanzania ilipaswa kukutwa kodi.

Wenzetu wanajisikia very proud kulipa kodi, miongoni mwa sifa za kuchaguliwa kuwa a public office, your tax clearance certificate ni moja ya sifa. Hadi Trump kule kwao analipa kodi, Obama analipa kodi, kila mtu analipa kodi.

Hata wanamuziki ma stars wao, na wana michezo wa kimataifa fedha wanazo make popote duniani, kodi inapaswa kulipwa nchini kwao, kuwa na off shore account is illegal kwa baadhi ya nchi.

Huku kwetu kwenye tax affairs tuna double standard kubwa. Kuna nafasi fulani za uongozi wana tax exemptions, then kiongozi ambaye yeye halipi kodi anaweza vipi kuuhamashisha ulipaji kodi?.

Niliwahi kushauri humu

P

Kama nimekuelewa vizuri raia wa UK walioko Tanzania walikuwa wanalipa kodi yao nyumbani kwao na si Tanzania? Hii ni kwa raia wote wa UK au ni wa shirika hilo tu na utaratibu huo bado unaendelea?

Nimeingia kwenye website ya TRA. Tuna income tax treaties na nchi hizi - Canada, Denmark, Zambia, Finland, India, Italy, Norway, South Africa na Sweden.

Sina uhakika ni kiasi gani treaties hizo zinatufaidisha na ziko designed vipi na kwa kiasi gani ziko enforced.

Kuhusu exemptions za kodi tunazotoa kwa viongozi, na mimi ni moja ya vitu nisivyopenda kabisa katika mifumo yetu ya kiutawala. Natumaini kuna siku tutapata Rais atakayesema hata yeye anastahili kulipa kodi kama mwananchi mwingine. Hivi kuna viongozi wengine hawalipi kodi? Tafadhali usiniambie ni zaidi ya Rais.
 
Tanzania haiwezi kuwa katika position ya kuwa na tax treaty na Marekani kama nchi haina mifumo ya kisheria, kiteknolojia na inayotekelezwa na kufuatiliwa na watu ambayo inaweza kufanya mambo yanayoafikiwa kwenye tax treaty yaweze kutekelezeka.

Wenzetu wanajua maana ya msemo "a law is as good as its enforceability".

Wanaweza kukubali kuingia treaty nasi, lakini je, treaty itabaki kwenye makaratasi au itatekelezeka?

Mtanzania akifanya kazi US, TRA itahakikishaje sehemu ya kodi yake inarudi Tanzania bila kuipa kazi ya ziada IRS?

Kuna reciprocity kati ya Tanzania na US hapo? Kuna Wamarekani wangapi wanafanya kazi Tanzania ambao IRS haiwezi kuwabana bila msaada wa TRA under this treaty? Sio tunaona wenzetu wanawatoza raia wao wanaofanya kazi Tanzania bila msaada wetu, halafu sisi tunataka mkataba nao ili wao watusaidie kuwatoza kodi raia wetu wanaofanya kazi kwao! No reciprocity there. A treaty is supposed to be reciprocal and mutually beneficial.

Is Tanzania a tax haven for Americans? Hardly!

IRS itajiridhishaje Tanzania haitumii sheria za kodi kubana watu ambao chama tawala hakikubaliani nao kisiasa tu? Marekani hawataki kuingia tax treaty na nchi ambayo kodi imetumika kama fimbo ya kisiasa kufunga mdomo watu fulani. Non-discrimination provisions za tax code Marekani ziko kali sana kuangalia kodi isitumike kisiasa. Tanzania tutaweza kukidhi viwango vyao wakati tax code yetu ina loopholes na discretionary clauses kibao?

Nimetolea mfano wa jinsi mfumo huo unaweza kutekelezeka. Ndiyo itahitaji kazi ya ziada kidogo kwa upande wa IRS hadi kuilipa TRA fungu lao. Hapo ndiyo diplomasia na ushawishi unapohitajika. Kumbuka IRS nao watafaidikia kwa sababu TRA na vyombo vyetu watawasaidia kuhakiki tax filing ya raia wa Marekani waliopo Tanzania.

Kuhusu kodi kutumika kama fimbo ya kisiasa nakubaliana na wewe ni point muhimu ya kuzingatia na inaweza kweli kuwa kikwazo ingawa inaweza kuwa addressed kama tutakuwa na nia ya kweli ya kuifanikisha.
 
Kwa utawala huu kuita watu mabeberu huku Tanzania na kule Marekani rais kuita Africa shithole countries naona kama hii si priority kwa pande zote mbili.

Na wewe unajikita zaidi kwenye mjadala wa academia kama mtu aliyepewa assignment ya chuoni ambayo katika maisha ya uhalisia haitekeleziki kwa mfumo uliopo sasa.

Wamarekani ni watu practical sana, Tanzania ingekuwa Switzerland, a leading banking hub ambapo Wamarekani wanakimbizia fedha zao ili wasilipe kodi kwao, habari hii ingepewa kipaumbele.

Sasa wakiangalia Tanzania wanaona kumejaa Wamisionari na corporations za kuhesabu, halafu hizo corporations wanajua kuzibana, this treaty business is not their priority.

Huku Tanzania hata hiyo TIN tu Watanzania wa diaspora hawana, sasa utaanzaje kuongelea treaty wakati watu hawana hata TIN?
 
Naheshimu mawazo yako ila naona bado hoja zako hazijanishawishi vya kutosha kuwa ni jambo lisilowezekana.

Kingine nilicho notice ni kuwa haujasema kama ni jambo ambalo litakuwa au halitakuwa na manufaa kwetu. Kwa sababu kama manufaa ni makubwa, issue ulizozitaja zinatatulika na kurekebishika.

Kwa mfano, kupata TIN ni issue ya ndani ya saa moja ukienda ofisi ya TRA. Nadhani TRA wanaweza kuratibu zoezi la upatikanaji wa TIN kwa Watanzania walioko Marekani.

Tayari tuna Income Tax Treaties (au Double Taxation Treaties) na nchi zifuatazo: Canada, Denmark, Zambia, Finland, India, Italy, Norway, South Africa na Sweden.

Karibu hizo nchi zote ni advanced economies sawa na Marekani kwa hiyo hoja ya teknolojia ya TRA kuwa duni sana kuhimili treaty ya namna hii nayo naona haina nguvu sana. Nasema hivi nikikiri bado sijajua mfumo wa treaties hizo umekaaje na kama unafanana na ule Marekani amefanya na nchi zingine ila malengo naona ni yaleyale. Nitazipitia nione zinasemaje.

Nilichonotice kingine ni kuwa hizi treaties zote tuliingia zamani sana, majority kabla ya 1980. Treaty pekee tuliyoingia baada ya 1980 ni South Africa (2005) na Canada (1995). Kama ni hivyo, swali langu linapata uzito zaidi. Kwa nini hatusimamii mikataba hii kama ina manufaa kwetu?
 
Naomba pia uchukue point hii.

Labda nikufahamishe tu. Mimi ni mtu critical sana kwenye mifumo yetu ya kodi. Haina usawa, haiko wazi, haina ubunifu hasa katika kuchochea maendeleo ya sekta fulani au kuchochea ulipaji kodi wa hiari, na pia inatoa nafasi kubwa za rushwa na uonevu. Kwa hiyo, I am not naive!

Nimeleta hii mada nikitambua changamoto hizo zote lakini pia nikitambua manufaa yake makubwa kama tutalitekeleza kwa umakini. Kuna wakati ni bora kuangalia mambo kwa mtazamo chanya.
 
First things first, wapi nimesema ni jambo lisilowezekana?

Please let's be very specific with wording.

Kusema hii si priority kwa pande zote mbili kwa sasa, na mifumo yetu haina basic requirements kwa treaty na Wamarekani, ambao ni a totally different animal from the rest of the world, ndiyo kusema hili ni jambo lisilowezekana?
 
Naomba pia uchukue point hii.

Labda nikufahamishe tu. Mimi ni mtu critical sana kwenye mifumo yetu ya kodi. Haina usawa, haiko wazi, haina ubunifu hasa katika kuchochea maendeleo ya sekta fulani au kuchochea ulipaji kodi wa hiari, na pia inatoa nafasi kubwa za rushwa na uonevu. Kwa hiyo, I am not naive!

Nimeleta hii mada nikitambua changamoto hizo zote lakini pia nikitambua manufaa yake makubwa kama tutalitekeleza kwa umakini. Kuna wakati ni bora kuangalia mambo kwa mtazamo chanya.
Unataka kuangalia mambo kwa mtazamo chanya wakati IRS wakiuliza ubalozi wa Marekani Tanzania vipi serikali ya Tanzania inatoza kodi Tanzania wanaambiwa hapa hakuna kodi kuna a Shylocking system?
 
Tax Treaty -- isiwe confined kwenye income tax only....

I am against the idea of a state to tax an individual outside the state's jurisdictions. You make money in Tanzania, you pay tax in Tanzania. You make money overseas, you pay tax overseas. You bring overseas money to Tanzania, you comply with Tanzanian laws. You take Tanzanian money to overseas, you comply with their laws. Simple!

I support the idea, and probably you may have not read such treaties in detail. They have clauses against double taxation.

Taxes are not always paid at the moment you get paid, they are only paid at the end of a certain period of time, norammly annually or quarterly after putting together the total income in that period. A Tanzanian resident in USA will pay tax in USA, not in Tanzania; however, a Tanzanian visiting USA for a day and makes money from acts such as winning lottery, making a paid speech or perfoming arts shows does not pay tax in USA because he/she is not resident, so he/she has no tax number or social security number. Unfortunately such income also does not reflect in his/her taxes in Tanzania; that is when tax treaties come into play.
 
Keynez anataka mpaka Watanzania wanaoishi Marekani walipe kodi Tanzania, au IRS ilipe sehemu ya kodi yao Tanzania.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom