Kwanini Tanzania haina Income Tax Treaty na Marekani (USA)?

Hili sio swala rahisi hivo hasa kama watanzania waishio nje wanachukuliwa kwanza kama sio wazalendo! Uzalendo ni kuishi Tanzania na kuitwa mnyonge!!

Pamoja na wazo hilo kuwa na faida kwa nchi, vipi haki za raia hao kupata haki za kiraia kama kupiga kura na kushiriki siasa kutoka nje?? Kama mjawaita mawakala wa mabeberu sijui!!

This is a give and take. Mpaka sasa hujapendekeza nchi itatoa nini kwa raia wake aliye nje!!

Inabidi Watanzania walioko Marekani watumie hoja kama hizi kama shawishi ili wapate mabadiliko wanayoyataka mfano kwenye uraia pacha, upigaji kura.

Kama ulivyosema, majadiliano ni give and take, Watanzania walio nje walikuwa wanaleta nini mezani?

Kauli ya 'no taxation, no representation' imepata maana kubwa zaidi kwa hoja hii.
 
Ni kweli tunajikongoja sana linapokuja suala la sanaa kwa ujumla. Bila wasanii wenyewe kusimama na kusema wanachotaka, serikali kamwe haitawaletea mabadiliko yanayohitajika. Suala la royalties bado linahitaji uwepo wa ushirikiano wa karibu kati ya TRA na IRS na ndiyo hapo tax treaty inapoingia. Hiyo haimaanishi vyombo vingine ya sanaa kama ulivyovitaja havitahusika.

Unajua fursa za muziki wa Kiswahili linaenda hadi kwenye soundtracks za filamu za Hollywood ambapo nadhani kuna fursa kubwa sana kwa muziki wetu hapo. Bila kuweka mfumo rasmi, rahisi na unaoeleweka na kuwa na ushirikiano wa karibu kati ya taasisi zetu na za Marekani, hizi fursa haziwezi kufunguka.

I am not a big fan to the involvement of government in business. Kazi ya serikali ni kukusanya kodi na kuweka mazingira wezeshi. Ushirikiano wa TRA na IRS utaleta ufanisi kwenye kukusanya kodi. Kwenye upande wa usambazaji kazi za sanaa, siku hizi ni zama za Indie Publishers na za ma aggregators. TRA na IRS hawahusiki kabisa, zaidi ya kukusanya their fair share.

To put it in another way, I don't see why one would need IRS or TRA to intervene for their work to get included in mega projects.
 
Tatizo ninaloliona ni kuwa bado tunatazama utoaji wa viza kama chanzo cha mapato.

Ikiwa tunategemea viza kama chanzo muhimu cha mapato, kuongeza urefu wa viza kutaongeza idadi ya wanaoshawishika kuja TZ. I hope watunga sera wanatumia vilivyo financial modelling na utaalam mwingine wa ma data analyst katika kupata optimum policies.
 
Naunga mkono hoja, miongoni mwa mikataba tulio ingia na Marekani ni mkataba wa Anga Huria uliosainiwa na Mkapa na Bush ambao unaruhusu ndege za Marekani kuingia kwenye anga la Tanzania wakati wowote na sisi ndege zetu kuingia Marekani anytime, wakati huo Tanzania tulikuwa hatuna ndege zenye uwezo huo, sasa tunazo, tuzitumie kwa wafabiashara wa Tanzania kuzichangamkia fursa za Marekani kama ambavyo tumechamkia fursa za China. Kwa mkataba huu, Marekani is just like a next door neighbor, tunafanya safari za non stop Dar-NY-Dar, wenzetu KQ wanafanya.
P.
Unadhani ni rahisi hivyo kuingia anga ya Marekani moja kwa moja?
 
Kuna biashara kubwa inafanyika kati ya nchi hizi mbili na hasa toka kipindi cha Urais wa Kikwete tumekuwa kwenye msukumo wa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani. Mfano ni hivi majuzi tu kuna kundi la wafanyabiashara wa Marekani walifanya mkutano na wafanyabiashara na mamlaka mbalimbali mjini Dar es Salaam.

Cha kushangaza mpaka leo hakuna Income Tax Treaty kati ya Tanzania na Marekani.

Kwa mtazamo wangu, hili jambo linaweza kuwa na faida kubwa sana kwetu. Kwa mfano, hii itawalazimu Watanzania waishio Marekani ambao bado hawajaukana Utanzania kulazimika kudeclare kipato chao kila mwaka kwa TRA na pia kulipa kodi ndani ya Tanzania kila mwaka. Tunaweza kuamua labda hii hela iende katika mfuko maalumu kwa ajili ya kazi fulani mfano elimu ya juu au ya msingi.

Hata Wamarekani wanaoishi nje ya Marekani wanalazimika kila mwaka wajaze fomu kusema wameingiza kiasi gani na wanalipa kodi huko Marekani hata kama wameishi mwaka mzima nje ya nchi yao.

Kuna masuala ya malipo ya royalty mfano kwenye shughuli kama za sanaa. Itakuwa rahisi sana kwa wasanii wa Tanzania kufaidika na kazi zao zinapotumika nchini Marekani. Sasa hivi sijui ni utaratibu gani unatumika kwenye suala kama hili. Badala ya kila siku kuja na sheria za kubana watu, embu mara moja moja tuje na sheria za kumfaidisha Mtanzania.

Pia itasaidia kujua takwimu sahihi zinazowahusu Watanzania walioko huko Marekani kitu ambacho kwa sasa hatuna. Tumekuwa tunafanya makongamano mbalimbali ya Diaspora kila mwaka tukiongelea fursa za uwekezaji na jinsi gani tunaweza kuwatumia Watanzania walioko nje kwa fursa za kiuchumi zilizoko Tanzania.

Takwimu ni zaidi ya kujua tu kuna watanzania wangapi walioko nje ya nchi. Inabidi kujua kipato chao, kazi wanazofanya, elimu yao, nk. Hatuwezi kuja na sera sahihi bila kuwa na takwimu sahihi.

Kwa haraka haraka hizo ni faida za kuwa na hiyo Income Tax Treaty lakini kuna faida nyingi zaidi zilizo direct na indirect ya kuwa na hii kitu.
Mkuu hizo faida ni nzuri sana. Naamini kila kitu kina faida na hasara zake; hebu tusaidie na hasara pia tuweze kupima.
 
Naunga mkono hoja. Wasiwasi wangu ni kuwa bila kuimarisha sekta zingine na kuja na mikakati ili ziwe tayari kufaidika na uwepo wa ATCL, ununuzi wa ndege unaweza kuwa 'hasara isiyo na faida'.

ATCL inabidi iwe cheaper kuliko mashirika mengine hata kwa usafiri wa ndani lakini iwe na ufanisi wa hali ya juu. Malengo makuu ya ATCL yawe kwa ajili ya kuboost sekta zingine hasa hasa kilimo na utalii na kuwe na mfumo rasmi wa kupima jinsi malengo hayo yanavyofikiwa. Kwa maana hiyo usafirishaji wa mizigo pia ungekuwa moja ya kipaumbele cha ATCL.

Pia tungeweka mfumo rasmi wa sekta za kilimo na utalii ku subsidize ATCL moja kwa moja kufidia gharama/hasara zake kwa sababu wao ndiyo wanatakiwa wawe wafaidika wa kwanza, ie. wadau namba moja.
Hilo la kuipa mizigo kipaumbele ni muhimu sana. Kuna maua Arusha yanaenda Kenya ili yapelekwe Ulaya. Nasikia Nyanda za Juu Kusini kuna kilimo cha mbogamboga na matunda, hivi navyo vinahitaji usafiri wa uhakika ili vifike kwa walaji huko Ulaya. Kukiwa na usafiri wa uhakika basi hata wakulima wetu wa Horticulture wataongeza uzalishaji na hivyo kujiongezea kipato.
 
Sullivan summit na ule utapeli wa treni ya kuanzia posta hadi gongo la mboto changanya na ule mpira alikuwa anapiga dana dana Obama pale Ubungo.

Mkuu ulikuwepo wapi kipindi hicho hayo yanafanyika au unaongelea USA river ya kule Arusha?
 
Unadhani ni rahisi hivyo kuingia anga ya Marekani moja kwa moja?
It's as simple as ABC, kasome mkataba wa Anga Huria kati ya Tanzania na Marekani, ndege za TZ zinaland US anytime without notice only landing clearance.

Ndege tunazo, why not?.
P
 
Suala siyo kuwa na ndege ila ukiritimba wa hao Wamarekani. Kuna ukiritimba mwingi sana ndege yako kutoka kiwanjani kwako kwenda moja kwa moja huko America. Jifunze utabaini kwamba siyo kama aaa beee cheee!!
 
Kuna biashara kubwa inafanyika kati ya nchi hizi mbili na hasa toka kipindi cha Urais wa Kikwete tumekuwa kwenye msukumo wa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani. Mfano ni hivi majuzi tu kuna kundi la wafanyabiashara wa Marekani walifanya mkutano na wafanyabiashara na mamlaka mbalimbali mjini Dar es Salaam.

Cha kushangaza mpaka leo hakuna Income Tax Treaty kati ya Tanzania na Marekani.

Kwa mtazamo wangu, hili jambo linaweza kuwa na faida kubwa sana kwetu. Kwa mfano, hii itawalazimu Watanzania waishio Marekani ambao bado hawajaukana Utanzania kulazimika kudeclare kipato chao kila mwaka kwa TRA na pia kulipa kodi ndani ya Tanzania kila mwaka. Tunaweza kuamua labda hii hela iende katika mfuko maalumu kwa ajili ya kazi fulani mfano elimu ya juu au ya msingi.

Hata Wamarekani wanaoishi nje ya Marekani wanalazimika kila mwaka wajaze fomu kusema wameingiza kiasi gani na wanalipa kodi huko Marekani hata kama wameishi mwaka mzima nje ya nchi yao.

Kuna masuala ya malipo ya royalty mfano kwenye shughuli kama za sanaa. Itakuwa rahisi sana kwa wasanii wa Tanzania kufaidika na kazi zao zinapotumika nchini Marekani. Sasa hivi sijui ni utaratibu gani unatumika kwenye suala kama hili. Badala ya kila siku kuja na sheria za kubana watu, embu mara moja moja tuje na sheria za kumfaidisha Mtanzania.

Pia itasaidia kujua takwimu sahihi zinazowahusu Watanzania walioko huko Marekani kitu ambacho kwa sasa hatuna. Tumekuwa tunafanya makongamano mbalimbali ya Diaspora kila mwaka tukiongelea fursa za uwekezaji na jinsi gani tunaweza kuwatumia Watanzania walioko nje kwa fursa za kiuchumi zilizoko Tanzania.

Takwimu ni zaidi ya kujua tu kuna watanzania wangapi walioko nje ya nchi. Inabidi kujua kipato chao, kazi wanazofanya, elimu yao, nk. Hatuwezi kuja na sera sahihi bila kuwa na takwimu sahihi.

Kwa haraka haraka hizo ni faida za kuwa na hiyo Income Tax Treaty lakini kuna faida nyingi zaidi zilizo direct na indirect ya kuwa na hii kitu.
Kuna mambo mawili
1. Tax treat
2.. International taxation
Tax treat ni makubaliano kati ya nchi na nchi kwenye suala la import product toka nchi hizo kwenda mojawapo ya nchi hizo hizo kwamba % ya tax itakuwa kiasi gani mfano 3%, or 10% ya import tax. Mfano USA na China walikuwa na tax treat Donald trump alipoingia akafungua nayo ndo maana ikaleta mzozo wa kiuchumi. Bidhaa zinazoingia toka China kwenda USA tax yake ni ndogo sana, ndo maana kampuni nyingi za marekani zikawekeza viwanda vingi China kwenye cheap labour, wakizalisha wanasafilisha kwenda marekani kwenye soko Kubwa la uwakika kwa kulipa tax kidogo sana. Vile vile USA walikuwa wanaexport agricultural products mfano soya beans kwenda China walikuwa wanalipa tax ndogo sana.
Kuna tax treat nyingine ya NAFTA North America free trade area, ukizalisha bidhaa zako toka Canada or Mexico or USA unaweza peleka nchi yeyote kwa kulipa tax kidogo sana. Kampuni nyingi za European countries waliwekeza sana upande wa Mexico karibu na border ya USA kwa sababu ya cheap labour kwa upande wa Mexico wakizalisha wanapeleka USA kwa vile wanakuwa ndani ya treat ya NAFTA, (Maquiladola industrial area) . Vile vile kampuni nyingi za USA walianzisha viwanda upande wa Mexico kufuata cheap labour. Wakizalisha tu wanapeleka USA kwneye soko la uwakika.
2. International taxation, hapa Unaongelea unayosema, kwa nchi nyingi duniani mfano USA, kama kampuni imesajiliwa kwenye Ardhi yao, ikifanya operations nje ya mipaka yake, lazima income proceeds na profit walejeshe kwenye kampuni mama uko USA, mfano kama wamepata profit ya $1billion toka Tanzania, na Tanzania wamekata corporate tax ya 30% hivyo basi kampuni lazima walejeshe yote USA, na USA wanapiga corporate tax yao ya 30%, wanakuwa refunded 30% waliyokatwa nchini Tanzania, vile vile kwa wafanyakazi wao lazima walejeshe mapato na makato yote, Serikali inacharge tax yake mwisho wa siku Wanakuwa refunded makato waliyokatwa Tanzania. Kama Tanzania watawapa tax holiday kwao USA lazima walipe kodi ya profit waliyotengeneza Tanzania. USA hakuna tax holiday Unalipa from day one unapoamza biashara.
Kama Tanzania watakuwa na system kama hiyo ni mzuri, swali litakuja kwenye refund itakuwa kichefuchefu, forgery nyingi.
 
Hilo la kuipa mizigo kipaumbele ni muhimu sana. Kuna maua Arusha yanaenda Kenya ili yapelekwe Ulaya. Nasikia Nyanda za Juu Kusini kuna kilimo cha mbogamboga na matunda, hivi navyo vinahitaji usafiri wa uhakika ili vifike kwa walaji huko Ulaya. Kukiwa na usafiri wa uhakika basi hata wakulima wetu wa Horticulture wataongeza uzalishaji na hivyo kujiongezea kipato.

Ningeshauri iundwe bodi au taasisi maalumu itakayounganisha watu wa ATCL, Fedha, Kilimo na Utalii. Halafu waje na mikakati ya pamoja ya jinsi ATCL inaweza kutumika kama kichocheo cha ukuaji wa sekta hizo.

Mzigo wa ATCL inabidi utoke Ikulu na ubebwe moja kwa moja na wadau wa kilimo na utalii. Ikibidi Ikulu isimamie tu na kuratibu mipango ili isirubuniwe.
 
Mkuu hizo faida ni nzuri sana. Naamini kila kitu kina faida na hasara zake; hebu tusaidie na hasara pia tuweze kupima.

Swali limekaa kimtego hili. Nadhani cha muhimu ni kuhakikisha suala zima linatekelezwa kwa maslahi ya taifa huku tukihakikisha usiri wa taarifa za watu unazingatiwa siku zote.

Sioni hasara za kuhofia sana kwenye hili ingawa itabidi wahusika wafanye homework ili iwe na manufaa kwa wote.
 
Kuna biashara kubwa inafanyika kati ya nchi hizi mbili na hasa toka kipindi cha Urais wa Kikwete tumekuwa kwenye msukumo wa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani. Mfano ni hivi majuzi tu kuna kundi la wafanyabiashara wa Marekani walifanya mkutano na wafanyabiashara na mamlaka mbalimbali mjini Dar es Salaam.

Cha kushangaza mpaka leo hakuna Income Tax Treaty kati ya Tanzania na Marekani.

Kwa mtazamo wangu, hili jambo linaweza kuwa na faida kubwa sana kwetu. Kwa mfano, hii itawalazimu Watanzania waishio Marekani ambao bado hawajaukana Utanzania kulazimika kudeclare kipato chao kila mwaka kwa TRA na pia kulipa kodi ndani ya Tanzania kila mwaka. Tunaweza kuamua labda hii hela iende katika mfuko maalumu kwa ajili ya kazi fulani mfano elimu ya juu au ya msingi.

Hata Wamarekani wanaoishi nje ya Marekani wanalazimika kila mwaka wajaze fomu kusema wameingiza kiasi gani na wanalipa kodi huko Marekani hata kama wameishi mwaka mzima nje ya nchi yao.

Kuna masuala ya malipo ya royalty mfano kwenye shughuli kama za sanaa. Itakuwa rahisi sana kwa wasanii wa Tanzania kufaidika na kazi zao zinapotumika nchini Marekani. Sasa hivi sijui ni utaratibu gani unatumika kwenye suala kama hili. Badala ya kila siku kuja na sheria za kubana watu, embu mara moja moja tuje na sheria za kumfaidisha Mtanzania.

Pia itasaidia kujua takwimu sahihi zinazowahusu Watanzania walioko huko Marekani kitu ambacho kwa sasa hatuna. Tumekuwa tunafanya makongamano mbalimbali ya Diaspora kila mwaka tukiongelea fursa za uwekezaji na jinsi gani tunaweza kuwatumia Watanzania walioko nje kwa fursa za kiuchumi zilizoko Tanzania.

Takwimu ni zaidi ya kujua tu kuna watanzania wangapi walioko nje ya nchi. Inabidi kujua kipato chao, kazi wanazofanya, elimu yao, nk. Hatuwezi kuja na sera sahihi bila kuwa na takwimu sahihi.

Kwa haraka haraka hizo ni faida za kuwa na hiyo Income Tax Treaty lakini kuna faida nyingi zaidi zilizo direct na indirect ya kuwa na hii kitu.
Watanzania walio Tanzania wana declare income TRA kila mwaka?
 
Tax Treaty -- isiwe confined kwenye income tax only....

I am against the idea of a state to tax an individual outside the state's jurisdictions. You make money in Tanzania, you pay tax in Tanzania. You make money overseas, you pay tax overseas. You bring overseas money to Tanzania, you comply with Tanzanian laws. You take Tanzanian money to overseas, you comply with their laws. Simple!
I concurr.

That will avoid double taxation.
 
Kuna mambo mawili
1. Tax treat
2.. International taxation
Tax treat ni makubaliano kati ya nchi na nchi kwenye suala la import product toka nchi hizo kwenda mojawapo ya nchi hizo hizo kwamba % ya tax itakuwa kiasi gani mfano 3%, or 10% ya import tax. Mfano USA na China walikuwa na tax treat Donald trump alipoingia akafungua nayo ndo maana ikaleta mzozo wa kiuchumi. Bidhaa zinazoingia toka China kwenda USA tax yake ni ndogo sana, ndo maana kampuni nyingi za marekani zikawekeza viwanda vingi China kwenye cheap labour, wakizalisha wanasafilisha kwenda marekani kwenye soko Kubwa la uwakika kwa kulipa tax kidogo sana. Vile vile USA walikuwa wanaexport agricultural products mfano soya beans kwenda China walikuwa wanalipa tax ndogo sana.
Kuna tax treat nyingine ya NAFTA North America free trade area, ukizalisha bidhaa zako toka Canada or Mexico or USA unaweza peleka nchi yeyote kwa kulipa tax kidogo sana. Kampuni nyingi za European countries waliwekeza sana upande wa Mexico karibu na border ya USA kwa sababu ya cheap labour kwa upande wa Mexico wakizalisha wanapeleka USA kwa vile wanakuwa ndani ya treat ya NAFTA, (Maquiladola industrial area) . Vile vile kampuni nyingi za USA walianzisha viwanda upande wa Mexico kufuata cheap labour. Wakizalisha tu wanapeleka USA kwneye soko la uwakika.
2. International taxation, hapa Unaongelea unayosema, kwa nchi nyingi duniani mfano USA, kama kampuni imesajiliwa kwenye Ardhi yao, ikifanya operations nje ya mipaka yake, lazima income proceeds na profit walejeshe kwenye kampuni mama uko USA, mfano kama wamepata profit ya $1billion toka Tanzania, na Tanzania wamekata corporate tax ya 30% hivyo basi kampuni lazima walejeshe yote USA, na USA wanapiga corporate tax yao ya 30%, wanakuwa refunded 30% waliyokatwa nchini Tanzania, vile vile kwa wafanyakazi wao lazima walejeshe mapato na makato yote, Serikali inacharge tax yake mwisho wa siku Wanakuwa refunded makato waliyokatwa Tanzania. Kama Tanzania watawapa tax holiday kwao USA lazima walipe kodi ya profit waliyotengeneza Tanzania. USA hakuna tax holiday Unalipa from day one unapoamza biashara.
Kama Tanzania watakuwa na system kama hiyo ni mzuri, swali litakuja kwenye refund itakuwa kichefuchefu, forgery nyingi.

Nadhani unachanganya madesa mkuu. Makubaliano ya namna hiyo yanayohusu import duties tayari tunayo mfano Millenium Challenge (MCC).

Hapa tunazungumzia Income Tax.

By the way, faida nyingine ni kuwa Watanzania walioko Marekani watakuwa wanasamehewa au kupunguziwa baadhi ya kodi za mapato wanazotakiwa kulipa nchini Marekani badala yake watazilipia Tanzania.
 
Watanzania walio Tanzania wana declare income TRA kila mwaka?

Kisheria nadhani tunatakiwa ila wengi hawafanyi hivyo. Kwa mantiki hiyo, technically speaking Watanzania waishio nje ya Tanzania inabidi nao wa declare income yao nchini Tanzania.

Income Tax Treaty inasaidia kuondoa double taxation na siyo chanzo chake.
 
Kisheria unadhani au unajua?

Form ya kujaza kwa kila Mtanzania ku declare income inaitwaje? Inapatikana wapi?

Unaelewa kwamba Wamarekani wenye income inayopita filing threshold (about $12,000 for single person for 2018) wanatakiwa ku declare income IRS (TRA yao) kila mwaka, bila kujali kama wako Tanzania ambako hakuna treaty au siyo?

Sasa kwa nini Tanzania ihitaji treaty ili kuwafanya Watanzania wanaoishi Marekani ku declare income TRA?
 
Kisheria unadhani au unajua?

Form ya kujaza kwa kila Mtanzania ku declare income inaitwaje? Inapatikana wapi?

Unaelewa kwamba Wamarekani wenye income inayopita filing threshold (about $5000) wanatakiwa ku declare income IRS (TRA yao) kila mwaka, bila kujali kama wako Tanzania ambako hakuna treaty au siyo?

Sasa kwa nini Tanzania ihitaji treaty ili kuwafanya Watanzania wanaoishi Marekani ku declare income TRA?

Hatuwezi ku enforce kitu kama hicho bila mfumo rasmi tutakaokubaliana na Marekani. Inabidi kukubaliana ni kodi zipi zitalipwa Tanzania na zipi zitalipwa Marekani. Au kama kuna punguzo litakuwa ni asilimia ngapi, nk.

Marekani siku zote hawamsubiri mtu. Wameona tranparency na consistency kwenye mifumo yao ni muhimu kuliko kingine chochote. Nina uhakika tukiwaapproach kuhusu hili watakuwa tayari kutusikiliza.

Bila treaty, Tanzania itakuwa inafanya double taxation au wewe unaona uwezekano wa TRA kuwarefund Watanzania kodi walizolipa Marekani?Tukiamua kufanya hivyo si ni afadhali basi tuwe na treaty kabisa ili huo mzigo usiwaangukie TRA?

Najibu kulinganisha na uelewa wangu ilivyo.
 
Hatuwezi ku enforce kitu kama hicho bila mfumo rasmi tutakaokubaliana na Marekani. Inabidi kukubaliana ni kodi zipi zitalipwa Tanzania na zipi zitalipwa Marekani. Au kama kuna punguzo litakuwa ni asilimia ngapi, nk.

Marekani siku zote hawamsubiri mtu. Wameona tranparency na consistency kwenye mifumo yao ni muhimu kuliko kingine chochote. Nina uhakika tukiwaapraoch kuhusu hili watakuwa tayari kutusikiliza.

Najibu kulinganisha na uelewa wangu ilivyo.
Kama hatuwezi ku enforce filing kwa Watanzania walio Tanzania, kipi kinakufanya ufikiri tutaweza ku enforce filing kwa Watanzania walio Marekani?
 
Ni kwa sababu wengi walio Tanzania bado hawako kwenye mfumo rasmi wa ulipaji kodi. Hiyo ni tofauti na wale walioko Marekani.

Labda useme ugumu wa kisiasa itakapoonekana tunajaribu kuenforce sheria kwa Watanzania walioko nje huku walioko ndani tunasuasua? Mbona hiyo itaipa nguvu ya kisiasa serikali kuweza kuanza kuenforce sheria hizo kwa walio ndani. Umeone jinsi vitambulisho vya Wamachinga vilivyoleta kashkash? Ku declare siyo lazima kuwa utatakiwa kulipa kodi mfano kama kipato chako kiko chini ya kiwango fulani.

Mwisho wa siku hii haimuongezei Mtanzania aliye nje mzigo wowote zaidi wa kodi.
 
Back
Top Bottom