Kwanini Tanzania haina Income Tax Treaty na Marekani (USA)?

Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,441
Points
2,000
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,441 2,000
Kuna biashara kubwa inafanyika kati ya nchi hizi mbili na hasa toka kipindi cha Urais wa Kikwete tumekuwa kwenye msukumo wa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani. Mfano ni hivi majuzi tu kuna kundi la wafanyabiashara wa Marekani walifanya mkutano na wafanyabiashara na mamlaka mbalimbali mjini Dar es Salaam.

Cha kushangaza mpaka leo hakuna Income Tax Treaty kati ya Tanzania na Marekani.

Kwa mtazamo wangu, hili jambo linaweza kuwa na faida kubwa sana kwetu. Kwa mfano, hii itawalazimu Watanzania waishio Marekani ambao bado hawajaukana Utanzania kulazimika kudeclare kipato chao kila mwaka kwa TRA na pia kulipa kodi ndani ya Tanzania kila mwaka. Tunaweza kuamua labda hii hela iende katika mfuko maalumu kwa ajili ya kazi fulani mfano elimu ya juu au ya msingi.

Hata Wamarekani wanaoishi nje ya Marekani wanalazimika kila mwaka wajaze fomu kusema wameingiza kiasi gani na wanalipa kodi huko Marekani hata kama wameishi mwaka mzima nje ya nchi yao.

Kuna masuala ya malipo ya royalty mfano kwenye shughuli kama za sanaa. Itakuwa rahisi sana kwa wasanii wa Tanzania kufaidika na kazi zao zinapotumika nchini Marekani. Sasa hivi sijui ni utaratibu gani unatumika kwenye suala kama hili. Badala ya kila siku kuja na sheria za kubana watu, embu mara moja moja tuje na sheria za kumfaidisha Mtanzania.

Pia itasaidia kujua takwimu sahihi zinazowahusu Watanzania walioko huko Marekani kitu ambacho kwa sasa hatuna. Tumekuwa tunafanya makongamano mbalimbali ya Diaspora kila mwaka tukiongelea fursa za uwekezaji na jinsi gani tunaweza kuwatumia Watanzania walioko nje kwa fursa za kiuchumi zilizoko Tanzania.

Takwimu ni zaidi ya kujua tu kuna watanzania wangapi walioko nje ya nchi. Inabidi kujua kipato chao, kazi wanazofanya, elimu yao, nk. Hatuwezi kuja na sera sahihi bila kuwa na takwimu sahihi.

Kwa haraka haraka hizo ni faida za kuwa na hiyo Income Tax Treaty lakini kuna faida nyingi zaidi zilizo direct na indirect ya kuwa na hii kitu.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
31,030
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
31,030 2,000
Naunga mkono hoja, miongoni mwa mikataba tulio ingia na Marekani ni mkataba wa Anga Huria uliosainiwa na Mkapa na Bush ambao unaruhusu ndege za Marekani kuingia kwenye anga la Tanzania wakati wowote na sisi ndege zetu kuingia Marekani anytime, wakati huo Tanzania tulikuwa hatuna ndege zenye uwezo huo, sasa tunazo, tuzitumie kwa wafabiashara wa Tanzania kuzichangamkia fursa za Marekani kama ambavyo tumechamkia fursa za China. Kwa mkataba huu, Marekani is just like a next door neighbor, tunafanya safari za non stop Dar-NY-Dar, wenzetu KQ wanafanya.
P.
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
773
Points
1,000
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
773 1,000
Tax Treaty -- isiwe confined kwenye income tax only....

I am against the idea of a state to tax an individual outside the state's jurisdictions. You make money in Tanzania, you pay tax in Tanzania. You make money overseas, you pay tax overseas. You bring overseas money to Tanzania, you comply with Tanzanian laws. You take Tanzanian money to overseas, you comply with their laws. Simple!
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
773
Points
1,000
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
773 1,000
...

Cha kushangaza mpaka leo hakuna Income Tax Treaty kati ya Tanzania na Marekani.

...

Kuna masuala ya malipo ya royalty mfano kwenye shughuli kama za sanaa. Itakuwa rahisi sana kwa wasanii wa Tanzania kufaidika na kazi zao zinapotumika nchini Marekani. Sasa hivi sijui ni utaratibu gani unatumika kwenye suala kama hili. Badala ya kila siku kuja na sheria za kubana watu, embu mara moja moja tuje na sheria za kumfaidisha Mtanzania.
You are providing right remedy to a wrong malady.

Issues za royalties ni za taasisi za sanaa, hakimiliki na hakishiriki kuwa na mahusiano na similar taasisi overseas. Lakini kumbuka business model ya kazi za sanaa ilishabadilika saana. Kwa sasa sheria za kwetu zimepitwa na wakati na uhalisia.

Kwa mfano, siku hizi muziki hauuzwi sana. Mtu unapewa access to an "all-you can eat" repertoire of music you can listen to. Most are ad-supported or subscription-based.

Ndio maana hata kauli za kusema miziki inayopigwa kwenye kumbi ilipiwe, iko based on pre-internet realities. Siku hizi za Spotify, Mkito, Mdundo, Youtube na distributors wengine, watu wanaweka nyimbo zao ili ziwe played bure... how do you want someone to pay for a service already paid for via shitariki au matangazo?
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
773
Points
1,000
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
773 1,000
Ukienda Marekani, unapewa maximum visa ya miaka miwili -- ukiwa ni Mtanzania. Ukiwa ni raia wa nchi nyingine, say, Jamaica, unapewa visa ya miaka 12 or something like that... Nasikia jamaa wanareciprocate the favors we give to their citizens. Probably we may need to look at whether we want things to be like this, and react accordingly.
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
12,050
Points
2,000
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
12,050 2,000
Kwa mfano, hii itawalazimu Watanzania waishio Marekani ambao bado hawajaukana Utanzania kulazimika kudeclare kipato chao kila mwaka kwa TRA na pia kulipa kodi ndani ya Tanzania kila mwaka.

Je wakipatwa na misukosuko huko kama inavyoendelea SA, serikali yetu itawatambua na kuwasaidia? Kuna kejeli nyingi zinaandikwa juu ya wahanga wa kitanzania kwenye vurugu zinazoendelea huko SA
 
kapalamsenga

kapalamsenga

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2013
Messages
6,986
Points
2,000
kapalamsenga

kapalamsenga

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2013
6,986 2,000
Naunga mkono hoja, miongoni mwa mikataba tulio ingia na Marekani ni mkataba wa Anga Huria uliosainiwa na Mkapa na Bush ambao unaruhusu ndege za Marekani kuingia kwenye anga la Tanzania wakati wowote na sisi ndege zetu kuingia Marekani anytime, wakati huo Tanzania tulikuwa hatuna ndege zenye uwezo huo, sasa tunazo, tuzitumie kwa wafabiashara wa Tanzania kuzichangamkia fursa za Marekani kama ambavyo tumechamkia fursa za China. Kwa mkataba huu, Marekani is just like a next door neighbor, tunafanya safari za non stop Dar-NY-Dar, wenzetu KQ wanafanya.
P.
KQ wanafanya waulize hasara wanayopata, Mmarekani aache kupanda Delta au Southwest kwenda Ulaya na kisha apande Emirates au Qatar kuja Afrika, kuna mikataba ambayo tunaweza kufaidika nayo lakini si ya anga ndege 2 ushindane na mababa yenye ndege zisizo na idadi+ huduma iliyotukuka
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
12,050
Points
2,000
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
12,050 2,000
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,441
Points
2,000
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,441 2,000
Naunga mkono hoja, miongoni mwa mikataba tulio ingia na Marekani ni mkataba wa Anga Huria uliosainiwa na Mkapa na Bush ambao unaruhusu ndege za Marekani kuingia kwenye anga la Tanzania wakati wowote na sisi ndege zetu kuingia Marekani anytime, wakati huo Tanzania tulikuwa hatuna ndege zenye uwezo huo, sasa tunazo, tuzitumie kwa wafabiashara wa Tanzania kuzichangamkia fursa za Marekani kama ambavyo tumechamkia fursa za China. Kwa mkataba huu, Marekani is just like a next door neighbor, tunafanya safari za non stop Dar-NY-Dar, wenzetu KQ wanafanya.
P.
Naunga mkono hoja. Wasiwasi wangu ni kuwa bila kuimarisha sekta zingine na kuja na mikakati ili ziwe tayari kufaidika na uwepo wa ATCL, ununuzi wa ndege unaweza kuwa 'hasara isiyo na faida'.

ATCL inabidi iwe cheaper kuliko mashirika mengine hata kwa usafiri wa ndani lakini iwe na ufanisi wa hali ya juu. Malengo makuu ya ATCL yawe kwa ajili ya kuboost sekta zingine hasa hasa kilimo na utalii na kuwe na mfumo rasmi wa kupima jinsi malengo hayo yanavyofikiwa. Kwa maana hiyo usafirishaji wa mizigo pia ungekuwa moja ya kipaumbele cha ATCL.

Pia tungeweka mfumo rasmi wa sekta za kilimo na utalii ku subsidize ATCL moja kwa moja kufidia gharama/hasara zake kwa sababu wao ndiyo wanatakiwa wawe wafaidika wa kwanza, ie. wadau namba moja.
 
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,441
Points
2,000
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,441 2,000
You are providing right remedy to a wrong malady.

Issues za royalties ni za taasisi za sanaa, hakimiliki na hakishiriki kuwa na mahusiano na similar taasisi overseas. Lakini kumbuka business model ya kazi za sanaa ilishabadilika saana. Kwa sasa sheria za kwetu zimepitwa na wakati na uhalisia.

Kwa mfano, siku hizi muziki hauuzwi sana. Mtu unapewa access to an "all-you can eat" repertoire of music you can listen to. Most are ad-supported or subscription-based.

Ndio maana hata kauli za kusema miziki inayopigwa kwenye kumbi ilipiwe, iko based on pre-internet realities. Siku hizi za Spotify, Mkito, Mdundo, Youtube na distributors wengine, watu wanaweka nyimbo zao ili ziwe played bure... how do you want someone to pay for a service already paid for via shitariki au matangazo?
Ni kweli tunajikongoja sana linapokuja suala la sanaa kwa ujumla. Bila wasanii wenyewe kusimama na kusema wanachotaka, serikali kamwe haitawaletea mabadiliko yanayohitajika. Suala la royalties bado linahitaji uwepo wa ushirikiano wa karibu kati ya TRA na IRS na ndiyo hapo tax treaty inapoingia. Hiyo haimaanishi vyombo vingine ya sanaa kama ulivyovitaja havitahusika.

Unajua fursa za muziki wa Kiswahili linaenda hadi kwenye soundtracks za filamu za Hollywood ambapo nadhani kuna fursa kubwa sana kwa muziki wetu hapo. Bila kuweka mfumo rasmi, rahisi na unaoeleweka na kuwa na ushirikiano wa karibu kati ya taasisi zetu na za Marekani, hizi fursa haziwezi kufunguka.
 
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,441
Points
2,000
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,441 2,000
Ukienda Marekani, unapewa maximum visa ya miaka miwili -- ukiwa ni Mtanzania. Ukiwa ni raia wa nchi nyingine, say, Jamaica, unapewa visa ya miaka 12 or something like that... Nasikia jamaa wanareciprocate the favors we give to their citizens. Probably we may need to look at whether we want things to be like this, and react accordingly.
Tatizo ninaloliona ni kuwa bado tunatazama utoaji wa viza kama chanzo cha mapato.
 
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,441
Points
2,000
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,441 2,000
Je wakipatwa na misukosuko huko kama inavyoendelea SA, serikali yetu itawatambua na kuwasaidia? Kuna kejeli nyingi zinaandikwa juu ya wahanga wa kitanzania kwenye vurugu zinazoendelea huko SA
Hatujawahi kuwa wazuri sana kuwasaidia Watanzania walio nje ya nchi. Kiufupi mfumo wetu wa mambo ya nje unahitaji mabadiliko ya kimtazamo na ya kiutendaji.
 
N

NewOrder

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
697
Points
500
N

NewOrder

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
697 500
Hili sio swala rahisi hivo hasa kama watanzania waishio nje wanachukuliwa kwanza kama sio wazalendo! Uzalendo ni kuishi Tanzania na kuitwa mnyonge!!

Pamoja na wazo hilo kuwa na faida kwa nchi, vipi haki za raia hao kupata haki za kiraia kama kupiga kura na kushiriki siasa kutoka nje?? Kama mjawaita mawakala wa mabeberu sijui!!

This is a give and take. Mpaka sasa hujapendekeza nchi itatoa nini kwa raia wake aliye nje!!
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
33,198
Points
2,000
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
33,198 2,000
Itapendeza sana... ngoja tuone...

Cc: mahondaw
 
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
5,389
Points
2,000
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
5,389 2,000
Kuna biashara kubwa inafanyika kati ya nchi hizi mbili na hasa toka kipindi cha Urais wa Kikwete tumekuwa kwenye msukumo wa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani. Mfano ni hivi majuzi tu kuna kundi la wafanyabiashara wa Marekani walifanya mkutano na wafanyabiashara na mamlaka mbalimbali mjini Dar es Salaam.

Cha kushangaza mpaka leo hakuna Income Tax Treaty kati ya Tanzania na Marekani.

Kwa mtazamo wangu, hili jambo linaweza kuwa na faida kubwa sana kwetu. Kwa mfano, hii itawalazimu Watanzania waishio Marekani ambao bado hawajaukana Utanzania kulazimika kudeclare kipato chao kila mwaka kwa TRA na pia kulipa kodi ndani ya Tanzania kila mwaka. Tunaweza kuamua labda hii hela iende katika mfuko maalumu kwa ajili ya kazi fulani mfano elimu ya juu au ya msingi.

Hata Wamarekani wanaoishi nje ya Marekani wanalazimika kila mwaka wajaze fomu kusema wameingiza kiasi gani na wanalipa kodi huko Marekani hata kama wameishi mwaka mzima nje ya nchi yao.

Kuna masuala ya malipo ya royalty mfano kwenye shughuli kama za sanaa. Itakuwa rahisi sana kwa wasanii wa Tanzania kufaidika na kazi zao zinapotumika nchini Marekani. Sasa hivi sijui ni utaratibu gani unatumika kwenye suala kama hili. Badala ya kila siku kuja na sheria za kubana watu, embu mara moja moja tuje na sheria za kumfaidisha Mtanzania.

Pia itasaidia kujua takwimu sahihi zinazowahusu Watanzania walioko huko Marekani kitu ambacho kwa sasa hatuna. Tumekuwa tunafanya makongamano mbalimbali ya Diaspora kila mwaka tukiongelea fursa za uwekezaji na jinsi gani tunaweza kuwatumia Watanzania walioko nje kwa fursa za kiuchumi zilizoko Tanzania.

Takwimu ni zaidi ya kujua tu kuna watanzania wangapi walioko nje ya nchi. Inabidi kujua kipato chao, kazi wanazofanya, elimu yao, nk. Hatuwezi kuja na sera sahihi bila kuwa na takwimu sahihi.

Kwa haraka haraka hizo ni faida za kuwa na hiyo Income Tax Treaty lakini kuna faida nyingi zaidi zilizo direct na indirect ya kuwa na hii kitu.
Income Tax Return wanafaidi wabunge wakurugenzi

Mfumo mbovu
 
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
2,724
Points
1,250
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
2,724 1,250
Ilitakiwa TRA iwe na verified account hapa JamiiForums ili iweze kutujibia maswali ya namna yanapojitokeza

Tatizo kubwa la JF wapo wengi zaidi hapa ambao wanaangalia matumbo yao. Wengi wao ni wafuata upepo hawaangali maslahi ya taifa. wanaangalia zaidi maslahi binafsi.
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
12,050
Points
2,000
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
12,050 2,000
Hatujawahi kuwa wazuri sana kuwasaidia Watanzania walio nje ya nchi. Kiufupi mfumo wetu wa mambo ya nje unahitaji mabadiliko ya kimtazamo na ya kiutendaji.

Sure!! Nilidhani tunahamasishana kuzaliana ili kuliimarisha taifa, kinyume chake hata raia waliopo hatuwathamini, je kuna haja gani kuhamasisha kuzaliana kama mwisho wa siku hatuthaminiani? Au tunahamasishana kuzaliana kumbe kiuhalisia tunamaanisha kuburudika?
 
Forum statistics

Threads 1,336,689
Members 512,697
Posts 32,547,763
Top