mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,960
- 2,464
mzee mwanakijiji mi sioni sababu za kufanya hivyo sisi kama tanzania, mwalimu alikuwa anapima nani anaonewa ndo anasasimama kwa upande unaoonewa, ndo maana alisimama upande wapalestina dhidi ya islaeli pia akaitambua BIAFRA KAMA NCHI katika ule mgogoro wa nigeria, sasa kwa upande wa libya kwa mtu mwenye akili zake hawezi kuwaunga mkono waasi sababu wale wanatumiwa na nchi za maghalibi kuleta uasi libya. kama basi kila anayeitwa dikteta na nchi za magharibi ni wa kumkataa basi angemkataa kamanda fidel castro. mi naona ni sahihi kwa tanzania kuwa na msimamo wake bila kuangalia nani yuko wapi, hao senegal na liberia wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, je unataka na sisi tuwatambue waasi kulinda maslahi yetu pasipokujali ukweli uko wapi?