Kwanini Tanzania haijavunja Uhusiano na Gadaffi?

Utawala alioupindua Gaddaf ulikuwa wa aina gani labda utusaidie kwenye hili, hizi nchi Dubai, China, Qatar, Saudia Arabia, Kuwait, Abu Dhabi, Korea Kaskazini, Urusi, Cuba, ni rafiki wa Marekani sijui wewe unaweza kutuambia lini walifanya uchaguzi wa kidemokrasia? Itabidi tuvunje nazo mahusiano
Hoja yako ni nzito sana Ritz. Ila Korea Kaskazini na Cuba kwa kipimo chochote kile si marafiki wa Marekani. Hata China na Urusi uhusinao wao na Marekani siyo wa kirafiki. Ni uhusiano usioepukika (friendship of convenience/necessity).
 
MWanakijiji, I believe this time you wrong about Libya and the so called pro-democracy rebels. Ukweli ni kwamba huo ni ukoloni unarudi kivingine, na historia iatashuhudia haya.
Say it again. Say it loud ......................
 
Hoja yako ni nzito sana Ritz. Ila Korea Kaskazini na Cuba kwa kipimo chochote kile si marafiki wa Marekani. Hata China na Urusi uhusinao wao na Marekani siyo wa kirafiki. Ni uhusiano usioepukika (friendship of convenience/necessity).
Mkuu,Hizo nchi nimeziweka makusudi ili nijenge hoja huyo member aliosema Libya aijawahi kufanya uchaguzi wa kidemokrasia kwa hiyo ni sawa tu tukivunja uhusiano, ndio maana nikaziweka hizo nchi vipi nazo tuvunje nazo uhusiano sababu azijawahi kufanya uchaguzi wa kidemokrasia
 
suala la Libya linatugawa kati ya wale tunaomwona ni dikteta na wale wanaomuona ni hero yaani ndg zetu Waslam kisa kawajengea misikiti na alikuwa ana-finance daily running ya Islamic institutions! Hizo ndivyo siasa zetu zilivyokuwa cheap kiasi cha haki ya wana-Libya wanaopigania Uhuru kuwa compromised kisa kujengewa nyumba za ibada na serikali ya dhalimu huyu wa wananchi wa Libya
 
Here you are againa Mwanakijiji na spinning zako

Kama kawaida kumtumia Mwalimu kuhalalalisha spinning zako. Hakuna kiongozi Afrika ambaye alikuwa mtata katika masuala ya siasa za kimataifa kama Nyerere. Alilazimu kuheshimu mipaka ya kikoloni lakini akaunga mkono kujitenga Biafara. Kitu ambacho hata yeye aliamini na kukiri kuwa anajichanganya. Alijitutumua na Ujamaa huku miradi yake yote ya ujamaa ikitegemea ufadhili wa mabebari. Alisiamama kidete kuunga mkono haki ya mataifa yote kuwa na sialaha za nyuklia huku akiwa mstari wa mbele katika kupigania dunia ya amani isiyo na ushindani wa silaha. Aliongoza mapambano ya haki kwa kila binadamu huku akivutiwa na "ujamaa" wa uzayoni wa kiisraeli (kibbutz) hadi pale Misri ilipoomba kuungwa mkono katika OAU baada ya Waisraeli kuteka maeneo yao lakini sio waisraeli walipoteka maeneo ya wapalestina na kuwakandamiza. ......Declaration: I am still die hard Nyerereist and unrepented Socialist....

Umeulizwa, mbona hatukutambua Rebels au magaidi wa RENAMO dhidi ya "ukandamizaji" na hata mauaji ya kimbari ya Frelimo huko Msumbiji tukaishia kupeleka maelfu wa majeshi yetu kumsadia Samora ambaye alikuwa tayari hata kufanya dili na Makaburu (Mkomati Accord). Lakini ni aibu kujaribu kufananisha POLISARIO ambao wanatetea uhuru wao kutoka kwa ukoloni wa taifa lingine (Morocco) au ANC ambao walikuwa wakipigana na makaburu waliokuwa wakiwakandamiza kutokana tu na rangi yao. No wonder kuna wehu hapa nchini wanaona ufahari kupeperusha bendera za Israel halafu wakajidai kuwa wao ni wazalendo wa Tanzania hihii iliyojengwa kwa misingi ya binadamu wote ni sawa na historia ya kupambana na ukoloni, ubeberu na ubaguzi......

Pitia historia kaka, tulijitoa Commonwealth kutokana na Uingereza kutukuwa tayari kuacha kumkumbatia Ian Smith na serikali yake ya masetla na sio Afrika Kusini.....

Hivi hujui msimamo wa Tanzania katika hili suala ama unataka kudanganya watu tu? Hivi ni nchi gani iliyo mstari wa mbee katika Umoja wa Afrika kukemea na kukosoa ubabe wa mataifa ya Magharibi huko libya kama sio Tanzania na Uganda ambao hapo kabla wote walikosewa na Ghadafi ambaye baadae alijirudi na kuwa rafiki wa kweli kwa mataifa hayo...Hivi kama sio sauti ya Tanzania katika msimamo wa mataifa yaliyo mengi Afrika ukitoa mataifa matano hadi nane kama Senegal, Liberia, Gambia, Rwanda, Malawi, Botswana, Guinea ya Obiang, Mama Clinton angekuja huku akitokea Qatar kujaribu kuokoa ushirika wao dhidi ya Ghadafi?

Enzi zina tofauti. Enzi ya sasa si ya kunyosha kidole na kupiga kelele (Activist politics) bali ni enzi ya constructive engegement with both friends and adversary...Kutosikika kwenye vyombo vya habari jinsi viongozi wetu wanavyopinga sera za hao jamaa zenu haina maana kuwa hatuwaambii pale wanapokosea.....Ukiwa kama mchambuzi wa siasa una wajibu wa kuuliza undani wa mambo hasa yale yasiopata headlines Mwanahalisi, CNN ama Aljazeera.....

Huu ni uongo wa wazi kabisa. Kama nilivyosema hapo kabla, Tanzania na Uganda ndiyo vinara wa msimamo wa AU kuwa mataifa hayo hasa Uingereza na Ufaransa wame abuse resotution ya UN kwa kiasi kikubwa, kuwa mataifa ya Magharaibi yanapaswa kutoa nafasi kwa suluhu la Kiafrika (Africa solutions) na kuwa AU haitatambua matokeo yoyote yatakayokuja bila ya kuhusisha pande zote huko Libya....

Cheap and medicore argument kaka.....Kama ni misaada ya magari ama msikiti kama anavyosema jamaa yako Matola imefanya Tanzania inyamaze kama unavyodai wewe kuisemea Libya, itawezaje kuacha kuunga mkono maslahi ya marekani waliosaidia zaidi ya billioni 400, Uingereza zaidi ya bilioni 250, Ufaransa ambao mara baada ya kuanza udhalimu wake huko Libya iliongeza mara mbili "msaada" wake kwa Tanzania kufikia zaidi ya bilioni 300?

Senegal - Huyu inaeleweka kuwa anajipendekeza kwa Sarkozy ili anyamaziwe atakapobadili katiba kujiongeza muda wa kutawala mwakani ama atakapomusimika mtoto wake kumrithi. Alipodai kuwa eti Ghadafi hajaisaidia Afrika kuliko Ufaransa na Uingereza akaulizwa ni wapi alitoa pesa za ule Mnara wa Africa Renaissance aliozindua kwa mbwembwe na nani alikuwa mstari wa mbele kugharamia Muungano wa Afrika na ni nchi gani inayolipa madeni ya mataifa zaidi ya kumi ya Afrika sio tu AU bali hata Umoja wa Mataifa na kuhakikisha nguvu ya sauti ya afrika inalindwa?

Liberia - Nchi pekee iliyotayari kuwa na AFRICOM huwezi kutegemea tofauti na msimamo huo. Bila ya kusahau historia yake na nini asili ya kina Serliff na wengine waliopita ukimtoa Doe

Gambia - Wote tunajua madudu yake na ni jinsi gani alivyo vulnerable na kimbunga hiki endapo hatakuwa loyal kwa maslahi ya wakubwa..

Rwanda - Historia inamtetea lakini pia tofauti yake na Ghadafi ni kuwa yeye ni msomi na udikteta wake una baraka za wakubwa lakini wote wanashabihiana katika kile tuitacho benign dictatorship ama falsafa ya udikteta poa

Guinea ya Obiang - huyu naye ni mmoja ya wale ambao kila mwanademokrasia anapoona anaungwa mkono naye inabidi ajiangalie mara mbilimbili....

Kwa kifupi kaka ni wazi kuna mengi ya kumsema Kikwete lakini msimamo wake katika masuala ya kiafrika bado anajitahidi kusimamia misingi ya taifa letu ingawa sio kwa style ya enzi za Mwalimu....

Omarilyas,

Some points nakubaliana na wewe ila kuna nyingine sikubaliani.Hebu tujadili katika optimism kwanza

Hapo kwenye utata wa Nyerere kwenye Siasa za Mataifa nakubaliana na wewe.Pia suala la armament and disamarment alikuwa na misiamo ambayo ni ambiguous sana ukilinganisha na wenzake kama akina Jawahlal Nehru.Nyerere na Nehru wanashabihiana sana katika influence yao kwa foreign policy ya nchi zao wakiwa madarakani.Wali-centralize foreign policy au walikua na strong hand katika hizo policy.

Pia msimao wa Nyerere ambaye alitaka kuunganisha mataifa umeshabihiana kwa kiasi fulani katika utata na wa Gadddaffi aliye-preach US-Africa at the same time akatoa ushauri kuwa Nigeria Igawanywe.Pia ali-play Role kubwa sana kwenye partition ya Sudan.

Ndiyo maana nimesizitiza ni lazima tujaribu kuframe rigid foreign policy lakini ambayo ni flexible kwa zile primary and secondary National interests tu.

As For Toothless Body,UN: Sote tunatambua Resolution 1973 haiko properly executed,na hapa ndipo ninapojenga hoja za kuondoa Veto power na ku-expand National Security council ili tuepushe UN kutumika vibaya na Major Powers.Ninaandaa makala mfululizo zitakazochapishwa kwenye international journals zitakazokuja kuunganishwa baadae niandike kitabu.UN inastahili kufanya nini sasa ili kuepuka yaliyotokea tukawa na Korea mbili,au vita ya Vietnam ikatokea.Tusirudi kule kule,The rising of China is a threat .Redback(China) Vs Greenback(The united states) with their interwoven political-economical ideologies most likely tutarudi kwenye terrible state kuliko ya Cold war,ukizingatia kundi la BRIC nalo limeshtuka.Ni lazima UN Security council ifanyiwe Radical reforms
 
Hapo (kwenye red) ndipo mimi nachanganyikiwa pia! Kwa hiyo wewe unashauri tufuate vyombo vipi vya habari!!??? ...si ndiyo hivyo bali cha msingi badala ya kiviona kama 'not independent and objective sources of information' ni bora 'uweka zako' kama Mbayuwayu!
Nakubaliana na kuchanganyikiwa kwako kwa kiasi fulani. Kwa sababu miaka zaidi ya 50 baada ya nchi nyingi za KiAfrika kupata uhuru hatuna reliable news agency au electronic media ambayo inaweza kutupa taarifa zenye mtazamo wa bara la Afrika. Ni upungufu na aibu kubwa. Ukweli ni kwamba vyombo vya habari vya nchi za magharibi ni vyombo vya kuendeleza maslahi ya mataifa yao. Obama akisema Gaddafi muuaji usitegemee CNN, ABC au FOX waseme Gaddafi ni muungwana. Tony Blair aliposema Saddam Hussein ana silaha za maangamizi na mkurugenzi mmoja wa BBC akatoa taarifa zinazopingana naye tunajua lililomtokea. Lakini ukweli na usahihi wa yule mtu ulikuja kujulikana baadae. Si vyombo vya habari tu. Hata mashirika ya "kutetea haki za binadamu" kama Human Rights Watch na Amnesty International mitazamo yao ni ile ile inayosupport misimamo ya serikali zao. Hutayasikia hata siku moja yanasema George Bush na Tony Blair wapelekwe The Hague. Lakini mara Gaddafi anapolaumiwa tu na serikali zao wanalivalia bango Gadadfi kupelekwa THe Hague hata kama hakuna ushahidi wowote. In fact yenyewe ndiyo yatatumiwa kutengeneza ushahidi wa uongo.
 
Tuvunje uhusiano ili iweje?
Tuwakubali waasi kwa misingi ipi? tusiburuzwe na kila wanalotaka nchi za Magharibi. Hata huyo Nyerere angekuwepo asingeunga mkono ijapokuwa alikuwa na ugomvi na Ghadafi miaka hiyoo zama zimebadilika. Hatuwezi kuwa vibaraka wa nchi za Magharibi
 
Wenye akili wanasema "ni afadhali mtu anayefanya maamuzi mabaya kuliko yule asiyefanya maamuzi kabisa". Kweli katika hili uongozi wetu umeonyesha kuwa sisi ni ndumilakuwili wa ajabu kabisa. Nadhani kama nchi ilipaswa itoe msimamo wake, kama upande wa Waasi au wa Gadaffi.

Kwa upande wangu naona hawa waasi ni vibaraka tu wa mataifa ya wakubwa. Naona kuna hatua ya maksudi katika kuhakikisha kuwa huyu bwana mkubwa anaondolewa madarakani. Kwani yeye kosa lake kubwa ni nini hasa?

Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa Libya ni moja ya nchi za kiafrika zenye maisha mazuri sana. Ghadaffi amejitahidi sana kuibadilisha nchi hiyo na kuwaletea maendeleo wananchi wake. Amekuwa mstari wa mbele kabisa katika kutetea maslahi ya waafrika dhidi ya mataifa yanayotaka kunyonya utajiri wao. Na hiyo ndo dhambi yake kubwa kabisa.

Sasa katika yote hayo ilibidi nchi yetu itoe msimamo wake kuhusiana na hili. Kama ni upande wa Ghadaffi basi waseme au upande wa waasi. Hatutakiwi kubaki vuguvugu hata siku moja. Huu ni unafiki uliozidi kiwango.
 
Mzee mwanakijiji... nataka kukumbusha ... msimamo wa serikali ya tanzania ni msimamo wa AU.. hata kesho AU wakisema hatumtambui ghadafi basi automatically huo ndio utakuwa msimamo wa serikali yetu ya tanzania
 
Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.

Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).

Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.

Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?

Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?

MMM Ni kweli sera zetu za mambo ya kigeni kwa sasa ni utata mtupu!! Lakini ukiacha hilo, mie binafsi NAPINGA KWA NGUVU ZOTE KITENDO CHA KUWATAMBUA WAASI WA BENGHAZI LIBYA.. Hakuna ushahidi unaojitosheleza kumhukumu Ghaddafi kama wa-Magharibi wanavyofanya..

1. Kama kweli wananchi wa Libya wamemchoka Ghaddafi, kwa nini mabomu ya NATO yatumike kumwondoa Ghaddafi, Nguvu ya Umma iko wapi???

2. Kwa nini BBC, CNN na vyombo vingine wanatunga story za kipuuzi ili kuhalalisha uvamizi?? Toka lini uvamizi ukathibitishwa na vyombo vya habari tu, bila vyombo vya ki-intelijensia kutoa ushahidi wa kuhalalisha uvamizi?? Hata hivyo story za western media haziko balanced na wanatunga uongo mwingi tu..

3. Kwa nini NO-FLY-ZONE, Imegeuka kuwa Regime change?? Kwa nini western waingilie kiasi hichoo?? Kwa nini waasi kwa haraka haraka wanaanzisha serikali yao, Je, walibya wote wamekubaliana na hili???? Kwa nini Ghaddafi asingetoka kama ilivyofanyika Egypt na Tunisia???
 
Mwanakijiji
Unataka Ghadafi aondoke Madarakani kwa sababu zipi za msingi?
Kwamba ni dictator, well tuna madictator wangapi africa?

Mimi simlinganishi Ghadafi na kiongozi hata mmoja wa kidemocrasia
katika Bara la Africa. Zipangeni serikali zooote za africa kisha mniambie ni
ipi inaweza ikafikia japo asilia 30% ya ufanisi wa serikali ya Ghadafi katika
kutumikia wananchi wake, there after, nnaweza kuwasilikiliza juu ya swala
udictator.

By the way what do we need the governments and heads of state for?
hasn't this man delivered on his duties beyond expectations?
Every Citizen has a home
No one person in his landis is deemed to be poor
Free high quality health care
Free education
Very stable economy
the land with the lowest level of criminal cases
Water is flowing into the deepest part of the desert.

Haya ndio mambo ambayo watanzania tunalalamika
kila siku kwamba serikali yetu imeshindwa kutupatia,
Libya yanapatikana in prenty, and you want this president
out.

Tuyapime mema ya Ghadafi na Mabaya yake kisha tumuhukumu
ama sivyo his blood will be required from our hands.
na katika hili Mwanakijiji damu ya watu wanaowawa LIBYA
itatakiwa mikononi mwako.
 
Si ajabu mwanakijiji anaamini zile habari , zilizorushwa kwenye BBC, Al-jazeera, Yahoo, habari za Ghadafi kuwapa Askari wake Viagra ili wawabake wanawake wa Libya kama adhabu ya kuunga mkono waasi!- just thinking though
 
MWanakijiji, I believe this time you wrong about Libya and the so called pro-democracy rebels. Ukweli ni kwamba huo ni ukoloni unarudi kivingine, na historia iatashuhudia haya.

Mkuu, ingawa mimi siyo Mwanakijiji, lakini kwavile nimeisoma huu uzi, naomba nimsaidie!!

Dukuduku kubwa la Mwanakijiji ni kwamba kwanini serikali ya Tanzania chini ya Kikwete ipo kimya juu ya suala la Libya?
Kwanini serikali haisemi kama inawaunga mkono wapambanaji wa Benghazi au inamuunga mkono Gaddafi na serikali yake?

Hiyo ndio hoja ya Mwanakijiji, nilivyomuelewa!
 
mzee wa kijiji
mbona wewe huvunji uhusiano wako na chadema. watakuja kuchukua dola zao elfu kumi walizokutoa lupango kwa kuishi nchi za watu bila papers.
tanzania nayo imesaidiwa sana na gadaffi na wanajikuta wamenasa. njaa kitu mbaya baba.

J, ukizungumzia kuhusu njaa; kuna wengine wana njaa za familia nzima. Kama mtu ambaye dadake anauza favors mbalimbali na sasa she is ready to cash in kwenye dola laki tano za kujenga kibanda huku kaka mtu akichangamkia tenda ya "shamba" huko Iringa. Ukizungumzia njaa kuna watu hasa wana njaa zao.
 
Hapo kwenye Red mkuu,nilishtuka sana.Kissinger bado yuko hai.Na bado ni jembe kwenye Diplomacy,kwa kweli kama kuna wanadiploamsia nawahusudu kwa uzalendo wao kwa mataifa yao ni Kissinger.The guy is still alive,hata juzi alikuwa toronto canada kwenye mdahalo vs Ferguson a proffesional Historian.Kissinger ali-debate vizuri kuhusu Role ya China katika dilution of unipolarism.Alisema China haiwezi kuwa superpower kutokana na kuwa inastahili kuweka political institutions in place kabla ya ku-concentate on building the world dominannce.Kwa kweli hii ni lugha kali ya kipropaganda katika diplomasia.Tuachane na hili

Yeah, ni kweli kama sitakosea aliyefariki ni Warren Christopher.
 
MWanakijiji, I believe this time you wrong about Libya and the so called pro-democracy rebels. Ukweli ni kwamba huo ni ukoloni unarudi kivingine, na historia iatashuhudia haya.

Ukoloni hauitaji kurudishwa kwa bunduni na risasi; ukoloni unakaribishwa kwa kukaa chini na kutiliana mikataba kama walivyofanya kina Karl Peters. Tofauti ni kuwa mababu zetu enzi za Karl Peters walikuwa na udhuru wa kusema hawajui mikataba waliyosaini ilikuwa inatoa nchi yao kwa wageni, leo hii hatuna udhuru huo na hivyo tunakaribisha ukoloni tukijua wazi kabisa tunachokifanya.
 
J, ukizungumzia kuhusu njaa; kuna wengine wana njaa za familia nzima. Kama mtu ambaye dadake anauza favors mbalimbali na sasa she is ready to cash in kwenye dola laki tano za kujenga kibanda huku kaka mtu akichangamkia tenda ya "shamba" huko Iringa. Ukizungumzia njaa kuna watu hasa wana njaa zao.
Siri nje nje
 
Yeah, ni kweli kama sitakosea aliyefariki ni Warren Christopher.

Ni kwa wale wasioona tu ndiyo wanaunga mkono waasi wa Libya na ndugu zao wa NATO. Mapinduzi hayaji kwa kuiga kilichofanywa Tunisia na kifanyike Libya. Waasi, NATO na vitaifa vya kijinga vya kiarabu vinafanya biashara ya damu katika mafuta. NATO na Waasi lao moja siyo kulinda raia ila ni kuua na kubomoa Libya.
Nani asiyejua kwamba mataifa ya magharibi hayataki Afrika iendelee? Imefikia mahali NATO wanafikiri libya siyo Afrika ila ni Mashariki ya kati!!! Wajinga kweli wa dunia. Tatizo wanaokwenda kusoma huko ulaya wanalogeka kabisa kufikia hatua ya kuona kila kitu wafanyacho hawa wajinga NATO ni sahihi.
NATO wanataka mafuta na si vinginevyo. Libya iling'ara sasa wanaharibu na hata hao waasi ni madaraka tu wanataka maana walinyang'anywa toka kwa sultan wao wa Benghazi. Na ndo maana wameanzia kule kwa sultan wao Benghazi na bendera yake ikipepea. Wahuni hawa.... Nyerere alijihusisha na watu walionyonywa na wala si waasi kama wa Libya.
Kama wanataka madaraka basi iwe somalia ya pili kila mmoja atawale kaeneo kake na pirates waanze hapo medteranian.
 
Here you are againa Mwanakijiji na spinning zako

Unatakiwa kushambulia hoja na kuifanya hoja yangu kuwa dhaifu; hoja yako haiwi na nguvu kwa kumbeza mwanakijiji. Inaonesha tu kuwa inahitaji nguvu nje ya nguvu zake kuweza kuilazimisha ikubalike.

Kama kawaida kumtumia Mwalimu kuhalalalisha spinning zako. Hakuna kiongozi Afrika ambaye alikuwa mtata katika masuala ya siasa za kimataifa kama Nyerere. Alilazimu kuheshimu mipaka ya kikoloni lakini akaunga mkono kujitenga Biafara. Kitu ambacho hata yeye aliamini na kukiri kuwa anajichanganya. Alijitutumua na Ujamaa huku miradi yake yote ya ujamaa ikitegemea ufadhili wa mabebari. Alisiamama kidete kuunga mkono haki ya mataifa yote kuwa na sialaha za nyuklia huku akiwa mstari wa mbele katika kupigania dunia ya amani isiyo na ushindani wa silaha. Aliongoza mapambano ya haki kwa kila binadamu huku akivutiwa na "ujamaa" wa uzayoni wa kiisraeli (kibbutz) hadi pale Misri ilipoomba kuungwa mkono katika OAU baada ya Waisraeli kuteka maeneo yao lakini sio waisraeli walipoteka maeneo ya wapalestina na kuwakandamiza. ......Declaration: I am still die hard Nyerereist and unrepented Socialist....

Ukizungumzia kujichanganya hii inaweza kuwa ni mfano usio na mfano.

Umeulizwa, mbona hatukutambua Rebels au magaidi wa RENAMO dhidi ya "ukandamizaji" na hata mauaji ya kimbari ya Frelimo huko Msumbiji tukaishia kupeleka maelfu wa majeshi yetu kumsadia Samora ambaye alikuwa tayari hata kufanya dili na Makaburu (Mkomati Accord). Lakini ni aibu kujaribu kufananisha POLISARIO ambao wanatetea uhuru wao kutoka kwa ukoloni wa taifa lingine (Morocco) au ANC ambao walikuwa wakipigana na makaburu waliokuwa wakiwakandamiza kutokana tu na rangi yao.

Kama wewe ni Nyerereist kama unavyodai huwezi kuona utata katika hayo yote unayoyasema.

No wonder kuna wehu hapa nchini wanaona ufahari kupeperusha bendera za Israel halafu wakajidai kuwa wao ni wazalendo wa Tanzania hihii iliyojengwa kwa misingi ya binadamu wote ni sawa na historia ya kupambana na ukoloni, ubeberu na ubaguzi......

Tanzania hii kweli imejengwa hivyo? Hii ambayo inashindwa kutambua uabguzi na ukandamizaji unaofanyika leo hii sehemu mbalimbali duniani? Hii ambayo imeshindwa kutoa kauli yoyote ya kupinga mashambulizi ya NATO na US huko Libya, Afghanistani n.k? Kama ilivyoshindwa kutoa kauli yoyote dhidi ya Iran, Bahrain au Saudia? Is this the neutrality of the principled or the neutrality of the cowards (assuming cowards can be neutral!)

Pitia historia kaka, tulijitoa Commonwealth kutokana na Uingereza kutukuwa tayari kuacha kumkumbatia Ian Smith na serikali yake ya masetla na sio Afrika Kusini.....

Absolutely, lakini Tanzania ilikuwa inapata misaada toka Uingereza! Kitu gani kilitufanya tuthubutu kwenda nje ya "wakubwa" ambao tulikuwa tunawategemea kwa misaada?

Hivi hujui msimamo wa Tanzania katika hili suala ama unataka kudanganya watu tu? Hivi ni nchi gani iliyo mstari wa mbee katika Umoja wa Afrika kukemea na kukosoa ubabe wa mataifa ya Magharibi huko libya kama sio Tanzania na Uganda ambao hapo kabla wote walikosewa na Ghadafi ambaye baadae alijirudi na kuwa rafiki wa kweli kwa mataifa hayo...Hivi kama sio sauti ya Tanzania katika msimamo wa mataifa yaliyo mengi Afrika ukitoa mataifa matano hadi nane kama Senegal, Liberia, Gambia, Rwanda, Malawi, Botswana, Guinea ya Obiang, Mama Clinton angekuja huku akitokea Qatar kujaribu kuokoa ushirika wao dhidi ya Ghadafi?

I wish you were serious on this one. Tanzania kuna kivuli cha Nyerere bado! Bado wapo watu wanaofikiri Tanzania yenye clout iliyiokuwa nayo wakati wa Mwalimu bado ipo. Kikwete kama ilivyokuwa Mkapa kabla yake hana uwezo wa kuchukua msimamo based on our national values. Hawawezi kwani wakifanya hivyo wanaweza kujihisi wanabanwa na ni kweli Tanzania ikianza kuchukua msimamo dhidi ya Marekani au Uingereza leo hii itaanza kubanwa kwenye misaada!

Enzi zina tofauti. Enzi ya sasa si ya kunyosha kidole na kupiga kelele (Activist politics) bali ni enzi ya constructive engegement with both friends and adversary...Kutosikika kwenye vyombo vya habari jinsi viongozi wetu wanavyopinga sera za hao jamaa zenu haina maana kuwa hatuwaambii pale wanapokosea.....

Enzi hizi ni enzi za kupiga kelele (active activism) siyo enzi za kulalamika sirini au kunong'onezana sirini. Watawala wetu hawapingi sera za hao jamaa zaidi ya kubembeleza. Wanazipinga based on what principles? Tusaidie kutuambia ni principles gani zinawaongoza kuwapinga hao jamaa zako?

Ukiwa kama mchambuzi wa siasa una wajibu wa kuuliza undani wa mambo hasa yale yasiopata headlines Mwanahalisi, CNN ama Aljazeera.....

Unlike you, I don't depend on MwanaHalisi, CNN au Aljazeera kujua serikali inafanya nini. You should know that by now.

Huu ni uongo wa wazi kabisa. Kama nilivyosema hapo kabla, Tanzania na Uganda ndiyo vinara wa msimamo wa AU kuwa mataifa hayo hasa Uingereza na Ufaransa wame abuse resotution ya UN kwa kiasi kikubwa, kuwa mataifa ya Magharaibi yanapaswa kutoa nafasi kwa suluhu la Kiafrika (Africa solutions) na kuwa AU haitatambua matokeo yoyote yatakayokuja bila ya kuhusisha pande zote huko Libya....

What on earth is so called African solution? Ni ile ambayo Zuma alienda nayo Libya na kupendekeza kuwa ni suluhisho la Africa? Kwanini Tanzania haijaonesha njia ya kutafuta hilo suluhisho la Africa? Yaani, leo Uganda inaweza kusimama usawa mmoja na Tanzania katika diplomasia ya Kimataifa? Tanzania kutokana na hicho nilichokisema hapo juu ilitakiwa iwe kiongozi; once we were leaders leo tunafuata- na hapo tujisikie vizuri?

Cheap and medicore argument kaka.....Kama ni misaada ya magari ama msikiti kama anavyosema jamaa yako Matola imefanya Tanzania inyamaze kama unavyodai wewe kuisemea Libya, itawezaje kuacha kuunga mkono maslahi ya marekani waliosaidia zaidi ya billioni 400, Uingereza zaidi ya bilioni 250, Ufaransa ambao mara baada ya kuanza udhalimu wake huko Libya iliongeza mara mbili "msaada" wake kwa Tanzania kufikia zaidi ya bilioni 300?

Acha kushakizia wetu "jamaa yako", "jamaa zenu" ni urahisishaji wa hoja. Hoja yangu ihukumiwe nilivyoiweka mimi sasa hayo mambo ya Misikiti au Kliniki haihusiani na kile nilichokisema. Kama Tanzania inaamini Ufaransa inafanya vibaya na inaonea Libya au hata baada ya haya mabomu yaliyoua raia tisa kwanini Tanzania isitoe kauli yake kuonesha displeasure na hata ikibidi kukataa misaada ya Ufaransa? Haiwezi kwa sababu hatuna viongozi wenye kuthubutu kuchukua msimamo wa namna hiyo na kuwa tayari kulipa gharama yake. Si unakumbuka tulivyovunja uhusiano na Ujerumani Mashariki?

Senegal - Huyu inaeleweka kuwa anajipendekeza kwa Sarkozy ili anyamaziwe atakapobadili katiba kujiongeza muda wa kutawala mwakani ama atakapomusimika mtoto wake kumrithi. Alipodai kuwa eti Ghadafi hajaisaidia Afrika kuliko Ufaransa na Uingereza akaulizwa ni wapi alitoa pesa za ule Mnara wa Africa Renaissance aliozindua kwa mbwembwe na nani alikuwa mstari wa mbele kugharamia Muungano wa Afrika na ni nchi gani inayolipa madeni ya mataifa zaidi ya kumi ya Afrika sio tu AU bali hata Umoja wa Mataifa na kuhakikisha nguvu ya sauti ya afrika inalindwa?

Liberia - Nchi pekee iliyotayari kuwa na AFRICOM huwezi kutegemea tofauti na msimamo huo. Bila ya kusahau historia yake na nini asili ya kina Serliff na wengine waliopita ukimtoa Doe

Gambia - Wote tunajua madudu yake na ni jinsi gani alivyo vulnerable na kimbunga hiki endapo hatakuwa loyal kwa maslahi ya wakubwa..

Rwanda - Historia inamtetea lakini pia tofauti yake na Ghadafi ni kuwa yeye ni msomi na udikteta wake una baraka za wakubwa lakini wote wanashabihiana katika kile tuitacho benign dictatorship ama falsafa ya udikteta poa

Guinea ya Obiang - huyu naye ni mmoja ya wale ambao kila mwanademokrasia anapoona anaungwa mkono naye inabidi ajiangalie mara mbilimbili....

Kwa kifupi kaka ni wazi kuna mengi ya kumsema Kikwete lakini msimamo wake katika masuala ya kiafrika bado anajitahidi kusimamia misingi ya taifa letu ingawa sio kwa style ya enzi za Mwalimu....

Mifano mizuri kweli lakini hujamalizia nchi zote ambazo zimetambua Baraza la Mpito la Libya.

Nchi nyingine ni:
United Arab Emirates ambayo Tanzania ina uhusiano nayo wa karibu sana
Jordan
Kuwait

Nchi nyingine zimevunja uhusiano na Gadaffi bila kutambua Baraza la Mpito; miongoni mwa hizo ni pamoja na
Malawi
Tunisia
Arab League wao wamesema Gadaffi amepoteza legitimacy na watashirikiana na Baraza la Mpito.

Hivyo, si lazima kutambua Baraza la Mpito baada ya kuvunja uhusiano na Gaddafi; Kuna njia nyingi ambazo tayari nchi mbalimbali zimechukua kuonesha kupinga Gaddafi alivyowashell wananchi wake yeye mwenyewe. Tanzania ilikataa hili hili kwenye suala la Biafra (kama kweli unajua historia utakumbuka jinsi gani Nyerere aliumizwa na kuchukua msimamo wa kuitambua Biafra na reasoning yake - ambayo ni ile ile aliyoitumia kwenye Morocco na Palestina na Afrika ya Kusini!).

Leo watawala wetu (sidhani kama kuwaita viongozi inawastahili - kwani viongozi wanatakiwa kuongoza siyo kufuata) wanashindwa kuchukua msimamo based on our national value and our historical roles we have paid in the past. Kama mtu mwingine alivyosema nami kuweka kauli yake kwenye signature yangu kama Tanzania na viongozi wake wanaamini kuwa nchi za Magharibi zinaionea Libya na kuwa Gadaffi anaonewa tu kwa kutetea misimamo ya wanyonge then Tanzania itoke wazi na kutamka hivyo na kuarticulate its reasoning na sisi wengine tukishawishiwa tutasimama na nchi yetu.

Hufikiri kuwa ni vizuri TAnzania ijitokeza na kumuunga mkono Gadaffi na serikali ya Libya ili msimamo wake ujulikane? Au unaona ni vizuri kwa viongozi wetu kutokuonekana wana msimamo wowote ule isipokuwa ule wa siri ambao wao (na siyo wananchi wao) wanaojua? Je kama Watanzania hatuna haki ya kujua serikali yetu ina msimamo gani kuhusu Libya na Gaddafi kuilngana na tunu zetu za kitaifa?
 
Mag3 amesema hivi kama tunaunga mkono Libya iwe wazi na MMKJ kauliza kwanini tusivunje uhusiano na Libya? Kwa lugha nyepesi wote wawili na ninawaunga mkono wana mantiki kuwa nini msimamo wa taifa letu katika diplomasia siku hizi? Tumekuwa watu wa kujibanza ukumbini kwa kivuli cha AU na UN. Umasikini siamini kuwa ni sababu,enzi za mwalimu tulikuwa hivyo hadi kufikia mahali Tanzania ikaitwa Masikini Jeuri, tena kwa heshima. Huenda hili la kutembeza bakuli kudunduliza ndilo linatukwaza, yaani omba omba na umatonya.

Wanaosema eti tukae kimya kulinda maslahi nawashangaa, mwaka 1965 tulimwambia mwingereza aliyekuwa anatoa 1/2 ya bajeti yetu, No! tunavunja uhusiano kwa suala la South Rhodesia. Tukamtimua Mwi-Israel aliyekuwa anasimamia miradi kadhaa nchini kwasababu ya Palestina.
Tukamwambia Henry Kissinger, tunataka unga wa yanga na bulga lakini kwa siasa zako za kibeba na za kumuunga mkono kaburu Big No. n.k

Ivory coast, inatumika ili kujenga ubaya. Ukweli ni kwamba nchi za magharibi zilipoanza kuingilia kati AU wakasema 'this is Africa problem, it needs Africa solution'. Wakaunda tume akiwemo Kikwete na Membe. Mauaji yakaendelea huku JK akitabasamu na Bagbo, membe akikatiza anga kutafuta solution asiyoijiua. Hakukuwa na Africa solution yoyote ile hadi pale mfaransa alipoingilia kati tena kwa maagizo ya wakubwa. Sasa tuna fail ku deliver as AU tunalaumu western countries! c'mom.

Ni kutafuta visingizo ndiyo maana watu wanasema Libya is all about Oil. Wanasahu kuwa Ghadaffi ana bifu la Lockerbie Bombing na ni threat kwao. Wanasahau kuwa Ghadaffi aliwahi ku develop nuclear wepons na ilikuwa katika hatua za enrichment. Lakini watu wanasahau kuwa kiongozi anayetumia ndege kuua watu wake inatisha zaidi!!

Tunasahau kuwa ni NATO walikomesha mauaji kule Bosnia ambayo ethenic cleansing ilifikia alarming state. kuna mafuta kule.
Tunaposema waasi tuwe waangalifu maana jasmine revolution sio FRODEB au banyamulenge ni regional uprising, kwanini tuite waasi wa Libya na si wa Egypt au Tunisia n.k!

Ni ukweli usio na shaka kuwa sasa tumepoteza nguvu ya hoja kama taifa, tumepoteza thamani zetu kama watu huru. Siasa zetu chini ya membe zimekuwa ni kama alivyosema Ben Saanane, '' tuna unga mkono hoja ya maziwa makuu, tunaunga mkono AU, tunaunga mkono UN resolution against Libya' halafu tunanung'unika ah hii si sahihi ni kwa ajili ya mafuta n.k.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom