Kwanini TANESCO hawatangazi ratiba mgao wa umeme?

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,044
2,000
Kila mkoa kuna majanga ya kukatika umeme kila pasipo ratiba maalumu na kusabisha usumbufu hasa kwa wenye salooni na wachomea vyuma na hata shughuli zingene kusimama.
Natoa wito kwa TANESCO kutoa ratiba ya mgao ili sisi wateja wao tuweze kupanga mpangilio kwa kazi.
 

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,576
2,000
Mkuu usijisumbue hata mimi nilishawakwenda kwenye ofisi zao na kuwauliza kuwa kwanini hawatoi ratiba ya mgao wa umeme wakanijibu kuwa hata wao huwa hawajui umeme unazimika saa ngapi au siku gani! Endelea kuwa mpole tu!:confused2:
 

chuse tbr

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
430
500
mboma kwetu unakatika kila siku saa moja jioni na unarudi saa saa tano usiku na tushazoea hata kama hatujatangaziwa mtu anaekaa kinondoni studio ama mkwajuni analijua hili yani inaboa ile mbaya na ondoke tu huyo waziri
 

TECHMAN

JF-Expert Member
May 20, 2011
2,658
1,250
Mbona profesa mwongo alidai hakuna mgawo wa umeme?
Nani kakwambia huu ni mgawo? Kawaida unagawa kile kidogo ulichonacho, sasa kama huna kitu unagawa nini? Hakuna umeme ndo maisha ukiwaka ni bahati mbaya, siku hizi watoto hawashangilii umeme ukirudi wanashangilia ukikatika, maana ukirudi wanakuwa washalala
 

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,505
2,000
Mi nalia na haya mashirika ni kutokuwa na page katika mitandao ya kijamii,ingesaidia sana,mfano ilala kule fb unakuta tanesco ilala inakuwa rais kwa wakazi wa ilala kujua na kupangilia mambo yao umeme unapokatwa ,pia ingewasaidia tanesco kuwafikia wateja wao,si tanesco hata uda,yale matren ya ndani ya jij yangesaidia kupunguza usumbufu kama wangekuwa wana page zao kwenye mitandao ya kijamii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom