Kwanini taifa la Amerika (USA) lina nguvu kwa mengi kuliko mataifa mengine nini kilijiri huko nyuma na sasa?

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,023
Nimekuwa najiuliza siku nyingi sana kwanini taifa hili siku zote linatamkwa kuwa ni taifa kubwa lenye nguvu kiuchumi duniani na hata kijeshi.

Hata ukiangalia ugunduzi wa mambo mengi ya kisayani utasikikia yameanzia Amerika.Limekuwa taifa la kwanza kumtuma binadamu wa kwanza kukanyaga mwezini na alipokuwa kule akampigia raisi wake simu Richard Nixon wakaongea akiwa ofisini kwake oval office.

Super power wa kwanza walikuwa warumi miaka ya YESU wakati wake na kabla yake kuja kibao kimebadilika imekuwa Amerika.

Wingereza naweza kusema ndio taifa la wajanja toka miaka mingi ya nyuma limetawala karibia nusu ya dunia na wamewatawala hata wamarekani wenyewe lakini bado limekuwa nyuma ya USA kwa sasa.

Nchi hii ya Amerika ilikuwa haijulikani kwenye ramani ya dunia kuwa ipo kulikuwa na wahindi wekundu lakini siku zilivozidi kwenda limezidi kung'ara nini hasa sababu kuu za wao kuwa juu kiasi hiki.

Naombeni tupeane elimu katika hili
 
Jibu ni rahisi tu, waliojenga Ulaya ndiyo walioijenga USA, ni sawa na leo hii kuchukuwa Wajapani ukawakabidhi nusu ya Afrika kuanzia Kongo mpaka AK baada ya miaka 50 hili eneo litakuwa ni moja kati ya mataifa tajiri Duniani kuliko hata Ujapani yenyewe, kwa maana nyingine ni sawa na kuuliza kwa nini AK ndiyo nchi tajiri kuliko zote Afrika, hivyo kwa kifupi ni swala la Utamaduni tu!
 
Vita vya pili viliathiri sana mataifa makubwa ya ulaya....ilipelekea mataifa mengi kufirisika....kwa sabab marekan hakushiriki moja kwa moja kwenye vita hivyo akapata upenyo wakuongeza nguvu nakuanza kuwauzia bidhaa mataifa yalio kwenye vita....
 
Jibu ni rahisi tu, waliojenga Ulaya ndiyo walioijenga USA, ni sawa na leo hii kuchukuwa Wajapani ukawakabidhi nusu ya Afrika kuanzia Kongo mpaka AK baada ya miaka 50 hili eneo litakuwa ni moja kati ya mataifa tajiri Duniani kuliko hata Ujapani yenyewe, kwa maana nyingine ni sawa na kuuliza kwa nini AK ndiyo nchi tajiri kuliko zote Afrika, hivyo kwa kifupi ni swala la Utamaduni tu!
Jibu tamu sana asante kwa mchango wako
 
KASOME HISTORIA A LEVEL HUKO UTAPATA MAJIBU. UKISHNDWA INGIA LIBRARY, KAPITIE PITIE HISTORIA YA ULAYA, AMERIKA NA AFRIKA
 
Back
Top Bottom