Kwanini taasisi kama TRA, NSSF, TPA na zinginezo zisiwe na timu za mpira wa miguu?

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Jul 2, 2019
910
1,394
Ukiangalia kwa makini kwenye huu ukanda wetu wa Afrika Mashariki na KATI na hata Afrika kwa ujumla wake, soka linaendeshwa sana sana na Taasisi za Serikali, watu binafsi wenye hela na makampuni maana ndo waajiri ambao wana uhakika wa kulipa mishahara na kuhudumia timu kwa uhakika.. ZAMBIA na UGANDA ni mifano ya haraka kuangalia na ndo zimefanuikiwa kisoka kwenye nchi majirani kwetu.

Kwanini hapa kwetu TANZANIA taasisi kama TRA, NSSF, TPA na zingine ambazo kwa kifupi zinaingiza mapato, zisiingilie SOKA la Tanzania ambalo bado linahitaji nguvu ya pesa kwenye kuliendesha na kulifanya liwe shindani zaidi?
 
Swali ni kwanini wawe na timu za mpira?

Kwanini sio michezo mingine ambayo bado inachechemea?

Kila taasisi unataka iwe na timu? Mapenzi yako ya mpira yanafanya usione zaidi ya mpira.

Unatolea mfano ZA na UG, upo serious kweli mkuu? Soka la hizo nchi limefika wapi kwa mfano? Wachezaji wao wakubwa wanaota kuja kucheza bongo.

Hizo taasisi zijikite kulipa watu mafao kwa wakati na kutoa huduma bora. Sio lazima kila mtu aingine michezoni. Labda wajenge viwanda kama alivyoshauri mwendazake vitaajiri watu wengi zaidi na kukuza uchumi.
 
Mbona bado kuna timu za Taasisi za kiserikali na binafsi kama Prisons, Polisi, JKT, Mtibwa, Rhino, Kagera, KMC n.k

Ingawaje zamani kulikuwa na timu za mashirika na taasisi zilizoshiriki ligi daraja la kwanza (wakati huo ndio ilikuwa ligi kubwa) na kuleta upinzani haswa mathalani timu kama ya Reli, Sigara na nyinginezo
 
Kwani hizo taasisi zimeanzishwa kwa madhumuni gani? Mpira au kutoa huduma kwa wanachama wake?

Siyo kila kitu ni lazima tuige.
 
Zamani mashirika yalikuwa na timu za michezo karibu yote.
Ndiyo maana tulikuwa na timu kali za Pamba ya Mwanza, Reli ya Morogoro, Tumbaku ya Morogoro, RTC Kagera, RTC Kigoma, CDA Dodoma, Ndovu Arusha, Sigara, Bima, Kilitex Arusha, Urafiki Jazz, Bora Netball, Aluminium Africa Boxing team, Uhamiaji nk.
Hata hivyo baada ya ukaguzi wa hesabu za serikali ikaonekana wapigaji walitumia mwamvuli wa michezo na burudani kupiga hela za mashirika na taasisi za serikali.
 
Uhamiaji na Polisi walikauwa wanatoa wanamasumbwi wazuri sana...
 
Swali ni kwanini wawe na timu za mpira?

Kwanini sio michezo mingine ambayo bado inachechemea?

Kila taasisi unataka iwe na timu? Mapenzi yako ya mpira yanafanya usione zaidi ya mpira.

Unatolea mfano ZA na UG, upo serious kweli mkuu? Soka la hizo nchi limefika wapi kwa mfano? Wachezaji wao wakubwa wanaota kuja kucheza bongo.

Hizo taasisi zijikite kulipa watu mafao kwa wakati na kutoa huduma bora. Sio lazima kila mtu aingine michezoni. Labda wajenge viwanda kama alivyoshauri mwendazake vitaajiri watu wengi zaidi na kukuza uchumi.
Mawazo chanya kama mwamba mmoja wa kuitwa Infantry Soldier
 
Ni fikra mbovu, hazienandani kabisa na wakati uliopo.

Zanzibar mpira umepotea kabisa kutokana na kushamiri kwa timu za vikosi vya jeshi,
 
Back
Top Bottom