Kwanini Sumaye na Mwambe waligombea kwenye Kanda zao na tena wanagombea Uenyekiti Taifa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,193
25,504
Mzee Fredrick T. Sumaye na Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe waligombea Uenyekiti wa Kanda zao za Mashariki na Kusini. Kule Kanda ya Mashariki, Mzee Sumaye akiwa mgombea pekee wa Uenyekiti, alipata kura nyingi za HAPANA na hivyo kushindwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Kanda ya Mashariki.

Mbunge Mwambe naye aligombea Uenyekiti wa Kanda ya Kusini. Akazidiwa kura na Ndugu Mathew katika nafasi hiyo na hivyo kupoteza nafasi yake ya Uenyekiti wa Kanda ya Kusini aliyokuwa akiitetea. Mwambe yeye alizidiwa kura na Mathew kwenye boksi kwakuwa Kanda ya Kusini ilikuwa na mgombea zaidi ya mmoja wa Uenyekiti.

Mzee Sumaye na Mwambe wote walihamia CHADEMA wakitokea CCM. Wote waligombea Uenyekiti wa Kanda zao na ule wa Taifa wa CHADEMA mwaka huu (kabla ya leo Mzee Sumaye kujiweka pembeni kwenye uchaguzi huo na hata CHADEMA kwa ujumla wake). Kwanini waligombea nafasi mbili: kwenye Kanda zao na ile ya kitaifa?

Kwenye siasa kuna kushinda na kushindwa. Kwenye siasa kuna kuzidiana nguvu kiushawishi (wakati mwingine bila hujuma wala vitisho vyovyote). Wao walitaka vyote na sasa wanakosa vyote. Kwa jinsi mambo yalivyo, ni dhahiri Mwambe anakwenda kuzidiwa kura na Mbowe kwenye Uenyekiti CHADEMA Taifa. Naye sijui atakuja na kauli zipi na uamuzi gani.

Muda utatueleza.
 
Kwa nini usiwalalamikie waliotunga kanuni za uchaguzi ndani ya CHADEMA?

Yaani Kanuni za uchaguzi zinawaruhusu kufanya hivyo halafu wakifanya unaanza kuwalalamikia?

Huoni wenye tatizo ni wale waliotunga Kanuni za Uchaguzi ndani ya CHADEMA ndio maana baadhi ya watu ndani ya CHADEMA wamejirundikia vyeo kama vile hakuna wanachama wengine wa kushika nafasi hizo!

Kikubwa zaidi, wao wamesema walitaka kuonyesha umma kuwa ndani ta CHADEMA kuna demokrasia kwa sababu baadhi ya watu walikuwa wanasema nafasi ya Mwenyekiti Taifa niya Mbowe pekee.
 
Petro E. Mselewa,
Mheshimiwa ungetusaidia sana kuonyesha ni kifungu gani cha Katiba au kanuni za Chadema zilizokiukwa ungalikuwa umetusaidia sana, La sivyo na sisi tunzbaki tukishangaa kama wewe kuhusu utaratibu hizi za uchaguzi ndani ya Chadema.

Ati Mwenyekiti (Mgombea) ana nafasi ya kuitisha kikao kuazimia kuteua mtu anayemtaka ajaze fomu kugombea umakamu mwenyekiti.

Inawezekana na nauli atumiwe hadi Nairobi pamoja na kuwa hayupo nchini na hadharani atangazie Wanachama maamuzi yake😃😃
 
Nimemsoma Sumaye anasema alichukua form ya kugombea uenyekiti ili kuonesha CDM ni chama cha kidemokrasia, sasa kama alichukua form kwa lengo la kushindana ili awe mwenyekiti kweli, au alichukua form ili tu kuuonesha umma inawezekana kugombea uenyekiti ndani ya chama ni suala jingine, mimi sijui.

Sasa kaamua kukimbia chama, hata hiyo nafasi ya uenyekiti nayo kaikimbia, kaona kama kule kanda ya pwani alishindwa na kivuli tu, huku kwa taifa kwa Mbowe si ndio litakuwa balaa kabisa!

Huyo mwambe naye naona siku sio nyingi ataitisha press yake, alalamike, then aseme narudi ccm, na hivi juzi katoka kusifiwa na boss lazima akajiunge huko, yaani CDM inawachuja watu scientifically!
 
Mtani, hata mimi nilijiuliza hivyo hivyo...

..nimesoma kwa haraka haraka press release ya Mzee Sumaye.

..nilivyoelewa ni kwamba yeye hakuwa na mpango wa kugombea uenyekiti wa kanda.

..pia suala la uenyekiti wa taifa kwa maelezo yake anasema alijua kabisa kuwa hawezi kushinda, ila alichukua fomu kwa nia ya kuuonyesha umma kuwa ktk cdm kuna uhuru wa kugombea nafasi yoyote ikiwemo Uenyekiti wa chama.

..nini kimemtibua Mzee Sumaye?

..nilivyoelewa ni kwamba kuna watu walienda kumuomba agombee Uenyekiti wa kanda na yeye akawaamini akachukua fomu.

..ilipofika wakati wa kampeni na kupiga kura wajumbe wanaochagua mwenyekiti wa kanda wakawa wanapigiwa simu na kuambiwa wamtose Mzee Sumaye.

..habari kuhusu mikakati hiyo mibaya zikamfikia Mzee Sumaye. Na wakati wa kujieleza kabla kura hazijapigwa aliwaeleza wajumbe kwamba hicho wanachotaka kukifanya, au walichoshawishiwa kukifanya, siyo sahihi wala haki.

..Sasa kura zilipopigwa, matokeo ndiyo kama yale tuliyoyasikia.

..Hivyo ndivyo nilivyoelewa mtafaruku huu uliopelekea Mzee Sumaye kubwaga manyanga.

..Press release ya Mzee Sumaye imeniacha na maswali mengi ambayo naamini tuko wengi tunajiuliza. Natumaini tutapata majibu kadiri muda unavyokwenda.

NB.

..akiwa Arusha Mbowe alieleza kuwa pamoja na yaliyotokea bado CDM inamhitaji na itamtumia Mzee Sumaye.
 
Tundu Lisu anagombea umakamu mwenyekiti wakati anaishi Ulaya, fomu amejaza online, CHADEMA kuna vituko!
Na huku kanuni zinakataza ilo..Maana kanuni zinasema lazma fomu ijazwe mtu akiwa nchini na kuwasilisha kwa mkono.


2020 Wanaccm tuchukue fomu kugombea uwenyekiti Taifa
 
Sumaye na Mwambe ni wahanga wa “safisha safisha”. Hata itakuwa hivo kwa Nyalandu. Waliorejea CCM wengi walikuwa ni wale waliokuwa CCM kwanza. Hili lisisahaulike!!

Chadema wameona kuwa walikosea kuwakaribisha wanachama wa CCM mwaka 2015. Wamekubali kujisahihisha hata kama maana yake ni kuwatendea watu mambo yasiyo ya haki.

Walipaswa kueleza kwanini wanagombea nafasi mbili, je ni tamaa ya madaraka??
 
Back
Top Bottom