Kwanini sukari imekuwa ni kama anasa kwa Tanzania na kwa mwelekeo hapa Serikali imechemka

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,991
1,194
Ndugu zangu wana jukwaa hebu tujadili pamoja jambo hili la Sukari kwa Tanzania na bei yake ambayo sasa ni kero kwa nchi nzima, tulishuhudia Waziri akitangaza bei elekezi lakini cha ajabu bei iko juu palepale kwa maana ya Tshs 3000 na kuendelea.

Sasa tuamini hii ni biashara ya vigogo wenyewe Serikalini ndio maana bei haiwezi kushuka au tuamini kwamba serikali katika hili imeinua mikono na kusurrender.

Maana matangazo ni mengi,tumenunua ndege, sijui tunajenga treni ya mwendo kasi, umeme bwawa la Mwl nyerere, lakini tusipoangalia Hii sukari inayotumiwa na watu masikini itatutia aibu kubwa sana kwa sababu tutafanya mengi lakini hatutagusa maisha ya watu maskini.
 
Tanzania tumeshindwa mtihani mdogo kabisa. Malawi Wana eneo dogo Sana, lakini wanazalisha surplus ya sukari. Sisi 🇹🇿 tuna mabonde mengi makubwa yenye rutuba, lakini ndio hivyo Tena, tunayafugia tu majoka.

Hapa Kuna utetezi wa mwanasiasa mmoja. Sukari Ina wivu, inaona Kila msichana Facebook na JF anajiita Mara sweetie, Mara sugar, ikaona iadimike kidogo, tuone kama mtawaweka hao wasichana wenu kwenye chai
 
Ndugu zangu wana jukwaa hebu tujadili pamoja jambo hili la Sukari kwa Tanzania na bei yake ambayo sasa ni kero kwa nchi nzima,tulishuhudia waziri akitangaza bei elekezi lkn cha ajabu bei iko juu palepale kwa maana ya Tshs 3000 na kuendelea sasa tuamini hii ni biashara ya vigogo wenyewe serikalini ndio maana bei haiwezi kushuka au tuamini kwamba serikali katika hili imeinua mikono na kusurrender,maana matangazo ni mengi,tumenunua ndege,sijui tunajenga treni ya mwendo kasi,umeme bwawa la Mwl nyerere,lkn tusipoangalia Hii sukari inayotumiwa na watu masikini itatutia AIBU KUBWA SANA.kwa sababu tutafanya mengi lkn hatutagusa maisha ya watu maskini.
Kwahiyo sukari ndio maisha ya watu?!
 
Tanzania tumeshindwa mtihani mdogo kabisa. Malawi Wana eneo dogo Sana, lakini wanazalisha surplus ya sukari. Sisi 🇹🇿 tuna mabonde mengi makubwa yenye rutuba, lakini ndio hivyo Tena, tunayafugia tu majoka.

Hapa Kuna utetezi wa mwanasiasa mmoja. Sukari Ina wivu, inaona Kila msichana Facebook na JF anajiita Mara sweetie, Mara sugar, ikaona iadimike kidogo, tuone kama mtawaweka hao wasichana wenu kwenye chai
Sasa hayo mabonde si Mimi na wewe ndio tunatakiwa tukaya shughulikia
 
Kwa hiyo sukari ni maisha? Unalinganisha na mahindi, mchele na maharage? Ni kiasi gani cha watanzania kinatumia sukari kila siku?
 
Kwetu ni bei yenyewe elekezi 2,800/=.Hiyo Dar ni sehemu ndogo tu ya Tz sio Tz yote.
 
Nenda mkuranga Kuna sukar za magendo bei ni chini ya bei elekekez.Pengine usiwaamini sana wanasiasa wa ccm,huwa wanatangazwa halafu wanapotea.
 
Ndugu zangu wana jukwaa hebu tujadili pamoja jambo hili la Sukari kwa Tanzania na bei yake ambayo sasa ni kero kwa nchi nzima, tulishuhudia Waziri akitangaza bei elekezi lakini cha ajabu bei iko juu palepale kwa maana ya Tshs 3000 na kuendelea.

Sasa tuamini hii ni biashara ya vigogo wenyewe Serikalini ndio maana bei haiwezi kushuka au tuamini kwamba serikali katika hili imeinua mikono na kusurrender.

Maana matangazo ni mengi,tumenunua ndege, sijui tunajenga treni ya mwendo kasi, umeme bwawa la Mwl nyerere, lakini tusipoangalia Hii sukari inayotumiwa na watu masikini itatutia aibu kubwa sana kwa sababu tutafanya mengi lakini hatutagusa maisha ya watu maskini.
Mkuu ile bei elekezi ilikuwa uongo ulioelekezwa kwenu mlioozoea kudanganywa.Just imagine wewe ndo ungekuwa na duka then kule unakonunulia hiyo sukari ukauziwa kilo moja sh.2800 wewe ungeenda kuiuza kwa sh 2600? Hata magufuli hawezi
 
Back
Top Bottom