Kwanini suala la makinikia linawauma CHADEMA kuliko ACACIA wenyewe?

Sasa Wapinzani nao wameamua kufanya walichokifanya CCM toka 1998. Totally No SENSE!
Chintu,
Acha kuzuga akili za watu wewe.
Ati Wapinzani wanafanya walichokifanya CCM toka 1998!! Are you serious or insane?
Hoja ya Upinzani bado iko palepale kwamba: MIKATABA YOOTE HII YA MAKINIKIA ILISAINIWA NA CCM(Chama Cha Makinikia). Je, CCM walikuwa wapi?

Magufuli mwenyewe ni sehemu ya uoza huu akiwa Mbunge na Waziri tangu 1995!!! Kwa mana nyingine Magufuli alikuwa akiiingia kwenye Baraza la Mawaziri na Bunge katika kupitisha Mikataba hii mibovu.
Hivo hawa CCM ndio chanzo cha Migogoro yote ya Mikataba ya Uchimbaji Madini na GASI ASILIA Tanzania. Shame on you CCM and your Chairman.
 
Halafu kwa bahati mbaya hawa jamaa wanaolalamikiwa bado tu wanaendelea na uchimbaji wa madini, hii nchi hii
 
Wabongo siyo siri tuna roho mbaya wengi hawakupenda ripoti ya jana walitaka Magufuli ashindwe cha Kuongea, Ndio maana hata jana Mwenyekiti wa Tume Professor Osoro wakati anawasilisha Baadhi ya Vijana wa Chadema walikua wako Busy kukosoa Sauti yake na Wengine Kusingizia kuwa Professor anatatetemeka.

Wakuu nimepitia Comment mbalimbali hasa kwenye topic za Acacia yaani bado waoga sana kile alichotuaminisha Tundu Lissu Bado yapo Kichwani majitu maoga sana

Mi nimeona makaratasi yenye Mihuri humu eti Ushahidi hata Jamii Forums wameweka katika trends kama Ushahidi. Mmeshambiwa BRELA hakuna Acacia bado tunawaamini mabwenyeye wa Kizungu Tubadilike.

Suala lililobaki ni Kuipelekea acacia Invoice ya Sh. 108Trillion kama Kodi yetu.
Kule mwanzoni uliwatetea sana ACASIA.
Ulisikitika kitendo cha kuzuia mchanga wao usisafirishwe nje.
Na kusema kwamba kitendo hicho kunawasababishia hasara ya dola bilioni moja kwa siku.
Asante kwa kujitambua na kuwa mzalendo sasa.

Mr. Troll JF
 
Pamoja na makosa ya kusaini mikataba mibovu, ACACIA imejipiga rusasi miguuni. Hakuna mkataba una ruhusa kuvunja sheria kama ya wizi wa kudeclare uxito wa containa na Mali iliyopi kwenye container. Hiyo sio puma ni breach of contract, ukibreach contract huo unakuwa sio mkataba tena. Ndiyo maana Acacia wanasema wako tayari kwa mazungumuzo.
Acacia wamefanya makosa,makosa zaidi yamefanywa zaidi na watanzia wenzetu.
Kama una akili timamu unampaje mtu liseni ya uchimbaji na kila utakachokuta kwenye kitalu chake ni Mali yake?upumbavu uliopitiliza!
Hao wasomi walifanya nini? Ujinga tu!kama ndo ningekuwa presida sijui angebaki nani?
 
Huu ni upuuzi kuingiza siasa kwa jambo kama hili. Hawa watuhumiwa ni watu binafsi, waliyoyafnya waliyafanya sio kwa manufaa ya nchi wala CCM. Waliyafanya kwa manufaa yao wenyewe. Acheni siasa za kijinga kwenye jambo hili, tunaonekana wote wajinga.

Wote hawa ni Wana-CCM(Chama Cha Makinikia) hivo walikuwa wakifanya kwa MANUFAA YA CCM na BINAFSI ZAO. Kama tukianza kufukunyua fedha zilizopotea au kutolewa kama Rushwa utakuta FEDHA NYINGI ZIMETUMIKA KWENYE KAMPENI NA CHAGUZI ZA CCM. Huo ni ukweli mchungu ambao lazima CCM waumeze watake wasitake.
 
Wabongo siyo siri tuna roho mbaya wengi hawakupenda ripoti ya jana walitaka Magufuli ashindwe cha Kuongea, Ndio maana hata jana Mwenyekiti wa Tume Professor Osoro wakati anawasilisha Baadhi ya Vijana wa Chadema walikua wako Busy kukosoa Sauti yake na Wengine Kusingizia kuwa Professor anatatetemeka.

Wakuu nimepitia Comment mbalimbali hasa kwenye topic za Acacia yaani bado waoga sana kile alichotuaminisha Tundu Lissu Bado yapo Kichwani majitu maoga sana

Mi nimeona makaratasi yenye Mihuri humu eti Ushahidi hata Jamii Forums wameweka katika trends kama Ushahidi. Mmeshambiwa BRELA hakuna Acacia bado tunawaamini mabwenyeye wa Kizungu Tubadilike.

Suala lililobaki ni Kuipelekea acacia Invoice ya Sh. 108Trillion kama Kodi yetu.
Mtahangaika sana KUPOTOSHA ili kujisafisha. Ni nyie ndie mlioleta sheria mbofu mbofu za madini kwa nderemo. Hansard zipo. Ndo maana hata Mkullu ambae nae alikuwemo bungeni alikuwa mpole. Watu wenu walioharibu kwenye mikataba wapo peupe kabisa. WATZ watajuzwa vizuri hata mkiendelea kuzuia mikutano ya Wapinzani.
 
Na mwenye mamlaka ya kuondoa kinga ni huyohuyo anayesifiwa kama Mzalendo. Nina hakika kinga hiyo hawezi kuiondoa kwa sababu ni "mbinafsi" anawaza kuhusu yeye mwenyewe atakapo toka atajikuta na wakati mgumu. Mama Obama tunapigwa tuu change la macho hapa. Kwa nini Katiba mpya haitaki na ndiyo yenye majibu ya matatizo yote haya?

Katiba mpya inaweza kuwa jawabu na isiwe, ingawaje naunga mkono wa katiba mpya likiwa pamoja na Rais aondolewe kinga. Katiba mpya itakuwa na faida kama itafuwatwa na kuheshimiwa. Jirani zetu Kenya wana Katiba nzuri sana, leo ingekuwa inafuatwa 90% wanaoiongiza Kenya wasingeweza kuwa Viongozi kufuatana na kifungu namba 6 (leadership integrity). Ikiwa pamoja na Rais na msaidizi wake. Tanzania ndiyo itakuwa zaidi, kwa tabia zetu za undugu wa kuchungana na kuvumuliana huku wengine wanaumia bila ya Kujali. Hata hivyo namvulia kofia Rais Magufuli, kufanya anayoyafanya amejaribu. Hata kama upinzani ungechukuwa serikali, Rais angekuwa ni Lowassa, Lowassa alipokuwa CCM aliipinga Katiba mpya, na Sasa yuko upinzani amebadilika. Shida yetu wanasiasa wetu hawako kwenye siasa kwa principal zao, siasa kwao ni njia ya kutajirika bila ya kufanya kazi , Ndiyo maana tumefikishwa hapa tulipo. So far Watanzania hawana alternative, sioni kwenye upinzani kuna yeyote anaweza. Ndiyo wengi wamesema, lakini kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti.
 
Acacia wamefanya makosa,makosa zaidi yamefanywa zaidi na watanzia wenzetu.
Kama una akili timamu unampaje mtu liseni ya uchimbaji na kila utakachokuta kwenye kitalu chake ni Mali yake?upumbavu uliopitiliza!
Hao wasomi walifanya nini? Ujinga tu!kama ndo ningekuwa presida sijui angebaki nani?

Nakubaliana na wewe. Ni uongozi mbaya, sio tu mawaziri, ni kutoka Ikulu. Kama baba hajali familia yake, basi matokeo yake ni haya.
 
Waliyafanya kwa manufaa ya ccm.

Huu ni ubishi wa kijinga. Waliohusika walitafuna hata Mali ya CCM. Tanzania nzima ilikuwa na uongozi wa ajabu. . Hata kama upinzani ukishinda kwanza ingekuwa balaa. Anayoyafanya Rais Magufuli Lowassa asingeyafanya, ni mtu mwenye kupenda Utajiri, wengemunyamazisha na pesa za muchanga na wala asingeyakamata macontainer. Angalia baada ya watu kutoka upinzani ulivyokuwa wakioinga kukamatwa kwa muchanga Huu..
 
ccm ni ile ile oooohhh ni ile ileee oooohhhhh!!
tumejipangaaa,mwaka huu mtaisomaaa x2

Mumejipanga, ni nani kuwa Rais wetu. Mimi sioni kwenye upinzani. nilifikilia Tundu `Lissu, kwa hili la muchanga limemuangusha, hana la kusema tena. Watanzania hawatamuamini. So far our alternative ni Rais Magufuli, ndiye ameonyesha ujasiri hata wa kusimamama kwa hawa makaburu Wakati wote waliopita walikuwa wakinunuliwa kwa bei ya kutupa,.
 
Huu ni upuuzi kuingiza siasa kwa jambo kama hili. Hawa watuhumiwa ni watu binafsi, waliyoyafnya waliyafanya sio kwa manufaa ya nchi wala CCM. Waliyafanya kwa manufaa yao wenyewe. Acheni siasa za kijinga kwenye jambo hili, tunaonekana wote wajinga.
Waliyafanya hayo kwa manufaa ya CCM na kwa baraka za chama usituletee utetezi wako usio na kichwa wala miguu
 
Mbona mnawapaka watu rangi moja? CCM ! CCM, kwa sasa acheni siasa, ni Watanzania wote wameibiwa, .
Mimi sizungumzii walioibiwa, bali walioiba. Nafahamu kuwa walioibiwa ni Watanzania, ila pia lazima iwekwe wazi kuwa walioiba wote ni CCM
 
Huu ni ubishi wa kijinga. Waliohusika walitafuna hata Mali ya CCM. Tanzania nzima ilikuwa na uongozi wa ajabu. . Hata kama upinzani ukishinda kwanza ingekuwa balaa. Anayoyafanya Rais Magufuli Lowassa asingeyafanya, ni mtu mwenye kupenda Utajiri, wengemunyamazisha na pesa za muchanga na wala asingeyakamata macontainer. Angalia baada ya watu kutoka upinzani ulivyokuwa wakioinga kukamatwa kwa muchanga Huu..
Wewe sasa ndio umeingia ulipokuwa unataka kusema na katika utetezi wako wote lengo lako ni lowasa sasa umejuaje kama lowasa angeshindwa kufanya
 
Back
Top Bottom