Kwanini Spika Ndugai anawapigia upatu Wachina bandari ya Bagamoyo? Achunguzwe kama hana akaunti ya Benki nje

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,596
8,738
Mimi nina wasiwasi wa huyu Spika wetu na China. China wamekuwa wakinunua viongozi wa Africa kwa manufaa yao.

Leo hii baada ya Rais Magufuli kufariki huyu spika sasa anataka kumburuza Rais Mama Samia kwenye mtataba wa kuuza bandari ya Bagamoyo kwa China.

Lengo la China liko wazi na walishasema wanahitaji sehemu kama walivyofanya kwenye nchi nyingine kuwa na biashara na base ya kijeshi. Hii ndiyo sababu wanataka kupewa kwa miaka 99.

Sehemu iwe kama balozi eti huwezi kuingia na wanaweza kufanya lolote.

Sasa wamemweka spika mfukoni na watampa kila kitu ili Bunge limweke mama sehemu mbaya.

Tanzania bado tunatafuta pesa ya kujenga reli, kununua mabehewa, kujenga barabara, ni kwanini tuongie mzigo wa kuuza nchi hivi tena bure.

Mimi nina wahakikishia Spika tayari atakuwa na bank account nchi za nje kama sio yeye ni mke wake au watoto na kama hana aseme wazi na kama anayo yeye au ndugu aseme ina kiasi gani.

Watanzania tuwe makini na tuhakikishe Mama Samia hakubali hizi mbinu mbaya za Spika na wabunge wa Bagamoyo.
 
Mbowe ni mnafiki na wakala wa wazungu anatafuta huruma ya mama Samia ili dili lake alilokula 10% kwa kuleta chanjo Tanzania.

Kwa nini hakuyasema kipindi Magufuli yupo?
 
Mbona ameeleza vizuri tu hebu rejea alichokisema leo

Uwekezaji wa Bagamoyo tunauhitaji lakini sio lazima awe Mchina

Kikubwa tuangalie mkataba wenye maslahi tujenge bandari
 
Nini kinamfanya autetee kwa nguvu zote huu mradi

Naunga hoja mkono

Ila nani wa kumfunga paka kengele?
 
Nini kinamfanya autetee kwa nguvu zote huu mradi,

Naunga hoja mkono,

Ila nani wa kumfunga paka kengele??
Kivipi mkuu
Hebu niwaombe Watanzania tuwaamini viongozi wetu. Tunawahisi hizi mno kiasi kwamba mpaka tunawavunjia heshima. Usikute jamaa anao uzalendo wa kweli kabisa na nia njema lakini basi tu watu wanamavisa yao na machuki yao unakuta kila wakati wanamhisi hizi vibaya kiongozi wao
Tuwaamini
Tuwaombee
Nena mema kwa ajili yao Mungu ana nafasi yake kwenye hayo
 
Kwahiyo unataka tukae kama mazezeta bila kuuliza chochote hata kama kuna kila kiashiria cha kuleta mashaka,

Hapana, lazima tuulize,

Nyerere anatutaka vijana kuweka uzalendo mbele kwa kuto kaa kimya Lazima tuulize, hatuta nyamaza.
 
Hujauliza ila umemtuhumu. Hebu soma ulichokiandika
 
Kwahiyo unataka tukae kama mazezeta bila kuuliza chochote hata kama kuna kila kiashiria cha kuleta mashaka,

Hapana, lazima tuulize,

Nyerere anatutaka vijana kuweka uzalendo mbele kwa kuto kaa kimya Lazima tuulize, hatuta nyamaza.
Mkuu siku hizi uzalendo hakuna kila mtu yuko kimslahi

Huo ndiyo ukweli

Ova
 
Mbowe ni mnafiki na wakala wa wazungu anatafuta huruma ya mama Samia ili dili lake alilokula 10% kwa kuleta chanjo Tanzania.

Kwa nini hakuyasema kipindi Magufuli yupo?
Kutekana, kutesa, kuua, kubambika kesi ulikuwa ni ushamba wa SHUJAA kunyamazisha watu.
 
Kivipi mkuu
Hebu niwaombe Watanzania tuwaamini viongozi wetu. Tunawahisi hizi mno kiasi kwamba mpaka tunawavunjia heshima. Usikute jamaa anao uzalendo wa kweli kabisa na nia njema lakini basi tu watu wanamavisa yao na machuki yao unakuta kila wakati wanamhisi hizi vibaya kiongozi wao
Tuwaamini
Tuwaombee
Nena mema kwa ajili yao Mungu ana nafasi yake kwenye hayo

Hakuna wa kuaminiwa hata kama mmoja wao ni baba yako! Hata mimi kama ni miongoni mwao usijaribu kuniamini, wa kuamini ni wewe mwenyewe tu! Jiamini wewe peke na simama wewe kama wewe, wengine ni vichocheo tu!
 
Back
Top Bottom