Kwanini spika anazima hoja ya kujadili mgogoro wa Madaktari?

Asiwe mkali kwa nini? Unategemea akiugua yeye atatibiwa hapa? India itakuwa imepotea kwenye ramani ya dunia?
 
labda nikuulize wewe Black Rose kama mwanamke

wakati anateuliwa u spika wengi tuliona hafai na ni makosa kumzuia Sitta kugombea

lakini wanawake weengi mliona 'anafaa' ni sahihi kuteuliwa kuwa spika.....

je wewe hukuliona hilo toka mwanzo?
 
Ishu ya madokta ina usiri gani?
Mh Erasto ZAMBI akataka swala hili nyeti lijadiliwe.Spika kakataa na kawa mkali kama Mbogo

Haiwahusu wabunge .... hata wakijadili kasungura kamekua kadogo?
 
404284_342205012469229_100000391994771_1103093_1884948629_n.jpg
 
Wanatamani Babu angeibuka kipindi hiki,
pale nasikia wana kitu kinaitwa mpango mkakakati wa kuwapeleka waganga wote wenye leseni,
 
kama imeundwa kamati, ya nn kujadili?,, au wale jamaa wasiokuwa na sera wanataka kupata mahala pa kusemea?,,acheni kamati ifanye kazi yake itakuja na majibu pamoja na mapendekezo.
 
Ishu ya madokta ina usiri gani?
Mh Erasto ZAMBI akataka swala hili nyeti lijadiliwe.Spika kakataa na kawa mkali kama Mbogo

Wabunge wa CCM wanafiki.
Mara baada ya Zambi kuwasilisha Hoja walisimama kuunga mkono hija ijadiliwe bungeni.
Spika akakataaa.
Wabunge haohao, waligoma kuunga mkono hoja hiyohiyo bungeni siku ya ijumaa kisa imetolewa na wabunge wa Upinzani.
 
wabunge wa ccm wanafiki.
Mara baada ya zambi kuwasilisha hoja walisimama kuunga mkono hija ijadiliwe bungeni.
Spika akakataaa.
Wabunge haohao, waligoma kuunga mkono hoja hiyohiyo bungeni siku ya ijumaa kisa imetolewa na wabunge wa upinzani.

wabunge wa ccm wamekwisha kazi.
 
Labda wanaogopa mijadala itafika mbali na hata kuibua mijadala mingine kama walimu, na wafanyakaz wengine na changamoto zao.
 
kama imeundwa kamati, ya nn kujadili?,, au wale jamaa wasiokuwa na sera wanataka kupata mahala pa kusemea?,,acheni kamati ifanye kazi yake itakuja na majibu pamoja na mapendekezo.
kamati ilipewa kushughulikia mgomo wa interns,registrars na residents.lakini jana tumesikia speacilists wamegoma ikiwa inamaanisha ni jambo jipya na liko nje ya hadidu za rejea za kamati ile .sasa kwa nini lisijadiliwe ?tukubali tukatae makinda katoa mpya na kaonyesha kwamba amewekwa pale na serikali.sioni kama mbunge anaweza kujadili hoja ya gesi kwa amani moyoni huku akisikia vilio vya kina mama na watoto toka pale muhimbili.tutafakari tuache ushabiki.
 
labda nikuulize wewe Black Rose kama mwanamke

wakati anateuliwa u spika wengi tuliona hafai na ni makosa kumzuia Sitta kugombea

lakini wanawake weengi mliona 'anafaa' ni sahihi kuteuliwa kuwa spika.....

je wewe hukuliona hilo toka mwanzo?
sasa unaenda nje ya mada...kama hafai ni yeye binafsi na weakness zake..lakn yakija mambo ya wanawake hapa utakuwa unakosea...
 
sasa unaenda nje ya mada...kama hafai ni yeye binafsi na weakness zake..lakn yakija mambo ya wanawake hapa utakuwa unakosea...

kivipi nje ya mada?
mtu hafai na aliwekwa hapo kwa hoja kuwa ni mwanamke
na nyinyi mliuunga mkono kwa sababu ni mwanamke
hamkutaka hata kusikiliza hoja za kwa nini hafai..
now anafanya madudu....mnauliza why?????....

ni sawa na uambiwe dereva hafai na wewe ushikilie kumpa gari..
halafu akisababisha ajali unakuja juu kuuliza why???
 
Jamani, bunge hilo hilo ndio limeunda kamati, sasa bunge hilihilo lijadili kabla kamati haijaleta uchunguzi wake?
 
Jamani, bunge hilo hilo ndio limeunda kamati, sasa bunge hilihilo lijadili kabla kamati haijaleta uchunguzi wake?
mgomo wa madaktari bingwa ni kitu kipya,kamati ya kudumu ya huduma za jamii sio kamati maalumu ya kushughulikia mgomo hivyo haina meno.msiwafanye watu ni wajinga katika zama hizi.
 
mgomo wa madaktari bingwa ni kitu kipya,kamati ya kudumu ya huduma za jamii sio kamati maalumu ya kushughulikia mgomo hivyo haina meno.msiwafanye watu ni wajinga katika zama hizi.

Kumbuka kuwa Tanzania inaendeshwa kisheria na wabunge ndio watunga sheria. Sheria haziruhusu daktari kugoma, Daktari anaegoma ni kama mwanajeshi anaesaliti wenzake (traitor), hukumu yake ni kifo tu.
 
Kumbuka kuwa Tanzania inaendeshwa kisheria na wabunge ndio watunga sheria. Sheria haziruhusu daktari kugoma, Daktari anaegoma ni kama mwanajeshi anaesaliti wenzake (traitor), hukumu yake ni kifo tu.
kinachonitatiza ni kimoja tu!kwa nini serikali haifanyi maamuzi?kama kuwahukumu madaktari kifo basi ifanye hivyo sasa au kama ni kutekeleza mahitaji yao na iwe hivyo sasa na sio na kuendelea na danadana wakati watu wanateseka.
 
Back
Top Bottom