Kwanini spika anaijibia serikali..?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini spika anaijibia serikali..??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MtazamoWangu, Jul 2, 2009.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Waungwana leo kwenye kipindi cha maswali kwa PM bungeni sikufurahishwa na kitendo cha Spika kila wakati kuingilia kati maswali ya wabunge kwa PM, suala la wizi wa nyaraka ZNZ na chanzo cha kujiuzuru Jumbe na suala la mahakama ya kazi na ahadi za CCM, siulizi majibu yake ambayo mara zote hayana tija, bali nauliza:
  1. Je kati ya spika na waziri mkuu (PM) nani anayeisemea serikali??
  2. anaposimama PM bungeni nini nafasi ya spika???
  3. Je spika ni muongeaji wa chama, CCM, bungeni??? ana haki ya kukitetea chama chake??
  4. Spika anapojibu swali aliloulizwa waziri mkuu, anafanya vile kwa nafasi gani?? je majibu yake ndio msimamo wa serikali??

  hili limekuwa linatokea sana sio kwa PM tu bali hata kwa mawaziri wengine, mimi naona Spika aiche serikali ijibu yale wananchi wanayowatuma wabunge wao wakaulize wajibu wenyewe, watupe tu majibu ya "hovyohovyo" ili tujue hiyo ndio serikali yetu.
  bado najifunza kanuni za bunge ili tukapambane vizuri lakini pia swala la Spika kuzuia waziri asijibu swali la mbunge ni kukandamiza haki ya kujieleza, na kazi za bunge...serikali lazima iulizwe na itoe maelezo ya kutosha kwa wananchi wake.

  kama serikali haitaki kujibu au hawana majibu wanaweza wakatoa maelezo yakujitosheleza sio Spika kutumia nafasi yako kuwazima wabunge kuwakilisha hoja za wanaowawakilisha....
   
 2. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  inategeana na swali lenyewe na kanuni zinasemaje. hata mimi nilisikiliza leo asubuhi lakini sidhani kama alaumiwe spika, hata wale wabunge hawakuwa na maswali mazuli. mengi utaona yanarudiwa, (mf. kuhuzu malipo ya wapemba, limerudiwa) au swali lenye jibu linaloeleweka (mf. nchi ina dini gani? spika alimwambia aangalie kwenye katiba) nk mimi nafikiri Spika yupo sahihi ili wabunge waweze kuuliza maswali yenye mantiki kuliko kupoteza muda na story za kusikiasikia
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huyo ndiye Supika Six AKA mzee wa supidi AKA mzee wa misifa ... sidhani kama anajua mipaka ya kazi yake
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Spika SITTA anasimama kwa niaba ya Chama chake cha CCM na watu waliompa uspika
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni jukumu la spika kusimamia mijadala bungeni kama mbunge anauliza swali siivyo ndivyo au mahala sio pake spika humuelimisha kufanya hivyo si kuijibia serkali ni wajibu wake
   
Loading...