Kwanini skari Usalama barabarani wanajificha kwenye vichaka?

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Katika barabara zote kuu (Highways) kumekuwa na juhudi kubwa za kuzuia ajali barabarani zitokanazo na ukiukwaji wa taratibu zilizowekwa. Nadhani ni jambo la busara zaidi katika kuzuia ajali kuliko kusubiri ajali zitokee ndipo askari wachukue hatua.

Jambo kubwa na baya la kushangaza askari wengi wanaosimama katika barabara kuu hizo maarufu kama TOCHI hujificha katika vichaka na kuvizia gari ziendazo mwendo wa kasi kuliko mwendo unaotakiwa katika eneo husika. Swali la msingi ni kuwa lengo la askari hawa ni kukamata au kuzuia ajali? Ni vyema basi askari hawa wakasimama hadharani ili kujenga utamaduni kwa madereva wa kuheshimu taratibu kuliko kuvizia kukamata.

Itakuwaje kama askari watajificha na tochi katika kichaka halafu akang'atwa na nyoka?

si hivyo tu, bali hali hii inatia shaka kuwa vitendo hivi vinaashiria upatikanaji wa masilahi haramu (rushwa) katika zoezi hili na kendelea kuchafua Jeshi la Polisi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom