Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 580
- Wananipenda wakati nikiwa mzima nikiugua kidogo huanza kutoweka.
- Wananipendea uzuri wa sura na sauti yangu hawajui naweza kupata ajali nikapoteza reception hiyo na sauti ikawa ya kukoroma.
- Wanaangalia bambataa langu hawajui mwenyewe naona kero kwa kugeukiwa kila mara (wataweza kuvumilia nikitembea nao barabarani nikiangaliwa na wenzao?)
- Wanapenda waonje bila harusi, hawajui kuwa sina muda mchafu huo tena.
- Wanakuja kwa gia ya kudai bila mimi maisha hayaendi japo nimekutana nao wakiwa wanaishi vema tu.
- Wanadai mi mpole na mkarimu nafaa kuwa mke lakini wanasahau kuwa hivyo si vigezo vya mke bora.
- Wanadai niko mchangamfu na mwenye kuwa na haiba bila kujiuliza kama nikiwa nao watakubali kusikia wenzao wakinisifia hivi.
- Hawako wakweli, hata kama waliwahi kutembea na 'wenzangu' zaidi ya 20 wataniambia mimi ndiye wa tatu hiviiii
- Wanadai mimi ni msomi na naenda na wakati wakati si kipimo cha mapenzi katika ndoa.
- Wananipa ahadi kibao hata zisizoweza kutimilika kwa akili ya kibinadamu ili mradi niwaone bab kubwa.
- Wanadai wananipenda sana na nikiwambia nimeathirika wengi husahau hata kuniuliza nini kimeniathiri.
- Wengi wa habari, kila nikiwa nao naona wanageuka pindi 'wenzangu' wanapopishana nasi.
Sijui kina nani hawa? Wewe mmojawapo? Basi hunifai pia