Kwanini sitaupigia kura Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti wala Hifadhi ya Ngorongoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini sitaupigia kura Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti wala Hifadhi ya Ngorongoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CHASHA FARMING, Sep 22, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280

  Wakuu mimi sitapiga kura kwa ajili ya Kutafuta Kivutio cha Tanzania Kitakacho Ingia Kwenye Maaajabu saba ya Bara La Africa kwa sababu zifuatazo,

  1. Hifadhi za Taifa na Vivutio vingine havijawahi kunufaisha Watanzania

  2. Watakao Nufaika na Hizo Kura ni Viongozi wa Ngazi za Juu pamoja na Wazungu, Ndo maana wazungu wako mbele sana kwenye kuhamasisha,

  3. Hii kampeni ni neema kwa Wazungu na si Watanzania, sisi tutabakia kwenda kuomba vibalua tu kwao

  4. Hoteli zote zilizo Jengwa kwenye Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro zinamilikiwa wa wageni kwa asilimia 100, hakuna mzawa mmoja mwenye hoteli huko hata Camp tu,

  5. Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na Zinginezo wanawathamini sana Watalii wa Kizungu na si Watanzania, watalii wa kitanzania huwa hawapewi umuhimu wowote ule katika hizo hifadhi, na Kuna Kipindi Hifadhi ya Ngorongori iliwahi kujenga Vyoo kwa ajili ya Wazungu na vingine kwa ajili ya Watu weusi/wabongo,

  Na hadi leo hii Abilia wabongo wanaosafiri kwa Mabasi kwenda Musoma huwa wakifika Geti la Ngorongo hawaruhusiwi kutumia vyoo vya wageni bali kuna vya kwao viko Geti No 1 ukiwa unatokea Karatu kuingia Hifadhini

  - Wakuu Sekta ya Utalii hapa Tanzania Inaongozwa na Wazungu Kutoka Ulaya, Marekani, South Africa na Wahindi, na watanzania ni wachache sana kwenye hii secta na wengi ni wafanya kazi tu na si wamiliki wa Makampuni ya utalii,

  -Mlima Kilimanjaro- Huu Mlima wanao nufaika nao ni Makampuni ya Kitalii ya Wazungu yenye Makao makuu yao Mjini Arusha na Moshi, na asilimia zaidi ya 98 ya Makampuni ya Kitalii kanda ya Kasikazini yanamilikiwa na wazungu na ni asilimia kama 2 tu ndo inayo milikiwa na Wabongo na hata hivyo kampuni za wabongo ni Ndogo sana Kiuwezo ikilinganisha na Za wazungu

  Makampuni mengi ya Kitalii yana Offisi huko kwao Ulaya na Marekani na Booking zote na Payment hufanyika huko huko Ulaya na Marekani huku wageni huja kupanda Mlima tu na mara nyingi na pesa za kununulia Vinyago na kuwapa Tips Madreva wanao waendesha, sasa je TRA inawezaje kukagua mapato ya hawa watu wakati acaunt ziko Ulaya na Marekani? na Malipo yanafanyika hukohuko Ulaya?

  JE HAPO ANAYE NUFAIKA NI NANI?

  2. HIFADHI YA SERENGETI
  Hii nayo ni Hifadhi ya Taifa kwa Jina tu ila kimatendo wanao iongoza ni Wazungu kutoka Ulaya wa
  Frankfurt Zoological society, hawa ndo wana usemi wa mwisho kuhusu hizi hifadhi na si Serengeti pekee bali hata Ngorongoro, wakiongea hakuna wakupinga kitu na Maranyingi wamekuwa wanakuja na Policy za kuwakandamizaWatanzania na kuwaona wanyama ndo wana haki pekee na si watanzania

  3. Ngorongoro- hii nayo ni jina tu kwamba ni Hifadhi ya Taifa ila kimatendo hii hifadhi ni kama Limited Company,

  Kwa kifupi wanaonufaika na Hifadhi na Vivutio vingine ni Wazungu na Watanzania Wachache wanao Torosha Wanyama kwenda Nje ya Nchi, Wananchi wengine tumebakia Mashabiki wa kuhamasishwa kupiga kura tu,

  Ni iliaumu sana Serikali kwa kuto kuwezesha Watanzania wazawa Kumiliki Makampuni na Badala yake Makampuni yanamilikiwa na Wazungu, na wazawa wamebakia kuwa Vibarua
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa makampuni yote ya Utalii arusha yanamilikiwa na wazungu na watanzania tumebakia kuwa madreva tu na wabeba mizigo ya wazungu
   
 3. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  siku hitaji kuisoma makala yako yote naunga mkono hoja huu utakuwa ni ujinga mkubwa kura za nini? hata usipokuwa ajabu kuna ajabu gani? na ukiwa ajabu kuna maajabu gani tutatayo yaona kama sio kupoteza wakati tu ni vile hatuna cha kukifanya
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Na mimi sipigiiiiiii.
  Hivi ajabu siku hizi mpaka lipigiwe kura?
   
 5. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mura chacha, umesema vema na umejitahidi kutooa vizuri sababu zako ingawa nyingine ni za kijumla zaidi.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu za kiujuma ni zipi hizo? Mimi nilicho jaribu kueleza ndo ninacho kifahamu, Hifadhi za Tiafa zilisha uzwa ila kimawazo bado ni hifadhi zetu lakini kwa Matendo zainawenyewe wanao faidika na hizo hifadhi
   
 7. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mi sina hata habari na hivyo vitu
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuvipigia kura ivyo vivutio ni sawa na kulipa kodi Tz while beneficially wakubwa wa iyo kodi ni wakubwa
  Nikipataga mwanya wa kutolipa kodi huwa silipi bse ndo posho v8 za wakubwa ndo naifadhili safari za jk nalipa wauaji wa watz ie polisi
   
 9. N

  Njaare JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu nakuunga mkono asilimia mia moja. Nimeangalia maeneo mengi ambapo rasilimali zimegundulika. Badala ya kuwa faraja kwa jamii inayozunguka eneo hilo sasa imekuwa ni adha. Kitendo cha Mlima kilimanjaro kwa mfano ukitangazwa ni ajabu la saba la dunia, kwa uzoefu wa hapa Tanzania, wananchi wanaoishi kuzunguka mlima watahamishwa kwa nguvu kupisha wawekezaji na bila fidia. Angalia watu wanaoishi maeneo yenye madini na mbuga jinsi wanavyofanyiwa. SIUNGI MKONO MAENEO HAYA KUPANDISHWA HADHI.
   
 10. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sitapga kura
   
 11. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  "CHADEMA"watakua wanahusika!
   
 12. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,470
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180

  Maji yanayo miminika kutoka milima Kilimanjaro kupitia mito kadhaa sasa hakuna tena, mito mingi imekauka. Kisa cha kukauka mito hii na mifereji ni wazungu wanaoitwa wawekezaji katika mashamba makubwa ya kahawa, hutumia maji hayo kumwagilia mashamba ya kahawa.

  Katika mito ile, uoto asili umepotea.......mito na mifereji iliokuwa inatiririsha maji hakuna tena......wanyama kama kima waliokuwa wanaishi juu ya miti kando ya mito wanapotea......kima hao huingia majumbani kwa watu kutafuta chakula matokeo yake wengi huishia kuuwawa.

  Kibanga Msese
   
 13. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ila mtihani wa vyoo tulifeli vibaya sana !
   
 14. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  mie nitamshukuru ALLAH SWT, kwa kuweka wazi ishara zake kwa watu wenye akili !
   
 15. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli kabisa, Na hakuna hata Mtanzania wa Chini atakaye nufaika na haya maajabu, Wazungu ndo watakao nufaika, na ndo maana wako mstari wa mbele kwenye kuhamasisha.
   
 16. P

  Paul S.S Verified User

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu hoja yako na wote walioiunga mkono ya kutokuupigia kura haina mashiko hata kidogo maana inaonyesha dhahiri umefikiria hatua moja mbele, naamini ungetulia kidogo na kufikiri miaka hata mitano mbele basi ungekuwa wakwanza kuupigia na kushawishi wengine waupigie kura pia....................kwani unadhani CCM watatawala milele?

  Timiza wajibu wako kama mzalendo wa nchi hii maana kesho na keshokutwa wajibu wako utawasidia CUF au CDM au TLP au yeyote atakaye shika dola kuja kufaidi na matunda ya uzalendo wako
   
 17. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Badilisha I'd yako kwanza,unanilazimisha nikuchukie japo umeongea p point.
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,883
  Trophy Points: 280
  Kitu cha ajabu ni cha ajabu tu hakina sababu ya kupigiwa kura.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. Root

  Root JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,301
  Likes Received: 13,009
  Trophy Points: 280
  kwani tukivunja nao mkataba na ikaanzishwa taasisi ya hifadhi tanzania hatuwezi kutoka kama nchi?
   
 20. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Nashangaa dunia inatafuta vivutio vya kuingiza kwenye maajabu ya ulimwengu ilihali sisi wote Watanzania inatakiwa tuwekwe bila kupigiwa kura kwenye maajabu saba ya bara la Africa hata ya dunia tumeshakwishaqualify
   
Loading...