Kwanini sisi Waafrika (Tanzania) ukweli huu tunaukwepa?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,785
Tunapenda sana kujilinganisha na wengine, na kutwa kusema kwa nini hatuko kama USA, EU au sijui Uchina na Ujapani, lkn kuna jambo moja huwa hatutaki kulikubali na huwa tunalificha chini ya kapeti kwenye kuliganisha kwetu, na ukiniuliza mimi sisi tuko unfair sana kwetu sisi wenyewe, nalo ni hili nitatoa mfano, Columbia University (USA) kilianzishwa mwaka 1750 vs University of Dar es Salaam (TZ yetu) kilianzishwa mwaka 1970!

Sasa linganisha na hapo ujue USA inaitwa ni New World hivyo sijataka kuongelea old world ya EU, ina maana graduate wa kwanza Colombia alitoka kwenye mwaka 1770 huko graduate wa kwanza TZ labda kwenye miaka 50' kama ukichukulia waliosomea Makerere, Nairobi & Co.

Martin Luther aliandika PhD thesis iliyojulikana kama 95 thesis iliyoibadilisha Dunia mwaka 1517, alipata PhD University huko Ujerumani mwaka 1512, linganisha na sisi!

Hamuoni kwamba mnafanya maisha yenu yawe magumu bila ya sababu kwa kulinganisha visivyolingana? Kama ni demokrasia TZ tumeanza hata kulijua hilo neno miaka ya 80' tena mwishoni wakati USA tangu 1700' huko wanajadiliana demokrasia, hivyo fanyeni lililo muhimu na lililo ndani ya uwezo wenu kwa sasa hayo mambo ya kutaka kuwa kama USA au sijui EU mtachanika msamba, USA ina miaka zaidi ya 300 wakati Tanzania chini ya 60!

Kwanza hata hao Afrika ya Kaskazini tu (Moroko, Aljeria, Tunisia &Co.) wametuzidi hata miaka 50 kwenye kila kitu kama human development, lkn unakuta mtu anasimama anaongelea USA, kuweni realistic acheni kujidanganya hakuna miujiza, ...
 
Tujifananishe kwa vinavyofanana,visivyofanana tuendelee kuviboresha ili vije kufanana(vyenye manufaa tu) hebu sasa tuanzie pale tulipowakutia! Miaka hiyo ya 1750 wao walishakuwa na university ila hawakuwa na ndege(aeroplane) sisi pia hatukuwaza kuwa nayo ila leo wao wana miaka 300 sisi tuna miaka 56 na wote tunamiliki ndege,wao waliiasisi demokrasia,sisi leo tuna uwezo wa kuiishi demokrasia,

kama wao ndiyo waliogundua Nguo miaka hiyo ambayo sisi tulikuwa tunavaa majani ila leo hata sisi tunaweza kutengeneza zetu na tukawauzia hata wao,wao walipogundua umeme sisi hatukua hata na wazo hilo,ila leo tuna umeme wetu! Vitu ambavyo hatuna na wao wanavyo leo ni vichache tu!

Ama sisi tunavyo kwa uchache, hivyo wakati wewe unawashangaa watanzania wanaoifananisha Tanzania na marekani Watanzania nao wanakushangaa unavyofananisha mwaka 1750 na mwaka 2017!! Unapouficha ujinga wako nyuma ya namba namba nazo zinajificha na kuuacha ujinga ukiwa dhahiri! Usiwe mfungwa wa historia mkuu.
 
Barbarosa, weye ni miongoni mwa watu wanaodhani mpaka leo kuwa nyumba nzuri, magari mazuri, chakula vizuri, mtu kujiamini, kutoa yaliyo ya mayoni na kudhania wa kudhania ni mambo anayedaiwa kuwa nayo mzungu tu. Uhalalishaji huu wa yaliyo batili kwa kutumia reference ambazo hazina uhusiano wala mashiko ni aibu sana. Halafu, naona umebadili avatar kutoka ile ya mbwa anakunya hadi hii anapumzika baada ya shughuli nzito ya kunya. Hongera. Halafu, ni mbwa wa kizungu, huh?
 
Tujifananishe kwa vinavyofanana,visivyofanana tuendelee kuviboresha ili vije kufanana(vyenye manufaa tu) hebu sasa tuanzie pale tulipowakutia! Miaka hiyo ya 1750 wao walishakuwa na university ila hawakuwa na ndege(aeroplane) sisi pia hatukuwaza kuwa nayo ila leo wao wana miaka 300 sisi tuna miaka 56 na wote tunamiliki ndege,wao waliiasisi demokrasia,sisi leo tuna uwezo wa kuiishi demokrasia,kama wao ndiyo waliogundua Nguo miaka hiyo ambayo sisi tulikuwa tunavaa majani ila leo hata sisi tunaweza kutengeneza zetu na tukawauzia hata wao,wao walipogundua umeme sisi hatukua hata na wazo hilo,ila leo tuna umeme wetu! Vitu ambavyo hatuna na wao wanavyo leo ni vichache tu! Ama sisi tunavyo kwa uchache, hivyo wakati wewe unawashangaa watanzania wanaoifananisha Tanzania na marekani Watanzania nao wanakushangaa unavyofananisha mwaka 1750 na mwaka 2017!! Unapouficha ujinga wako nyuma ya namba namba nazo zinajificha na kuuacha ujinga ukiwa dhahiri! Usiwe mfungwa wa historia mkuu.

Unachanganya mambo, sisi tumenunua ndege kutoka kwao, wao wametengeneza ndege na kutuuzia tena siajabu kwa mkopo ambao tutawalipa kwa riba, hivyo ni vitu viwili tofauti, huwezi kuukwepa huu ukweli na ndiyo maana hata kuna nchi zinaitwa developed, devoloping, na underdeveloped waliotunga hiyo misemo hawakuwa wajinga!

Hakuna jamii iliyoruka hizo hatua, ukweli na ni lazima tuukubali kwanza ndiyo tuweze kwenda mbele, nao ni kwamba sisi kwenye human development tuko nyuma sana sasa unaweza kutafuta sababu za kwa nini iko hivyo lkn hiyo ni Mada nyingine tena ngumu tu, lkn ukweli ni kwamba huwezi kulinganisha TZ yetu na EU, USA, au Uchina na Ujapani, yaani kutumia USA kama kipimo cha maendeleo yetu ni ujinga na hakuna mahali tutakwenda kufanya hivyo ni kutokuwa realistic na utajiumiza bure!
 
Barbarosa, weye ni miongoni mwa watu wanaodhani mpaka leo kuwa nyumba nzuri, magari mazuri, chakula vizuri, mtu kujiamini, kutoa yaliyo ya mayoni na kudhania wa kudhania ni mambo anayedaiwa kuwa nayo mzungu tu. Uhalalishaji huu wa yaliyo batili kwa kutumia reference ambazo hazina uhusiano wala mashiko ni aibu sana. Halafu, naona umebadili avatar kutoka ile ya mbwa anakunya hadi hii anapumzika baada ya shughuli nzito ya kunya. Hongera. Halafu, ni mbwa wa kizungu, huh?

Labda uko sahihi lakini najaribu kuwa realistic tu, kutaka TZ kuwa na demokrasia kama USA siyo kuwa realistic kwani demokrasia siyo kitu unachoweza kuhamisha ktk sehemu A kwenda B, bali inakuwa mahali fulani na inachukuwa vizazi vingi sana mpaka kuweza kufika hapo wengine walipo leo hii, na ndiyo maana unaona kuna nchi hazifwati demokrasia ya Wazungu kama Uchina au hata Singapore lkn wamepiga hatua kubwa sana kwenye human development kutuzidi, sisi tunaiga kila siku lkn bado tunakwama tu, ni kwa sababu pengo ni kubwa sana na tunataka kuliziba kwa spidi ya super sonic, haliwezekani tutajiumiza tu!
 
Ebu jiulize wakati tunaanza kutumia smartphone wenzetu walikua wapi na sisi tulikua wapi.?kwa mantiki yako inabidi tusubiri miaka zaidi ya 200 ijayo ndipo tuanze kutumia smartphones na haiwezekani

Haujanielewa labda, hoja yako ingekuwa sawa kama leo hii sisi tungekuwa na uwezo ya kuunda smart phone, lkn tunanunua, uwezo wa kuunda hatuna, kujenga micro electronic industry Tanzania na kuweza kuunda micro chips kwa elimu hii yetu ni bado sana, siwezi kusema haiwezekani lkn bado safari ni ndefu sana!
 
Kwahiyo tusubiri miaka 200 ijayo? Kwasababu hicho ndicho unachotaka
 
Kwa hiyo tuende tuendapo, tuandike hata kwa mate, ni kwamba weye hutaki Africa na hasa Tanzania iwe na demokrasia! Sasa, unapendekeza nini? Maana umekuwa msumbufu.
 
Tunapenda sana kujilinganisha na wengine, na kutwa kusema kwa nini hatuko kama USA, EU au sijui Uchina na Ujapani, lkn kuna jambo moja huwa hatutaki kulikubali na huwa tunalificha chini ya kapeti kwenye kuliganisha kwetu, na ukiniuliza mimi sisi tuko unfair sana kwetu sisi wenyewe, nalo ni hili nitatoa mfano, Columbia University (USA) kilianzishwa mwaka 1750 vs University of Dar es Salaam (TZ yetu) kilianzishwa mwaka 1970!

Sasa linganisha na hapo ujue USA inaitwa ni New World hivyo sijataka kuongelea old world ya EU, ina maana graduate wa kwanza Colombia alitoka kwenye mwaka 1770 huko graduate wa kwanza TZ labda kwenye miaka 50' kama ukichukulia waliosomea Makerere, Nairobi & Co.

Martin Luther aliandika PhD thesis iliyojulikana kama 95 thesis iliyoibadilisha Dunia mwaka 1517, alipata PhD University huko Ujerumani mwaka 1512, linganisha na sisi!

Hamuoni kwamba mnafanya maisha yenu yawe magumu bila ya sababu kwa kulinganisha visivyolingana? Kama ni demokrasia TZ tumeanza hata kulijua hilo neno miaka ya 80' tena mwishoni wakati USA tangu 1700' huko wanajadiliana demokrasia, hivyo fanyeni lililo muhimu na lililo ndani ya uwezo wenu kwa sasa hayo mambo ya kutaka kuwa kama USA au sijui EU mtachanika msamba, USA ina miaka zaidi ya 300 wakati Tanzania chini ya 60!

Kwanza hata hao Afrika ya Kaskazini tu (Moroko, Aljeria, Tunisia &Co.) wametuzidi hata miaka 50 kwenye kila kitu kama human development, lkn unakuta mtu anasimama anaongelea USA, kuweni realistic acheni kujidanganya hakuna miujiza, ...
Nilivyokuelewa mtu aliyezaliwa 1977 kujilinganisha na kutumia nguvu nyingi kupambana na mtu aliyezaliwa 1990s ni kukosa uweledi kwa kiwango cha mv bagamoyo
 
Nilivyokuelewa mtu aliyezaliwa 1977 kujilinganisha na kutumia nguvu nyingi kupambana na mtu aliyezaliwa 1990s ni kukosa uweledi kwa kiwango cha mv bagamoyo

Tofauti kati ya 1977 na 1990 siyo kubwa kwani hata kizazi kimoja hakijaisha bado, hapa nazungumzia tofauti ya zaidi ya miaka 300 na kuendelea, mtu aliyejenga Chuo Kikuu mwaka 1750 na amekuwa akikiboresha miaka yote kwenda mbele kuja kumlinganisha na mtu aliyejenga Chuo Kikuu mwaka 1960, ni kujidanyanya!
 
Kwa hiyo tuende tuendapo, tuandike hata kwa mate, ni kwamba weye hutaki Africa na hasa Tanzania iwe na demokrasia! Sasa, unapendekeza nini? Maana umekuwa msumbufu.

Hapana haujanielewa labda, sijasema kwamba sitaki TZ au Afrika iwe na demokrasia, kwani hata sina uwezo huyo, demokrasia siyo swala la kuamua kwamba tunaitaka au hatuitaki bali ni huja tu, hujilazimisha na kujipenyeza wakati wake ukifika, na hailazimishwi, muda ukifika utaona hata TZ mashoga watadai haki ya kuoana, watoto watadai uhuru wa kwenda disko na kuwa girlfriend na haitajalisha kama mzazi anakubali au la, muda ukifika Watanzania watadai hizi tunazoziita haki kama EU, USA na kwingineko, lkn hatuwezi kuchukuwa njia ya mkato!

Ninachokipinga ni kujaribu kulazimisha jambo ambalo kwa sasa muda wake haujafika, hilo halitowezakana, hata ukiangalia kwenye doctrine ya neocons kama George Bush alitaka kupeleka demokrasia Uarabuni lkn matokeo yake ni mabaya kuliko hata kabla ya demokrasia, angalia Libya, Iraki na sasa Syria, hivyo maana yake ni kwamba haya mambo hayalazimishwi kwani muda ukifika hujilazimisha tu!
 
Tofauti kati ya 1977 na 1990 siyo kubwa kwani hata kizazi kimoja hakijaisha bado, hapa nazungumzia tofauti ya zaidi ya miaka 300 na kuendelea, mtu aliyejenga Chuo Kikuu mwaka 1750 na amekuwa akikiboresha miaka yote kwenda mbele kuja kumlinganisha na mtu aliyejenga Chuo Kikuu mwaka 1960, ni kujidanyanya!
Unajua chuo kikuu cha kwanza kujengwa /kutumika na kutoa wasomi ilikuwa lini? Vipi kuhusu ugunduzi na matumizi ya maandishi? Viwanda vya nguo, chuma nk? Uongozi na ulinzi (yote kwa Afrika) yalianza lini? Tatizo siyo kuanza. Tatizo lipo kwenye vichwa vya viongozi wa Afrika. Tatizo. Maandishi yako tukiyachambua kwa historia utakimbia.
 
Kwahiyo tusubiri miaka 200 ijayo? Kwasababu hicho ndicho unachotaka

Hapana hatuna haja ya kusubiri na wala sicho nilichomaanisha, nilichomaanisha ni kwamba tuendelee kufanya yaliyo ndani ya uwezo wetu bila ya kujaribu kutaka kuwa kama USA au hata kujisikia vibaya kwa sababu watu wa USA wana uhuru sijui wa kufanya nini na sisi kutaka iwe hivyo bila hata ya kuelewa kwa nini USA wameamua iwe hivyo!
Tusijitanue kuliko upana wa miguu yetu tutapasuka msamba!
 
Back
Top Bottom