Kwanini sisi waafrika pekee tuna rangi nyeusi tii, tofauti kabisa na binadamu wa mabara mengine?

Mkuu umeilezea evolution kwa weledi na urahisi wa kueleweka sana .
Nadharia ya mageuzi(Evolution) inaweza kuwa mada rahisi au ngumu kuielewa. Leo nitajaribu kuifanya iwe nyepese, nitatoa mifano mirahisi sana. Kabla sijakujibu swali lako kuhusu rangi ya mwafrika, nitaanza kuelezea maana ya nadharia ya mageuzi(Evolution/evolution theory), uteuzi wa asilia(natural selection) baadae ntakuja asili ya mwanadamu na mwafrika na kujibu maswali yako ya ustaarabu(civilization) japo itakuwa subjective zaidi.

Nini maana ya Nadharia ya mageuzi(Evolution)? kwa lugha raisi ni maendeleo ya maisha hapa duniani, evolution ndio inayoongoza uwepo wa maisha hapa ulimwenguni zaidi ya miaka 3.5 billion iliyopita. Maisha yalianza kama bacteria na hao bacteria wakagundua sex(kujamiiana) wakaanza kufanya mabadiliko mpaka dunia kukatokea binadamu , samaki, bacteria ,mijusi ,vyura na nk. Kuelewe zaidi kuhusu evolution tutachukulia mfano wa wanyama ila ntatumia mfano wa ndege na baadae mbwa(nikizungumzia artifical selection).

Kwa wanyama evulution inaanzia pale kwenye mbegu za kiume(sperm cell) and yai la kike(egg) cell hizo huwa zinapata mutation kwasababu ya kimazingira au kwa bahati mbaya tuu (kumbuka hii ni bahati tu hamna cell inaamua ipate mutation) . Baada ya hii mutation kinachofuata ni kuunganisha hizi seli mbili na kutengeneza mtoto. Watoto wote wanaozaliwa japo wana fanana na wazazi wao ila kila mmoja ni wakipekee, pia viumbe wanapenda kuzaa watoto wengi kwasababu ya kuongeza nafasi ya jamii yao kuishi, maana watoto wengi wa viumbe hufa wakiwa watoto. Nikitolea mfano hili jambo la upekee wa watoto ni pale watoto wa wazaa mmoja wanakuwa wengine warefu, wengine wafupi, wengine wananguvu wengine wanyonge na hizi tabia zao zinachangia katika natural selection.

Sasa tuje kwenye natural selection hapa ndio utaelewa nini maana ya evolution vizuri. Tuanze na mfano aliotumia darwins.
Katika kisiwa flani x kuna ndege walipeperushwa na kibunga kutoka bara la amerika wakatua kwenye hiko kisiwa x. Hiko kisiwa kilikua na vyakula ya kutosha na hakukuwa na maadui ambao walikuwa wanawau . Ndege wakazaliana sana (kumbuka kuwa kiumbe chochote hapa duniani kinakazi tatu amabazo ni kujistiri asife, kutafuta chakula akishashiba anatafuta kiumbe mwenzake na kuzaa nae) kama unakumbuka hapo juu kuwa mzazi mmoja anazaa watoto wenye tabia na muonekano tofauti japa wanafanana na wazazi wao na wao wenyewe kwa asilimia fulani. Kwahiyo jamii ikaongezeka na chakula kiaanza kupungua , hapo ndio vurugu linapoanza . Kwahiyo katika utofauti wao, kuna ndege walipata midomo ya kupasua mbegu , wengine kula wadudu na wengine kula vitu vingine ila kuna wengine hawakuzaliwa na sifa za kama hao ndege wengine kwa hiyo wao kupata chakula ikawashida wakafa njaa na DNA zao hazikupitishwa kwa vizazi vingine. Tukirudi kwa walioweza kuishi wakawa wanajitenga kutokana na sehemu zao za kula, kwahiyo wapasua mbegu wakawa wanakaa kivyao na wala wadudu wakawa wanakaa kivyao(kizungu wanaita Niche).

Hii ikapelekea ndege kwenye niche moja kuzaliana na kurithisa tabia na muonekana wa kupasua mbegu na vilevile wale wala wadudu walifanya hivyo hivyo. Ikumbuke kila kizazi kinazidi kutofautiana na kizazi kilichopita kwahiyo kutokana na ushindani wale viumbe waliokuwa wanaweza kupambana ndio walioweza kuishia na kuzaliana (hii inaitwa population pressure which bring survival of the fit enough) ikapita miaka zaidi ya mamilion japo walikuja ndege wa iaina moja kwenye kisiwa baadae wakawa tofauti kabisa kufika hatua wakawa aina ya ndege tofauti(specie) kiasi kwamba hawawezi tena kuzaa (wapasua mbegu walikua hawawezi tena kuzaa na walala wadudu).
View attachment 2059776
hapo juu ndio ndege niliowazungumzia.

Kwa mfano huo wa juu nadhania umeanza kuelewa maana ya evolution. Ikumbukwe evolution haipangi kuwa hii kitokee huwa anatokea kwa bahati ila natural selection ndio inamalizia kazi ya kuchukua wale ambao wameweza kuhimili mazingira. Kwa kuongezea tuu evolution pia haiweizi tokea kwa kitu ambacho hakipo mfano pundamilia hana mabawa kama ndege hii itampasa pundamilia arudi hatua nyingi nyuma za kievolution afikie ile hatua ambapo zebra na ndege walishare mzee wao mmoja(so evolution has no reverse).

Mfano wengine ni kati ya mwanaume na mwanamke wanaume hawahitaji maziwa ila yapo hii inatokana na gharama ya kutengeneza gene inayoondoa maziwa kwa mwanaume kuwa kubwa sana na vilevile jinsi ya ovary zinabadilika kuwa pumbu na kinembe kuwa uume (Nimetumia mfano wa mwanaume kutokea kwa mwanamke , kwasababu binadamu wa kwanza kinadharia na kiushahidi alikua mwanamke).
Kwahiyo cha kuchukua kutoka hapo juu kabla hatujaendelea mbele ni evolution hutokea kwa bahati(bila mpangilio) ila inapangwa vizuri na natural selection, pia evolution hairudi nyuma(kama yanga nyuma mwiko) .

Mpaka sasa nahisi utakuwa umeshanielewa mambo ya kuhusu evolution na natural selection sasa tunaweza kuikabili nadharia ya asili ya mwanadamua. Kabla hatujaenda mbali nataka kukusihi ufute ile picha uliyosoma sekindari na shule ya msingi kama sisi tumetokana na sokwe na evolution of a man/evolution ni kama mstari mmoja
View attachment 2059780
Hii picha ya juu imetumika kuchanganya watu wengi ulimwenguni japo ilitumika kurahisia maelezo . Kwahiyo chukulia asili ya binadamu na mabadiliko yake kama picha hapo chini.
View attachment 2059783
Binadamu anatoka na genus Homo na specie Sapiens, japo sisi ndio specie iliyobaki kwenye genus homo na sisi ni wamisho kufika hapa duniani. Sitoelezea sana jinsi ya sisi imekuwaje tumeweza simama na kuwa na akili hii ianhitaji uzi wake maalumu.
Tuje sasa kwenye mada yenyewe kwanini mwafrika ni mweusi na wengine ni weupe na kwanini nchi zinazoitwa zina joto hazina watu weusi.

Naomba nikukumbushe tuu kuhusu mutation niliyoelezea hapo kuwa kila kiumbe kanapitia mutation na hizo mutation kama zikitokea kwenye mbegu za uzazi basi sitarithishwa kwa vizazi vijavyo. Binadamu wa kwanza alikuwa mweusi na mpaka sasa mwafrika ni mweusi inatokana na gene moja inayoitwa melanin(gene ni kipande kwenye DNA ambayo ndio inataarifu kiwanda cha kutengeneza protini(ribosome)) hii melanine ndio inatupa dark pigmentation lakini inatumika kuzuia seli za binadamu za ngozi zisiuliwe na UV kutoka kwenye jua , maana miale ya UV huwa zina haribu cell DNA ambayo inaleta leta cancer ndio maana albino huwa wanapata cancer za ngozi kwasababu hawana/haifunguki hii gene ya melanin. Ila pia miale ya jua inatusaidia kutengeneza vitamini D(kwa ajili ya mifupa na meno) kwasababu sisi binadamu hatuna uwezo wakutengeneza vitamini yeyote( sina uhahika labda kuna chache tunaweza tengeneza).

kwahiyo baada ya kungundua umuhimu wa melanin na umuhimu wa vitamini D tuanze sasa safari ya binadamu kubadilika rangi, Kama inavyojulikana binadamu wa kale alikua mtu wa kutangatanga kwahiyo kundi la bindadamu liliondoka huku tanzania(Afrika mashariki) miaka kati ya (10000 - 10000) hiko kipindi bado dunia ilikua na baridi hao watu walipofika bara la ulaya tena hapo caucasus walifanya makazi wengine walisambaa kwenda asia wengine waliingia amerika ya kusini. Ila tutajadili ya hawa wa ulaya kufanya uzi uwe mfupi.

Kama nilivyokwisha kueleza mambo ya evolution na natural selection, tuanze angalia sababu ya kwanza ni uchache wa miale ya jua kwahiyo binadamu wa enzi hizo wakaanza pata tabu kutengeneza vitamini D3 kwaajili ya meno na mifupa nadhani mnajua mtu akiwa na mifupa milaini hawezi kimbia kwahiyo kutafuta chakula kwakwe inakuwa shida (nakukumbusha kiumbe chochote kina kazi tatu kwa mtirirko kuishi kula na kuzaa) kwahiyo watu wenye mifupa milaini walikufa mapema bila kuzaa na vizazi vyao vilipata vurugu lile lile na kwenye meno kama unameno mabovu kupata magonjwa na kushambuliwa na bacteria,virus na vidudu vingine ni rahisi kwahiyo nao walikufa mapema na ikumbukwe kibogoyo hali nyama (enzi hizo binadamu alikua hajagundua kilimo so chakula ni nyama au matunda).

Ikumbukwe evolution haisimami kwahiyo katika wale waliofika ulaya wakazaa watoto ambao ni weupe wao ikawa rahisi kutumia miale hafifu ya jua la ulaya kutengeza mifupa yenye nguvu kwahiyo waliweza kupata chakula na wao wakazaa watoto walirithisha hizo mitutation za melanin D so baada ya vizazi vingi watu weusi walipotea na wakabaki wazungu hapo tunaona natural selection watu wote unaowaona ni weupe asili yao jua ni hapo Caucasus.

Nikijibu swali la kwanini waarabu hawawi weusi tena , ninakujibu kwa nadharia mbili ya kwanza nilishasema kuwa evolution huwa hairudi nyuma kwasababu ya gharama na yapili inaitwa collective learning hii imesaidia binadamu asibadilike bali aishi na kuyaongoza mazingira yake. Mwarabu mweupe (Ikumbukwe uarabu ni tamaduni na sio race) yupo hapo jangwani si zaidi ya miaka 6000 hii haiwezi mpelekea abadilike haraka na hivyo pia kipindi mwarabu mweupe anaanza tawala hapo mashariki ya kati kilimo kilishagunduliwa na nguo pia zilishagundulia kwahiyo jua halikuweza kumchoma kama vile wazee wake walivyotoka afrika wanatembea uchi. uwezo huu wa jamii kujifunza maarifa kutoka kwa vizazi vilivyopita ndio inaitwa collective learning hii ndio imasaidia binadamu kuweza kupambana na natural selection kwa kiasi kikubwa.

Tuje kwenye civilization hilo ni somo lingine kubwa nimeona nisilijibu kwasasa ila ntabainisha vitu vya kusoma ili uweye elewa . tatufa za sababu kwanini mageuzi ya kiviwanda yalitokea UK na sio china( wakati china ilikua inachimba makaa ya mawe na chuma zamani kukilo uingereza)
NB: Mimi sio mtaalamu wa maswali ya evolution, nimejifunza yote haya kwa kuwa ni udadisi wangu kwahiyo kama kuna taarifa hapo nimeandika sio sahii naruhusu kurekebishwa na kama kuna kitu kinahitaji ufananuzi zaidi naruhusu pia kujaziwa. Elimu ni bahari sayansi haina mwisho hamna kitu sahii milele kwenye sayansi bali sayansi ipo kufichua uongo wa nadharia za huu ulimwengu.
Mimi ni mfuasi wa evolution na natural selection , nameandika hii ili msomaji wangu usipate maswali kuhusu niliyoongea kama nayaamini au nafundisha nisichoamini pia siamini katika mambo ya dini,mizimu,uchawi ,mungu na mashetani yake.
chamwisho kabisa mimi sio mwandishi mzuri nimejitahidi kuandika kwa kiswahili hizi mada ngumu naoma tuvumiliane kwa makosa ya kisafuri na kisanifu.
 
Wakuu merry chrismass.

Nimekaa nimewaza na kufikiri naona kama kuna kitu hakiko sawa kuhusu sisi waafrica.

kitu cha kwanza ni kwanini sisi waafrika pekee tuna rangi nyeusi tii, tofauti kabisa na binadamu wa mabara mengine, mfano ulaya ni weupe,asia ni weupe,australia ni weupe,america kaskazini na kusini ni weupe (isipokuwa black americans tu ambao nao pia wanatokana na mababu zetu waliopelekwa utumwani kule).
so najiuliza kwanini only africans are the black people ? Kwa majujibu wa takwimu za population, dunia mpaka sasa ina watu bilion 7.8, na africa pekee ina watu bilion 1.3 tukijumlisha na yale masalia ya america na carribean labda tunakuwa 1.4 au 1.5 billion ndo watu pekee weusi duniani, maana ake kati ya watu bilion 7.8 weusi ni 1.5 bilion pekee,wengine wote wanaobaki ni weupe, kwanini yani weupe mbona wengi sana, je imekuwaje weusi wakawa wachache alafu wametengewa bara lao, maana mabara yote 6 yenye watu matano ni weupe isipokuwa bara moja tu la africa ndo weusi tii why mbona sipati majibu sahihi ? Sijichukii kwa sababu mimi mweusi ila najiuliza tu kwanini waafrica pekee ndo weusi ? Alafu pia wakawa wachache kuliko weupe ? Kuna laana gani ilipita hapa ebu nambieni wadau.

Kitu cha pili, kwanini sisi watu weusi tunaonekana tuko nyuma kwa karibu kila kitu, kuanzia ustaarabu watuletea watu weupe, teknolojia nyingi zimetoka kwao (asilimia karibu 90 ya kila tunachotumia waafrica kilianza kwanza kugunduliwa na mweupe), kwanini mweusi akawa nyuma sana ? Kuna laana gani hapa ? Kwanini sifa ya mwafrica ni ya umaskini na ujinga tu why this ? Walitutawala kwa karne karibu 4, wakatutumikisha kwenye ardhi yetu wenyewe na kutufanya watumwa na sisi tukakubaliana na hali, why only africans we became very stupid ? Mbona sisi hatukuanza kuwatawala ila wao weupe wakaanza? Tuna rasimali kibao ila tumeshindwa kuzitumia zituboreshee maisha badala yake bado tumkabidhi mtu mweupe, kwanini sisi watu weusi tuna nini ebu nipeni majibu!

Cha mwisho, kwanini ngozi nyeusi inabaguliwa (racisim) na kuonekana duni, nadhani tunashuhudia wenzetu walioko ng'ambo jinsi wanavyobaguliwa na kuitwa nyani, ina maana sisi weusi duniani tulikuja bahati mbaya au ni vipi yani !...niki mnukuu mwarabu moja mweupe pale libya ambaye aliwateka waafrica wakiwa wanatorokea ulaya kupitia mediterania aliwaambia hivi "mnaenda wapi nyie watu weusi kutoka kuzimu watumwa mliolaaniwa ninyi"

Unaweza kuona ni jinsi gani sisi watu weusi tunavyochukuliwa na watu weupe, sasa kwanini sisi waafrica tukaumbwa weusi (rangi ya kudharaulika,duni) alafu tukawa wachache na bado haitoshi tukapewa bara la peke yetu weusi (bara la africa) wakati weupe wao wakaumbwa wengi alafu wakasambazwa kwenye mabara matano tofauti na pia wakapewa upeo wa uelewa kuliko sisi ? Au ni kweli mungu alitulaani nini sisi weusi ? Au sisi weusi ni uzao wa shetani kama wanavoamini baadhi ya weupe ?

NB: Sijaudharau uafrica wangu ila najiuliza tu kwanini mweusi anadharauliwa na kudunishwa wakati mweupe yupo mbele yetu kwa karibu kila kitu?
kwa sababu hamna akili
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom