Kwanini sio rahisi kusikia mganga wa kienyeji kutoka moshi?

mkubwa wapo ila hawavumi tu...ukienda huko wale wazee hasa wa koo wanajua fulani ni mtaalamu wa mitishamba, inawezekana hawawaiti waganga ila ukweli ni walewale tu... sema tu si unajua kuna makabila ambayo yanavuma kwa sababu yanaaminika ni kiboko katika mambo haya kama vile watu kama kutoka sumbawanga, tanga lakini pia siku hizi hata kenge nao wanaingia kwenye msafara wa mamba, unaweza kukuta masawe ndo mganga, ila kwa kuwa sumbawanga inavuma basi atabadili jina na anapotoka badala ya moshi atajifanya anatoka sumbawanga ili auze.

Ila hii haimaanishi kuwa mahali pengine hawapo, wapo ila hawavumi!!!
 
Kwetu cc wachagga tuna mtu anaitwa "mwangaliaji" hatuna mganga kwa neno la kichagga unasema "kulasha" wao hawatumii tunguri au miti shamba,wanatumia mmea wa "isaleh" kwa mfano,labda biasha haiendi vizuri,kuna matatitizo ndani ya familia,magonjwa ya ajabu kama,kuweweseka,homa za vipindi nk. Ukienda kwa "mlashaji"(kulasha) akichukua jani la mmea wa ishale,wakati analichuma tu,akianagalia jinsi lilivyokatika,1 kwa 1 anajua nini kinachokusibu. Hawatoi dawa,dawa siku zote ni mbuzi au kondoo. Tafuta mbuzi au kondoo aliyenona, mchinje. Kwa ajili ya kuwapa wazee/mababu(sio mizimu) Inabidi asomwe kimila baada ya kuchinjwa kwenye ini na utumbo,. Nataka niwahakikishie kama kulikuwa na tatizo total linaondoka. Kiukweli hamna mganga mchagga, wapo "walashaji'"
 
Wa moshi wawe waganga afu kupika vitimoto na wizi afanye nani? Huo ni mgawanyo wa majukumu. Ni kama wapare walivyo washona viatu na mafundi cherehani, wa iringa mahaousigeli, ...
dah umenikumbusha wapare pale motown jinsi walivyojaza korido za majengo kwa viatu vyao. nimevivaa sana enzi hizo
 
king'asti...mke mwe...ndio wewe unanisema vinaya hivyo? haya bwana....btw HAPPY NEW YEAR MKE MWEH!
 
Umeanza kwa fact mistari miwili ya mwanzo ila sijui nini kilitokea baadaye ukaanza
kuharisha toa utumbo huo fasta!
Wewe ndo umehara bila kujua,usipende kusifiwa hata pasipostahili,nenda katafute maji ukajitawaze fasta!
 
acha mawazo mgando! Ushawahi kuona kibao cha kusema mganga anatoka kagera, lindi, mtwara, mara, mbeya etc, umeona moshi tuu! Kama kupiga hatua ndo kigezo watu kibao kivyao bila kujalisha ni wa wapi wamepiga hatua kimaendeleo, be smart!
 
Nimekua Arusha kwa muda mwingi hii desember nimekutana na vijitangazo kibao kuhusu waganga wa kienyeji wengi utasikia wanatoka rukwa,sumbawanga,ufipa,kigoma alakini huwezi sikia mganga kutoka moshi,vipi hili lina uhusiano gani na maendeleo na changamoto zima la maendeleo ya kiuchumi kielimu na mambo mengine. Vipi kuna ukweli hapo au ni mtazamo wa watu??au tuelewe nini kuhusu hizo sehemu watokapo hao waganga??

umewahi sikia kwani kuna mganga toka dar es salaam?
 
Nenda Msaranga, msitu wa Tembo au TPC. Utakuta waganga wengi tuu.

Haha haaa umenikumbusha siku moja nilipita msitu wa tembo kwenye supervision kama eneo langu la kazi, ni eneo linalosifika kwa uchawi na uganga hata kupita hata huko ufipa na kigoma ambako kunasifika! Maana mzee mmoja kwa jina la ngowi alitamka wazi kuwa pale ni kiboko ya uchawi watu kutoka sehemu mbalimbali za tanzania hufika kuchukua dawa za utajiri pale na kabila maarufu pale ni wa"K".
Ninachotaka kusema ni kuwa hakuna sehemu ambayo inakosa haya mambo ya kishenzi!
 
Jamaa mkoa ule hawana imani na mambo haya ya uganga uganga,hata pia c wateja sana kwenda kuganguliwa, hata kwenye utafutaji jamaa wanachemsha akili plus wizi lkn c dawa dawa kama Wakinga wa Makete na kutapakaa Iringa nzima
Mbuzi kweli wewe sisi wakinga hatutumii dawa
 
Dini ilienezwa sana maeneo yao huko uchagani kiasi kwamba idadi ya watu wanao practise hayo mambo ya kiganga ni ndogo mno almost difficult to find! But its possible kuwakuta fake pastors wa kichaga wanaoongopea waumini kwamba wanaweza kuwatatulia matatizo yao...
 
Waganga wachaga hawapo. Wachaga hawakupewa vitu kama hivyo vipo sana mikoa ya kusini
 
Back
Top Bottom