Kwanini Sikukuu za miaka ya leo hazina tena mvuto/tashwishwi?!

Nakumbuka miaka ya nyuma Krismasi ilingojewa kwa hamu na ghamu!

Sikukuu hiyo ilikuwa ni Tukio kubwa na la aina yake katika jamii yote. Yafuatayo ilikuwa ni lazima yafanyike kabla ya Sikukuu hiyo;

Nguo mpya,

viatu vipya,

maandazi/wali,

sadaka,

pesa ya Aleluya.

Na bila kunukia mafuta aina ya Mamiz mwilini mwako hakika rafiki zako watakucheka!

Lakini pia,kurejea nyumbani huku ukiwa na miwa, mapera/embe ukiwa umezibeba ndani ya shati jipya maalum kwa Sikukuu hiyo ilikuwa si ujanja!

Mhenga mwenzangu karibu nawe uorodheshe baadhi ya mambo mengi yaliyotupatia hitimisho la kungojea Sikukuu hiyo pendwa km ya leo!
Mkuu kama hela unayo basi leo ni crismas kama huna bela leo ni j4
 
Shamra shamra zimepungua sana,hii Sikukuuu miaka ya nyuma ilikuwa moto.Kwanza wiki kabla "chingo beli" za kutosha.Lakini siku hizi ni kuforward sms "mti wa mkrismas tuu"
 
Enzi hizo lazima hapo mtaani tukinukishe na baruti aisee siku hizi woiii
Watoto wa siku hizi hata matairi hawachomi,Waoga sana.Sisi ilikuwa lazima tuwashe mapira hata kama Kuna patrol ya polisi.Baruti & matairi ni Pie.....
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom