Kwanini siku hizi watu wengi hupenda kusaidia watu wa nje zaidi kuliko ndugu zao?

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
250
Habari Wakuu
.
Binafsi Nimekuwa Najiuliz sana hili swala kwa kuwa nimelitazama kwa kina jambo hili na kugundua kuwa limekuwa tatizo kubwa linaloadhiri jamii nyingi sana.
.
Yaan ukiongea na watu watano juu ya matatizo ya familia zao watatu kati yao watakwambia juu ya tatizo hili la watu wengi wenye uwezo wa kifedha kwenye familia kupenda kusaidia watu back zaidi kuliko ndani ya familia au ukoo wake,
.
Mfano katika familia yangu wapo ndugu kibao ambao wapo tayari kusaidia watu back kuliko ndugu wa damu
.
Simaanishi kuwa watu wa nje ya familia wasisaidiwe la hasha..! ila waswahili husema kuwa
Huwezi Kwenda Kwa Jirani Kama Hujatokea Kwako...
.
Je Ni Zipi sababu za tatizo hili kushamiri kwa kasi sana
.
Nawasilisha.....
 
Sanja

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
503
250
Kwasababu koo nyingi zinaishi mbali, na yule aliye karibu( jirani yako) ndio msaada wa kwanza kwa jambo lolote. Wahenga walisha sema fimbo ya mbali haiui nyoka; na kuna kitabu kinasema mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
 
jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,074
2,000
bahat nzur nshakua muhanga wa kusaidia ndg...
1.wanakatisha tamaa mno maana unaeza jinyima kwa ajili yao lakin wao hawajal wanaona kua ilikua n haki yao kusaidiwa
2. weng n wavivu, au anafanya kitu kivivu vivu cuz anajua n cha ndg yake....
3.wanadharau and sometyms hua hawaapreciate ulichowasaidia
4. wana maneno mno hasa unapojarib kumwelekeza.....
5. anaeza kukukosanisha na uko mzima na kufanya wengine waone ww n mbaya kwa sabab ya maneno yao
mm nshanawa mikono
 
Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
250
Kwasababu koo nyingi zinaishi mbali, na yule aliye karibu( jirani yako) ndio msaada wa kwanza kwa jambo lolote. Wahenga walisha sema fimbo ya mbali haiui nyoka; na kuna kitabu kinasema mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
Kuna wakati hicho kigezo cha umbali hakipo
lakini bado mambo yanakuwa hovyo hovyo"
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,861
2,000
Wengine ni mazoea yao tu mkuu kutokana na tabia waliyojijengea, unaweza kukuta labda hana mahusiano mazuri na nduguze
 
The Chosen One

JF-Expert Member
May 24, 2017
3,584
2,000
Na kingine hatupendani baadhi hawapo tayari kumsaidia ndunguye kitu ambacho kitamfanya awe na uwezo kuliko yeye
 
butron

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,417
2,000
bahat nzur nshakua muhanga wa kusaidia ndg...
1.wanakatisha tamaa mno maana unaeza jinyima kwa ajili yao lakin wao hawajal wanaona kua ilikua n haki yao kusaidiwa
2. weng n wavivu, au anafanya kitu kivivu vivu cuz anajua n cha ndg yake....
3.wanadharau and sometyms hua hawaapreciate ulichowasaidia
4. wana maneno mno hasa unapojarib kumwelekeza.....
5. anaeza kukukosanisha na uko mzima na kufanya wengine waone ww n mbaya kwa sabab ya maneno yao
mm nshanawa mikono
Mkuu namba tano umegonga Ikulu mimi yashanipata hayo,kuna Kaka yangu wa damu kabisa ananifanyia mambo machafu sana alafu nishamsaidia sana.Ndugu nuksi mkuu hawafai.
 
Bandu Ncheche

JF-Expert Member
Jul 9, 2016
518
500

Hiyo namba 5 inanihusu sana, unaweza ukawa ulikuwa unamsaidia ndugu yako vizuri tu, lakini ikitokea siku mkapishana kauli baaaasi utakorofishana ndugu kibao, na bahati mbaya huyo ndugu awe ni wa upande wa ndugu yake baba/Mama,ugomvi wenu hufika mbali sana
 
Kodjoe Borris

Member
Jan 15, 2017
95
125
Sio kweli, kama kupenda sifa hata ndugu wanaweza wakakupa sifa
sio rahisi kusifiwa sana na ndugu kama mtu baki atakavyokusifia kwa sifa kede kede na kukupamba! Pia ndugu kutosaidiana kunachangiwa na malezi ya mtu na nduguze, mahusiano na mtu aina gani mtu kayaingia! hapa bongo baadhi ya watu wa jamii flani wana utamaduni wa kusaidiana wakati wengine wanajitahidi flani atoke ili aabudiwe na watu jamii yake(hawa ndio haswaa hupenda kusaidia watu baki)
 
ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,298
2,000
Wengi wetu tunapowasaidia ndugu ndipo wanatusema vibaya na hata kukiharibia. Uliza watu walioanza mradi wakaweka ndugu kusimamia. Asilimia 80 ya ndugu wanaharibu kabisa na hata kuiba kidogo kinachopatikana. Mimi na hata marafiki zangu kadhaa wameshakutwa na dhahama hiyo.
 
jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,074
2,000
Mkuu namba tano umegonga Ikulu mimi yashanipata hayo,kuna Kaka yangu wa damu kabisa ananifanyia mambo machafu sana alafu nishamsaidia sana.Ndugu nuksi mkuu hawafai.

Mmoja huyo alikuja anashida hajiwezi....nikajibana bana nikamkopesha mtaji alivofanikiwa akawa ananidharau na kejel juu.. et kwanza unanidai tsh ngap nkupe hela yako???
 
butron

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,417
2,000
Mmoja huyo alikuja anashida hajiwezi....nikajibana bana nikamkopesha mtaji alivofanikiwa akawa ananidharau na kejel juu.. et kwanza unanidai tsh ngap nkupe hela yako???
Mkuu unanipa machungu,mambo ya ndugu siyataki kuyasikia kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom