Kwanini Siku hizi wanajeshi/Askari wastaafu wanapatwa na ugonjwa Wa Kupooza? (Stroke)

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,525
21,999
Wadau habari!
Katika tembea tembea nimeshuhudia wazee wastaafu walio wengi (SIYO WOTE) ambao walikuwa wanajeshi/ Askari Wa jamhuri walio pigania muungano Wa nchi hii Kwa mazoezi chungu mzima! Wakipatwa na huo ugonjwa hatari sana Wa Kupooza mwili upande (Stroke).

Kinacho nifanya niulize swali hili ni pale madaktari na wataalam wanaotibu ugonjwa huo wanapotaja miongoni mwa Tiba ni pamoja na Kufanya mazoezi!

Ikumbukwe kwamba Mwanajeshi/Askari ni Mtu ambaye amepitia mafunzo (Mazoezi) si chini ya miezi (6 hadi 9) mfululizo, na miezi kadhaa Kwa mafunzo maalum (professional course).

Kama wizara ya Afya au serikali haijashtuka, Mimi binafsi nimeshitushwa na jambo hilo ambalo linaendelea kuwaumiza wazee wetu wastaafu. (Ingawa kuna makundi mengine ya wahanga kama walimu n.k) lakini kwanini na Wanajeshi?

Swali; kama Tiba ni mazoezi na kuepuka Vyakula vya mafuta; Je; Nini hatima ya wazee wetu wasiokuwa askari? Wanaofanya push-up wakati Wa msimu?
 
Babu yangu alikuwa polisi, aliwahi niambia enzi zao kulikuwa na gwaride kila siku asubuhi na jioni wakati wakuripoti kituoni na kuondoka, Gwaride lilikuwa gwaride kweli kweli hadi jasho linawatoka. Leo hii gwaride halipo tena, watu sahivi wanaripoti vituo vya kazi Kwa kuitwa Row-call (majina tu)! Utasikiaa Copro kamugisha- nipo afande! Wakati enzi zile row call iliitwa baada ya gwaride- na afande aliitika Kwa kukoki siraha! Leo hii askari anakitambi utazani ana mimba, Leo hii unakutana na askari ananukia pafyumu tupu, mazoezi Hamna, watu wanaendesha magari full AC tena wakiwa wamevaa sare! Ingawa mkuu Wa majeshi mpya kapiga marufuku wanajeshi kuvaa sare wanapoendesha magari yao mtaani na atakaye kamatwa atapokonywa hata gari lenyewe! Je ni nani wakuwakamata?
Tusitafte mchawi Wa ugonjwa! Chanzo ni wao wenyewe.
 
Kazi za kijeshi ni stressfull!wewe maisha yako yote unafunzwa na kuhimizwa kununa pasina sababu usipate stroke kwa nini?
 
Wazee wetu kule vijijini wanastaafu, wanalima, wanadesha baisikeli na wafanya mazoezi huwezi sikia ugonjwa huu labda uwe Wa kichawi
Wale wako na furaha moyoni hata kama kazi ni za harubu lakini hawa wanajeshi saa zote wanajizoesha kununa na kukunja sura ambayo hukaribisha stress ambayo pia huandaa mazingira murua ya stroke!
 
Babu yangu alikuwa polisi, aliwahi niambia enzi zao kulikuwa na gwaride kila siku asubuhi na jioni wakati wakuripoti kituoni na kuondoka, Gwaride lilikuwa gwaride kweli kweli hadi jasho linawatoka. Leo hii gwaride halipo tena, watu sahivi wanaripoti vituo vya kazi Kwa kuitwa Row-call (majina tu)! Utasikiaa Copro kamugisha- nipo afande! Wakati enzi zile row call iliitwa baada ya gwaride- na afande aliitika Kwa kukoki siraha! Leo hii askari anakitambi utazani ana mimba, Leo hii unakutana na askari ananukia pafyumu tupu, mazoezi Hamna, watu wanaendesha magari full AC tena wakiwa wamevaa sare! Ingawa mkuu Wa majeshi mpya kapiga marufuku wanajeshi kuvaa sare wanapoendesha magari yao mtaani na atakaye kamatwa atapokonywa hata gari lenyewe! Je ni nani wakuwakamata?
Tusitafte mchawi Wa ugonjwa! Chanzo ni wao wenyewe.
Mleta mada ameuliza kuhusu wanajeshi wewe unaleta mambo ya polisi, wewe vipi!
 
Kazi za kijeshi ni stressfull!wewe maisha yako yote unafunzwa na kuhimizwa kununa pasina sababu usipate stroke kwa nini?
mkuu umeongea ukweli.Baba yetu alikua polisi,muda wote alikua mtu wa kununa,kufoka na kututwanga bila hata mpangilio hadi tunajiuliza kosa letu ni nini? Afande wetu baada ya kustaafu haukupita muda kapigwa na stroke. Anavyo cheka cheka saa hivi ndio tumegundua kumbe anatumia meno ya bandia.Mungu amponye babaangu.
 
Kwani kuna tofauti?

Mbona wanasemaga 'Jeshi la Polisi?'
Mwanajeshi ni askari yeyote anayetokana na :
1. Jeshi LA wananchi
2. Jeshi LA police
3. Jeshi LA magereza n.k
Ingawa Hata wale Wa Jeshi LA wokovu wanastahili waitwe Wanajeshi pia. ...Kwa maana nyingine mwana+jeshi ...mwana ni kiunganishi cha ujumuika Wa jeshi lolote hapo juu
 
Maisha waliyoyazoea ujanani hadi kustaafu humkosesha mikikimikiki. Vilevile kuwepo kazini humfanya mtu kujihisi salama na kujiamini. Sasa anapotoka kazini anakuwa kama mpweke katika jamii mpya na kuwa mtu aliyekata tamaa katika ulimwengu mpya. Ukijumlisha, kwa mfano alikuwa na cheyo /mamlaka halafu anarudi uraiani anaona watu wanamuona wa kawaida tu au kumshangaa kimtindo, inaumiza na kunyong'onyeza sana.
Pia akifikiria alichopata kiinua mgongo ya kwamba hakirudii tena. Hivyo basi akitumia hovyo imekula kwake. Halafu wengi huwa hawaujui ujasiriamali. Na hii husababisha kutokuwa na mbinu ya kuitunza fedha na kuiendeleza. Huumia moyo sana. Kule jeshini yeye alikuwa ni www! Yaani "women, war and wine" (siyo rasmi usiitolee macho). Kwa ufupi alikuwa wa matumizi ya hovyo ingawa si wote.
Kwa ufupi ni hayo mafupi hufupisha afya hata uhai wa ex-soldiers wengi. Hata hivyo changanya na zako.
 
Mwanajeshi ni askari yeyote anayetokana na :
1. Jeshi LA wananchi
2. Jeshi LA police
3. Jeshi LA magereza n.k
Ingawa Hata wale Wa Jeshi LA wokovu wanastahili waitwe Wanajeshi pia. ...Kwa maana nyingine mwana+jeshi ...mwana ni kiunganishi cha ujumuika Wa jeshi lolote hapo juu
Kwahiyo hata police ni mwanajeshi
 
Kununa kwao ni kutokana na kuifanya kazi ya jeshi haliyakuwa hawaipendi ila basi...!

Katika hali ya kawaida haiwezekani kila siku stressfull na kununa..!
Kweli kabisa.
19fc1724b13b6e5dd5bb57a731911ab8.jpg
 
Back
Top Bottom