Kwanini siku(days) zilipewa majina ya kiislamu..?

NAOMBA NIKUAMBIE KUWA ULICHOKIANDIKA HAPO NI VIFUPISHO TU ILA YANAVIREFU VYAKE HALAFU KINGINE MAZOEA NA URAHISI WAKUTAMKA NENO NDO UMECHANGIA HAYO YOTE
 
Habari zenu wanajf ,kama kichwa cha habari kinavyosema ni hivi..

Jumatatu
apo kuna majina mawili juma na tatu,juma linafaamika sana na tatu linafaamika pia nilakike katika zunguka yangu nilkutana na tatu kama wanne wote waisilamu.

Jumanne
ili linafaamika ingawa pia kunawakristu hulitumia lakini wengi wao waisilamu.

Jumatano
Apa juma kamakawaida lakini tano sijawai liskia popote.

Alhamisi
Apa kunamajina mawili kuna Ali na Hamisi.

Ijumaa
Apa nilshakutana na watu wanaitwa "jumaa"kama wa tatu ivi ni waisilamu.

Jumamosi
Apa lipo jina la "juma" ila "mosi"sijawai kuliskia

Jumapili
Apa yapo majina mawili tena kuna "juma" na "Pili"nilishakutana na jina la Pili mala tatu wote waislamu.

Kwa ayo majina hakuna tatzo lolote ila tu kwanini yatoke upande mmoja

Karibuni ndugu mnipe majibu.....
Ukitoka hapo utakuja kuuliza kwanini majina ya miezi yanatumika na viongozi wa serikali, mfano kuna January Makamba.

Kwa kifupi nikujulishe tu kwamba hayo majina yanayoshabihiana ni eidha kwasababu ya utamaduni wa baadhi ya watu wa pwani kutoa majina kulingana na jina la siku mtoto alizaliwa, utamaduni huu upo pia kwa waghana..!!!
 
Nilifikiri kuna tofauti kati ya kiarabu lugha na uislamu dini. Pili hata mimi nisiejua kiarabu najua juma ni kitambulisho cha mwanzo cha siku fulani ndani ya wiki. Mosi, pili, tatu, nne na tano ni namba. Labda alhamisi na Ijumaa ndio tofauti. Ni vizuri tujue kama haya yana maana gani au imekuwaje yasiitwe jumasita na jumasaba? Nawasilisha.
Alkhamisi inatokana na neno la kiarabu 'khamsa' yaani tano, kumbuka kwa kiarabu jumapili ni Al-ahad yaani (siku ya) 'kwanza' ikaendelea hivyo hivyo 'Al-Ithnaan' yaani (siku ya) 'pili' vivyo hivyo mpaka 'Al-khaamis' yaani (siku ya) tano.
Sasa neno 'Al-jumu'ah' maana yake ni kusanyiko. Hii ni siku ya mapumziko na kutembeleana hivyo watu hukusanyika pamoja na kufurahi kwa ajili ya mapumziko ya wiki. 'As-sabt' imetokana na neno Sab'at yaani Saba. Hapo siku saba za wiki zimekamilika.

BTW; I'm stand to be corrected
 
Kuna siku utakuja kutwambia nukta,sekunde,dakika na saa nazo zinz majina ya kiislamu.
 
Hii mpya kama kiswahili ni kiarabu! !! Yaani nikiingia uarabuni napiga kiswahili nao wanapiga kiarabu tunaelewana! !!!! Sidhani hata kama kuna maneno lukuki ya kiarabu.
Asilimia 90 ya watanganyika tungeweza kusoma kuruani.
 
Jina Pili,Tatu, Tano au Khamis linaweza kuwa ni huyo mwenye jina kazaliwa jtatu, jnne au jtano lakini pia mtu mwenye jina kama hilo anaweza kiwa waPili kuzaliwa kwenye familia, waTatu au waNne. Na sio lazima awe Mwislam wapo hata Wakristu wenye majina hayo.

Lakini ukumbuke pia kuwa Kiswahili kimekopa maneno mengi toka lugha ya Kiarab kwa hiyo sio ajabu kuona maneno hayo kama Alkhamis au Jumaa kuafanana na Kiarab(namaanisha kiarab sio Kiislam maana hamna lugha ya Kiislam)
 
Back
Top Bottom