Kwanini shuleni hakuna somo la madini na uchimbaji wake?

Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
4,246
2,000
Nu kweli, ila kwa wenzetu mtu akimaliza sekondari anakuwa anaweza kutambua aina za madini na mbinu za uchimbaji. Unaweza mchukua ukampeleka field na akaonyesha tofauti na asiyeenda shule.
Sekondari Kuna mining kwenye geography! Advance pia wanaosoma geography ipo.
 
Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
4,246
2,000
Habari wandugu,

Wenzetu wazungu wanujuzi sana wa madini, wanafundishwa shuleni. Mzungu nu rahisi kutambua Ruby, dhahabu au almasi akiiona.

Lakini mbongo hata anafika form six hawezi tambua madini aina yoyote. Kama elimu inamuwezesha mtu kupambana na mazingira yake, na mazingira yetu yamejaa madini, kwa nini hatufundishi somo la madini, upatikanaji na uchimbaji wake shuleni?

Elimu ambayo itamuwezesha mhitimu kujijiri kwenye uchimbaji akimaliza.
Utakuwa ulikuwa mtoro mzuri sana kuanzia primary Hadi sekondari
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,924
2,000
Masomo yapo ila kama ulikimbilia HGL utaishia kulaumu. Extraction of metals. Ukija level ya degree kuna mining engineering na nyingine nyingi
Unataka kuniambia mtu wa form six anaweza kutambua kuwa hii ni almasi, hii ni dhahabu, hii ni ruby nk. Ukimpeleka machimboni, anaweza kuwa na maarifa yoyote kumzidi darasa la saba anayechimba?
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,739
2,000
Red Giant

Kwanza kwanini wabongo mnapoongelea mizungu lazima muanze na 'wenzetu'? Mizungu haiwezi kusema hivi hata kwa bahati mbaya ila watanganyika kila siku lazima mjinasibishe nao si viongozi au watu mitaani utasikia 'wenzetu'. So annoying.

Pili, sio kweli kwamba mizungu inajua madini kwa kuona tu, tunaishi nao tunawajua vizuri wengi hawajui hata nchi zinazozizunguka nchi zao let alone mabara au madini.

Wanaojua mambo ya madini ni ambao wamejiongeza wenyewe tokana na interests zao kitu ambacho mwanafunzi yeyote yule anaweza kukifanya TZ kama that interests them hasa ukizingatia tayari wamepewa basics kwenye masomo kama Geography na Chem.

Kazi ya shule ni kukupa basics sio kukutafunia kila kitu, wakati madini interests you mwingine interest yake ni magari nae atauliza kwanini shuleni hatufundishwi ufundi? So long as wote mna basics za kuanzia mengine jiongezeni wenyewe tuache kulaumu serikali kwa kila kitu.
 
Siyo madini tu 'wenzetu' mtu akimaliza sekondari anakuwa na ujuzi wa mambo mengi, anajua basic za afya, madini, hayo magari na mambo kibao. Siyo sababu ya interest tu, wanafundishwa shuleni. Huku mtu anatoka amesoma biology hadi form six lakini hajui chochote kuhusu afya, yupo kama la saba tu.

Mtu kasoma hadi form six biology na geography, lakini hajui chochote kuhusu kuhusu madini na uchimbaji, anazidiwa na la saba anayechimba.
 
MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
830
1,000

Kutambua almasi na dhahabu ni uzoefu wa field tu ndio maana std 7 akina msukuma wana migodi na wanajua madini wanayoyachimba.
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,739
2,000
Siyo madini tu 'wenzetu' mtu akimaliza sekondari anakuwa na ujuzi wa mambo mengi, anajua basic za afya, madini, hayo magari na mambo kibao. Siyo sababu ya interest tu, wanafundishwa shuleni. Huku mtu anatoka amesoma biology hadi form six lakini hajui chochote kuhusu afya, yupo kama la saba tu.

Mtu kasoma hadi form six biology na geography, lakini hajui chochote kuhusu kuhusu madini na uchimbaji, anazidiwa na la saba anayechimba.

With all due respect Madai yako yanakuvua nguo mwenyewe na wala sio hao form six.

Unashangaa la saba mchimbaji kujua madini kuliko muhitimu? Hujui experience is the best teacher wanasema hao hao 'wenzako' mizungu. Inawezekana unashangaa kwanini mtoto wa mvuvi aliyeanza kuvua akiwa na miaka 5 ni bora kuliko form 6 leaver. This is how absurd your argument sounds like.

Unadhani kwanini sehemu nyingi wanauliza experience yako kwanza kabla ya vyeti?

Naona umeamua kuwatetea mizungu wenzako kwa kila namna ila inaonekana huwajui, sisi tunaishi nao na tumesoma nao tunawajua fika.

Unawateteaje wenzako wanaoshindwa kujibu maswali mepesi kama haya? Hawajafundishwa shuleni? Nilidhani umesema wao wakimaliza wanajua kila kitu.

Hizo video zinapotosha sana sababu zinachagua waliojibu hovyo kwa nia ya kuprove ishu yao. Ukiwauliza maswali kama hayo watanzania utashangaa ujinga uliokithiri, kuna mmoja aliniambia Ulaya ni nchi!!

Pili ni kuwa, nafahamu umuhimu wa experience, na pia nafahamu mtu anayefanya jambo kwa experience na aliepita shule akajua abc wanakuwa tofauti sana.

Mfano, watu wanachenjua dhahabu kimazoea, lakini uchanjuaji mzima ni inorganic chemistry na mambo ya complex compounds formation. Sasa aliyesoma inorganic anaweza kuwa tofauti na asiyeenda shule, hata kama huyu anaexperience? Je shule imemuweka hatua yoyote mbele katika kupambana na mazingira yake?

Zamani kulikuwa na somo la kilimo shule ya msingi, watu walijifunza mambo ya mboji, crop rotation, mimea ya mikunde nk, hili liliwaweka waliosoma hatua mbele kuliko wale wanaofanya kilimo kwa mazoea(experience). Ndicho ninachosema, basic education inatakiwa kumuweka aliyeipata hatua fulani mbele katika kupambana na mazingira yake yule aliyeisoma, isiwe tu 1+2=3. Ifundihae pia basics za mining, kama kutambua madini. Basics za afya nk.
 
Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
9,029
2,000
Mnamshambulia mtoa uzi utadhani mliosoma hayo madini mkipewa mtayajua ni kweli hakuna somo la kutosha kuanzia level za chini kuhusu madini hiyo dhahabu tu watu wengi hawaijui achilia mbali hayo madini mengine na wengine hawajawahi kuiona kabisaa ingawaje Tanzania imezagaa wenzetu kama hayo madini ndio rasilimali zao hata wakina Ras Simba wao wangeanzisha vituo vya kufundisha aina mbali mbali za madini...
 
JAKUGOTE

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
551
1,000
Unataka kuniambia mtu wa form six anaweza kutambua kuwa hii ni almasi, hii ni dhahabu, hii ni ruby nk. Ukimpeleka machimboni, anaweza kuwa na maarifa yoyote kumzidi darasa la saba anayechimba?
Ishu ni kwamba masomo yapo au hayapo?

Uwasilishaji wa maarifa lengwa ndio haupo serious lakini mambo mengi yapo. Walimu wanapaswa wafundishe kwa mbinu mbalimbali ikiwemo matumizi ya zana(mwanafunzi ayaone hayo madini) na hata kufanya ziara kwenda kwenye maeneo husika(migodi) na kuoneshwa uhalisia wa kitu kinachofundishwa but hivi vitu havifanyiki, tunafundishwa kijuujuu tu (theoretically) na kulazimishwa kukariri ili tuweze kujibu mitihani.
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,739
2,000
Hizo video zinapotosha sana sababu zinachagua waliojibu hovyo kwa nia ya kuprove ishu yao. Ukiwauliza maswali kama hayo watanzania utashangaa ujinga uliokithiri, kuna mmoja aliniambia Ulaya ni nchi!!

Pili ni kuwa, nafahamu umuhimu wa experience, na pia nafahamu mtu anayefanya jambo kwa experience na aliepita shule akajua abc wanakuwa tofauti sana.

Mfano, watu wanachenjua dhahabu kimazoea, lakini uchanjuaji mzima ni inorganic chemistry na mambo ya complex compounds formation. Sasa aliyesoma inorganic anaweza kuwa tofauti na asiyeenda shule, hata kama huyu anaexperience? Je shule imemuweka hatua yoyote mbele katika kupambana na mazingira yake?

Zamani kulikuwa na somo la kilimo shule ya msingi, watu walijifunza mambo ya mboji, crop rotation, mimea ya mikunde nk, hili liliwaweka waliosoma hatua mbele kuliko wale wanaofanya kilimo kwa mazoea(experience). Ndicho ninachosema, basic education inatakiwa kumuweka aliyeipata hatua fulani mbele katika kupambana na mazingira yake yule aliyeisoma, isiwe tu 1+2=3. Ifundihae pia basics za mining, kama kutambua madini. Basics za afya nk.

Kwahiyo nje mtu aliyemaliza high school anajua madini kwa kuyaangali tu? Sijui nchi gani hizo unaongelea.

Na kwanini mkazo uwekwe kwenye madini tu kwanini wasifundishe uvuvi, kilimo, ufugaji, ufundi, uashi, ushonaji nk ili mtu akimaliza form 6 awe anajua kila kitu.
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,739
2,000
Mnamshambulia mtoa uzi utadhani mliosoma hayo madini mkipewa mtayajua ni kweli hakuna somo la kutosha kuanzia level za chini kuhusu madini hiyo dhahabu tu watu wengi hawaijui achilia mbali hayo madini mengine na wengine hawajawahi kuiona kabisaa ingawaje Tanzania imezagaa wenzetu kama hayo madini ndio rasilimali zao hata wakina Ras Simba wao wangeanzisha vituo vya kufundisha aina mbali mbali za madini...

Again, watanganyika na kujinasibisha na uzungu kwa kuwaita 'wenzetu' kila mara mnapoongelea mizungu. Wao hawawaiti nyie wenzao hata kwa bahati mbaya ila nyie mnakomaa tu. Smdh

Pili, kama unaona ufundishaji haukidhi hiyo ndo fursa yenyewe, kuwa ras simba wa madini wewe. Piga hela kabla watu hawajaamka acheni kulalamika kila kitu.
 
Baraja Gang

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
1,532
2,000
Naona wachangiaji mnamshambulia muanzisha uzi bila kuelewa alichokikusudia. Mnasema ni topic ya form two sijui habari ya Metal na Non Metal vitu gani, like seriously!? Halafu ndio nyie nyie mlioshika vitengo mnatuhudumia.

Nilichomuelewa huyu bwana ni kuwa, Kwa nini kusiwe na Somo lenye Topics zake mwanzo hadi mwisho(kuanzia majina, upatikanaji wake, kuyachimba, kuyasafisha, kuyachonga nk) nasio hizo kukaririshwa mambo za Mining za form two.

Liwe ni Somo lililokamilika kama Hisabati kuanzia Shule ya Msingi, ukifika chuo sasa unaamua kuspecialise utakakotaka.
 
Kabisa, mtu akitoka awe na ABC za madini na uchimbaji. Mazingira yetu yana madini mengi sana, elimu inatakiwa kutusaidia kuyatawala.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,924
2,000
Kwahiyo nje mtu aliyemaliza high school anajua madini kwa kuyaangali tu? Sijui nchi gani hizo unaongelea.

Na kwanini mkazo uwekwe kwenye madini tu kwanini wasifundishe uvuvi, kilimo, ufugaji, ufundi, uashi, ushonaji nk ili mtu akimaliza form 6 awe anajua kila kitu.
Kuna shule ya Meta Mbeya, mtu alikuwa anachukua umeme hadi form 4 kama somo la ziada. Akitoka hapo ni fundi umeme kabisa. Mwingine atachagua kile na mwingine kile.
 
Anonymous Caller

Senior Member
Sep 8, 2016
197
250
Mimi sijafundishwa na yeyote kuhusu hayo madini.
ila nimejiokotezea tu kama ifuatavyo:

Maana:
madini ni raslimali inayopatikana juu ya uso wa ardhi ama kwa kuchimbwa ama kutwaliwa.

Matumizi:
mapambo au shiny objects.

Aina:

(a) madini miamba
(b) madini ya vito
(c) madini vimiminika

Hayo yanakutosha.
haya ni ambayo unaweza kugoogle.
ninayo mengne ya kienyeji zaidi
 
Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
4,246
2,000
Hizo video zinapotosha sana sababu zinachagua waliojibu hovyo kwa nia ya kuprove ishu yao. Ukiwauliza maswali kama hayo watanzania utashangaa ujinga uliokithiri, kuna mmoja aliniambia Ulaya ni nchi!!

Pili ni kuwa, nafahamu umuhimu wa experience, na pia nafahamu mtu anayefanya jambo kwa experience na aliepita shule akajua abc wanakuwa tofauti sana.

Mfano, watu wanachenjua dhahabu kimazoea, lakini uchanjuaji mzima ni inorganic chemistry na mambo ya complex compounds formation. Sasa aliyesoma inorganic anaweza kuwa tofauti na asiyeenda shule, hata kama huyu anaexperience? Je shule imemuweka hatua yoyote mbele katika kupambana na mazingira yake?

Zamani kulikuwa na somo la kilimo shule ya msingi, watu walijifunza mambo ya mboji, crop rotation, mimea ya mikunde nk, hili liliwaweka waliosoma hatua mbele kuliko wale wanaofanya kilimo kwa mazoea(experience). Ndicho ninachosema, basic education inatakiwa kumuweka aliyeipata hatua fulani mbele katika kupambana na mazingira yake yule aliyeisoma, isiwe tu 1+2=3. Ifundihae pia basics za mining, kama kutambua madini. Basics za afya nk.
Acha ujuha, mining inafundishwa shuleni kwenye geography na minerals kuanzia primary mpaka chuo kikuu kwa wanaoopt geography...kutokujua kwako unataka kufanya mjumuisho usio sahihi.
Nenda shule ya sekondari iliyo karibu nawe omba syllabus ya geography
 
GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,976
2,000
Vyuo vya madini vipo,shinyanga na singida nenda ukasome..bongo mambo serious yanaanzia juu huko mbelembele kwa mbelee sana.
Shule za mtakatifu kayumba huwezi kufundishwa mambo ya muhimu..kwanza ili iwe je?
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,739
2,000
Naona wachangiaji mnamshambulia muanzisha uzi bila kuelewa alichokikusudia. Mnasema ni topic ya form two sijui habari ya Metal na Non Metal vitu gani, like seriously!? Halafu ndio nyie nyie mlioshika vitengo mnatuhudumia.

Nilichomuelewa huyu bwana ni kuwa, Kwa nini kusiwe na Somo lenye Topics zake mwanzo hadi mwisho(kuanzia majina, upatikanaji wake, kuyachimba, kuyasafisha, kuyachonga nk) nasio hizo kukaririshwa mambo za Mining za form two.

Liwe ni Somo lililokamilika kama Hisabati kuanzia Shule ya Msingi, ukifika chuo sasa unaamua kuspecialise utakakotaka.

Kwanini mkazo uwe madini tu? Me nadhani inabidi wafundishe kila kitu kuanzia uvuvi, kilimo, ufugaji, ufundi, uashi, ushonaji, upishi nk... ikiwezekana hata uhandisi, udaktari, sheria na kada zingine zote zifundishwe katika ngazi ya awali na sekondari ili mtu akimaliza form 6 awe anajua kila kitu. Hapo vp?
 
snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,339
2,000
Wewe ulisoma shule gani?
Mimi nakumbuka kusoma hivyo vitu form 2/3
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom