Kwanini Shule za Serikali za vipaji maalum hazifanyi vizuri mitihani ya kidato cha nne (CSEE) tofauti na ile ya kidato cha sita(ACSEE)

Sijasoma uzi wako ola nataka nikuambie hakuna shulw wanaiva mitihani kama private school. Enzo za ujana wangu niliwahi kuwa mwalimu wa taaluma private school fulani hivi; hivyo msinibishie
Sasa ujasoma unajibu nn?Nyie ndo zile mbuzi za MiFive tena na Katiba mpya🤣🤣🤣🤣
 
Hizi shule zinachukua wanafunzi wa wastani wa juu kabisa, yani wanafunzi waliofanya vizuri darasa la saba kwa kifupi wanachukua Cream tupu, Hapa naongelea shule kama Kibaha, Mzumbe, Kisimiri, Msalato, Tabora Boys n Girls , Kilakala na Ilboru .Shule hizi upande wa Olevel hazifanyi vizuri sana unakuta mpaka 0 za kutosha unabaki unajiuliza hii kweli ilikua Cream au samri? wakati mtoto alitoka shule ya msingi akiwa na Ufauru wa kutisha A zote anaenda kipaji maalumu kipaji kinayeyuka anazungusha yai.

Kwa Advance shule hizi kiukweli zinajitahidi na hapa tuangalie ulinganyifu wa ufaulu wa baadhi ya hizi shule kati ya Olevel(CSEE) na Advance (ACSEE) kwa miaka ya nyuma na sasa 2021

2️⃣0️⃣1️⃣6️⃣

1. MZUMBE (O LEVEL KITAIFA YA 27 ikiwa na div 4-1, na 3-12. ADVANCE KITAIFA YA 8)

2.ILBORU ( O LEVEL KITAIFA YA 42 ikiwa
na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 9)

3.KIBAHA( O LEVEL KITAIFA YA 1️6️ ikiwa na div 4-1. ADVANCE KITAIFA YA 7)

4.KISIMIRI (O LEVEL KITAIFA YA 592 ikiwa na div 0-22, 4-95, 3- 25. ADVANCE KITAIFA YA 1)


2️⃣0️⃣1️⃣8️⃣

1.KILAKALA (O LEVEL KITAIFA YA 76 ikiwa na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 14)

2.MSALATO ( O LEVEL KITAIFA YA 102 ikiwa na div 4-12. ADAVANCE KITAIFA YA 17)

3.TABORA GIRLS ( O LEVEL KITAIFA YA 90 ikiwa na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 11)

4.TABORA BOYS ( O LEVEL KITAIFA YA 67 ikiwa na div 4-1.ADVANCE KITAIFA YA 15)


2️⃣0️⃣2️⃣1️⃣

kISIMIRI ( O LEVEL KITAIFA YA 404 ikiwa na div 4-60. ADVANCE KITAIFA YA 1)

KILAKALA ( O LEVEL KITAIFA YA 30. ADVANCE KITAIFA 56).

ILBORU (O LEVEL KITAIFA YA 23. ADVANCE KITAIFA .18)

MZUMBE ( O LEVEL KITAIFA YA 10. ADVANCE KITAIFA 10)


Baaada ya kuangalia viwango hivyo vya miaka ya nyuma mpaka karibuni utaona kabisa pamoja na kwamba shule za serikali zinachukua cream lakini wanashindwa kuzirutubisha ziendelee kubaki cream ambapo wengine hubadirika kutoka Cream kwenda maziwa mgando.kutoka kuingia na wastani wa A shule ya kipaji na kuchomoka na Div 4 au 0 ni hatari mno.

Ona shule kama Kisimiri unaweza kudhani wao labda wamejikita zaidi Advance na kuwaacha wale wa o level wapambane na hali zao shule Advance inakua ya 1 lakini O level 0 za kutosha na 4 wakati utaratibu kwa level zote ni ule ule kuchukua Cream.

Shida ipo wapi wazee wangu? Huku government hususani o level ni kwamba serikali inashindwa kuvilea vipaji vyenye umri wa balehe na kuweka mkazo zaidi kwa wanaojitambua maana Advance kidogo mtu akili inaelewa na kupambanua majambo.

Hii tofuati kabisa na shule za binafsi ambazo pia moja ya sababu za ufaulu wao mkubwa kuchukua cream inatajwa lakini mbona wenzetu wanawasha kote kote mfano Marian boys and girls, Feza Boys n Girls wakiwasha top 10 olevel unakuta na Advance wamo....Pia wenzetu wa Binafsi O level ambapo government inachechemea wao ndo wanawasha haswa si unaona Cream za KEMOBOS zote one , Cream za St Francis Zote one, Cream za Bright na waja zote one sasa kwa nini Cream zetu za O level ni ngumu kutoa one zote basi angalau muishie 3 kweli Cream mnailambisha 4 na 0 sijapenda aisee.

Eti wakuu mnaona sifa kuitwa wakuu wa shule special na kupewa kipaumbele cha kufanya selection? Wakati mikakati ya kumaintain vipaji vyetu ni 0 😱

Kwa nini yani Whyyyy jaman whhhhy ??
Jibu ni rahisi tu, advance shule za vipaji, asilimia kubwa uchukua wenye one kali kutoka shule za kata, ambao wamefaulu kwa uwezo halisi bila kubebwa (wakuu wa shule ulizingatia sana hili kwenye selection zao), ndiyo maana a level ufanya vzuri kuliko private na hao unao waonaga advance wana 2 na 1 za kuchechemea kutoka kwenye hizi shule za vipaji ni wale waliotoka private kwa asilimia kubwa. Pili advance shule ni chache kwa ni rahisi kudhibiti wizi wa mitihani ukilinganisha na o level yenye maelfu ya shule, ndiyo maana unaonaga mara nyingi wanafunzi walio ongoza kitaifa utokea shule za serikali za vipaji maalumu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom