Steven Mamba
Member
- Feb 14, 2015
- 39
- 15
Kwanini serikali ya Magufuli inaogopa maandamano ? Nchi kuruhusu maandamano, uhuru wa habari nk ni ishara hiyo nchi imekomaa kidemokrasia. Kwanini tuna rudi nyuma ? Watanzania washamkubali sana Magufuli, kila siku wanampongeza na kumsifia kwa kazi nzuri anayoifanya. Watanzania wengi waliowapigia upinzani kura leo wanamkubali Magufuli. Tanzania ni nchi ya kidemokrasia katiba na sheria ya nchi inaruhusu maandamano na mikutano ya siasa. Kuwazuia upinzani wasiandamane inasaidia nini serikali ya JPM ? Binafsi nakubaliana na kauli ya raisi wabunge waende kufanya mikutano majimboni kwao lakini sheria ni sheria na sheria inwaruhusu chadema kufanya mikutano yao. Watu wakiandamana masaa matatu manne kisha wakaenda zao manyumbani inawakera nini serikali ? Kama sio ubabe usio na maana. Kama ni machafuko na watu kuumia yataletwa na serikali na sio mtu mwingine. Tusubirie CNN