TAMKO
JF-Expert Member
- Oct 11, 2011
- 1,090
- 762
Tumeikosea nini maskini sisi wananchi, kwanini serikali hii itutendee hivi kikatili kila siku afadhali ya jana. kama lipo tulilo kukoseeni mtusamehe jamani lakini sio hivi. nchi yetu wenyewe lakini twaiona chungu kweli kweli.
BIASHARA mtaji utafute kwa jasho mwenyewe, ufungue ujasiriamali wako kisha sikilizia hiyo kero utayoipata mpaka upate leseni. ukiitenga bishara faster wameshawahi kudai makato ya kodi na ushuru ushenzi mtupu. mnavuna msipopataabikia.
wakulima wanasota kulima mazao yao, mtu anafungasha kiroba chake atoke porini aje mjini akiuze apate hela lau ya sukari anapambana na mlolongo wa mijitu njiani inakaba ipewe ushuru wa mazao, hata ndizi nne tano wanakukaba. mbaya zaidi huna pa kushtaki. Kiongozi yeyote utayemshatakia atakupatia kero kubwa zaidi.
kwenye usalama ndio Hovyo kabisa. Polisi mwenye uzalendo kumpata ni kama almasi. hata ikitokea akawepo ni tone la maji masafi kwenye bahari, system nzima imeoza. ukimwona polisi mwenye bidii ukampongeza kosa kubwa sana umemchongea kwa misukule mabosi wake watamtupia porini msimwone tena, polisi mzalendo ni adui wa kutisha sana ndani ya jeshi letu. naamini ipo CV maalum ya kumpa askari cheo kikubwa. nadhani lazima aprove ukatili wake na roho mbaya yake kabla ya kuwa mkuu wa kituo au kamishna. Siamini na tena sitaki kuamini kwamba Polisi wameshindwa kuligundua, kulisaka na kulitokomeza kundi la vijana hatari "mbwamwitu" ambao hufanya matukio makubwa na mabaya ya uharifu. miaka na miaka nasikia habari za kundi hilo. ni kundi la wavulana wadogo kabisa ambao sipati picha wakikua watakuwa na matunda gani ndani ya taifa letu.
kama kweli Intellijensia ya Polisi na serikali wameshindwa kulidhibiti kundi hili basi usalama wa nchi hii uko mashakani sana. Vijana hawa ambao interest yao ni fedha akitokea mjinga mmoa mwenye fedha akawafadhili ni rahisi kuwatoa kwenye mtazamo wa uchumi na kuwadumbukiza kwenye mtazamo wa kisiasa ambao madhara yake hayata pimika. sote tunajua dogodogo army ilianza kama kundi la vibaka kama hili.
polisi wa leo hawakamati wahalifu kabisa. ile tabia ya nyakati zile ukamwona polisi anatimua mhalifu na kumtia nguvuni haipo tena. kila mtaaa kuna vijana wanajipulizia mabange tu tena waziwazi na polisi wanawachekea tu. KIKWETE kwani nani kakulazimisha kuwa mkuu wa nchi?? Kushindwa uongozi ni kitendo cha uzalendo ACHA..! JIUZULU sio aibu..! NI USHUJAA.Uongozi ni Kipaji labda mwenyezi Mungu hakukupatia kipaji hicho babangu acha tu waachie wengine ni Ushujaa sio aibu.
unajichanganya mwenyewe unaichanganya na nchi basi mambo yote holela holela. Uliona wapi on earth mtu anaunda tume yeye mwenyewe, Tume imfanyie kazi yake yeye ya kukusanya maoni ya Kuunda katiba, kisha Tume inamletea majibu husika, anawapongeza na kuwasifia kwa kazi nzuri, anaikubali ripoti na kuilabel kwamba ni ripoti yake halali kwa kuisaini. anaipeleka pahala watu waijadili ripoti yake mwenyewe. kisha kwenye maneno ya utangulizi akiongea na wanamjadala anaanza kwa kuiponda ripoti yake mwenyewe. means anajiponda mwenyewe mbele ya kadamnasi hii kama sio zaidi ya kiroja ni nini. ?? kama from point Pai uliona ripoti sio unawamegea waziwazi kwamba HIKI-SICHO FULL STOP. . ni kama mfano wa baba mwenye nyumba, anaham ya kula jogoo, basi anawaita watoto wake anawaonyesha moja ya jogoo wakalikamate. wanapiga mbio na kwa jasho wanamkamatia mzee alichotaka. kisha mzeee anamwendea mchinjaji anamsihi amchinjie jogoo wake akamle. lakini wakati anamkabidhi mchinjaji anamponda sana jogoo, "kwanza jogoo mwenyewe hovyo, aliwahi kuugua kifaduro, jogoo huyu kwanza ana dengue, hata ukimchinja simli" Mchinjaji lazima abaki ameduwaa, huyu mzee vipi, kuku alete mwenyewe na kumponda amponde yeye huyo huyo tena..!!
Simtakii Mkuu wa nchi ashuke barabarani kuwakamata trafic wanaokamua madereva kila siku, simtakii raisi ashuke azikemee serikali za mitaa kwa kuwakaba raia kwa ushuru usio na tija, simtakii rais akawasake Mbwamwitu awaangamize no.. wajibu wake mkuu ni kuisimamia na kuitekeleza katiba aliyonayo mkononi mwake. kama tatizo ni mbwamwitu ng'oa wakuu wa polisi au wakuu wa kanda maalum weka wengine wameshindwa kazi ndio wajibu wako, rungu unalo mbona umeliweka uvunguni miaka karibia tisa sasa?. Raisi angekuwa na meno, akaisimamia katiba kikamilifu kiongozi mmoja angemwajibisha mwenzake na mwenzake na ufanisi wa kazi lazima ungetokea. asilimia kubwa ya wanawake wanaokwenda ofisi zenye mabosi wanaume ukianzia mawaziri lazima waombwe "ngono" . sikatai mwanamke kutongozwa lakini pale ngono inapoombwa kukiwa na hitaji kwa raia ni ubakaji na hongo ya nguvu. lakini unadhani ni kwanini Kiongozi anajiachia na kutumia ofisi kwa mambo yake binafsi ni kwa sababu ya UUngu-mtu aliojipachikia. anaamini hayupo wa kumwadabisha. hata kama yupo hana meno ya kung'ata ni mbwa koko tu. hata ukienda kumshataki kwa bosi wake bosi wake nae ndo zaidi yake. kama katiba ingetekelezeka hakuna ambaye angeichezea nchi, mpaka unakuta zanzibar wanampokonya Madaraka raisi naye anaangalia tu anachekelea hapo kuna mkuu wa nchi tena?.
ni kama mwanaume mwenye wake wawili, siku moja anakuja mwanaume na kumwambia kuanzia leo huyu bibi mdogo nachukua mimi, na wewe unachekelea tu.. hauwezi kuitwa mwanaume tena. jinsia ni ya kiume lakini matendo.. mm.
naandika haya kwa machungu sana kwa sababu ni wajibu wako.kama wananchi wa kiwalani leo wanateswka na mbwamwitu hao, kesho kkoo keshokutwa dar yote na kisha mikoani tarajia hata usalama wa makazi yako utakuwa hatarini. ukiwa kiongozi unajivunia ulinzi ila utashangaa kesho utapoacha uongozi ulinzi utayeyuka. hata kama utakuwa nao sio kivilee,.. unapewa askari koko wawili watatu ambao wakistuliwa mbio kisha utaona machungu ya mbwamwitu au wahalifu. sio vizuri kujivuna, ukiwa juu jua kesho utakuwa chini, kama usipokiondoa kinyesi leo utakuja chini utakikuta wewe na watoto wako na jamii yote. ukibisha rudia somo la historia. Ingawa kuna mazuri umeyafanya tunayaona, umetengeneza barabara kwa kweli hapo dole.. ingawa watu wanasema ni kazi ya magufuli lakini magufuli ni nani si waziri wako!! hapo dole, cha pili Umefanikiwa kumleta Obama Tanzania. heko. ingawa mie mwananchi wa kawaida sijaona matunda ya ziara yake. kingine kizuri umevunja rekodi ya kutembelea nchi nyingi zaidi kuliko rais Yeyote Tanzania. heko. na kingine una utu aisee, kutembelea wagonjwa, misiba na sherehe umevunja rekodi. kuna wakati niliwahi kupropose tuwe na maraisi wawili. rais mwenye meno ambaye ni mtendaji na mkuu wa nchi pamoja na ceremonial president.
Ok hata kama ni kweli kwamba CCM hiyo 2015 itaondoka madarakani, but kwa Muda uliobaki embu jaribu kuonyesha kwamba nchi hii ina Raisi. fanya liwalo na liwe, safisha nchi at least tukiwa wazee sana tuseme yule ceremonial president ukingoni mwa uongozi wake alipata meno, akaisafisha nchi..