Kwanini serikali wasiwape pikipiki vijana wa Dodoma wanawapa wa Arusha waliowakataa?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Hebu na wewe jiulize,

Vijana wa Arusha wengi wao waendesha toyo (bodaboda) waliikataa CCM yote kuanzia rais, mbunge hadi madiwani lakini ndio waliopewa upendeleo wa pikipiki.
View attachment 442472
Je, serikali ya CCM inatuma ujumbe gani kwa vijana wa Dodoma na sehemu zingine ambao walikesha kuichagua CCM kuanzia rais, madiwani na wabunge wote kutoka CCM, watajisikiaje?

Quinine.
 
Sisi kama mvua ikiamua kunyesha inanyesha nchi nzima na hawana mpango wa kugawa kwa upendeleo na pia ni kazi nzuri ya Mkuu wa mkoa wa Arusha.

Naamini CHADEMA haiwez kugawa maeneo ambayo hajachaguliwa.
 
Wagogo wameshatumika hawana faida tena, arusha kama hujui endelea kutafakari kabla ya uchaguzi mkuu pale kuna kura za ubunge arusha mjini, subirini kijacho sio mtabiri mimi
 
1. Chanzo cha fedha hizo ni nini?
2. Sababu za kugawa pikipiki arusha
3. Serukali imeshindwa kutoa ajira kwa vijana waliosoma inagwa bodaboda?

4. Lengo LA kugawa bodaboda ni lipi?

Kqa ujumla wake hii ni rushwa kubwa kutokea hapa nkoani arusha. Utasikia serikali inatamba eti inachukia rushwa.
 
Serikali ikifanya majukumu yake mnasema rushwa.....dah binadamu kazi sana.Zirudisheni basi basi kama mnaona ni rushwa.
 
Sio Rushwa Ndugu.....
Ila serikali inatekeleza ajira kwa vijana wa Arusha kama alivowaahidi Rais wao wa Arusha MH LEMA ...
Usishangae Serikali kutekeleza ahadi hizi kwenye Jimbo LA Upinzani kwani ndo Sera inataka hivyo....Apa Wabunge wa CCM km Mabura wa Nyamagana vijana wake waliokua wamejiajiri wamefukuzwa mijini japo yeye ni mbunge wa CCM tena MSUKUMA lakini kwa vile hana Sera maskini inasikitisha mwaka sasa hakuna alichofanya Mwanza Miradi mingi imekwama at a Yale majengo makubwa yaliyokua yanatekelezwa na mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwishnei inasusua balaa.....Hongera LEMA ongereni wana Arusha ahadi imetimia na bado za Hospitali kujengwa
 
Tatizo la misukule wa ufipa ni wavivu wa kufuatilia habari yote, pia wana wivu uliopitiliza.

Wanaahidi alafu Wanakuja kuyapinga tena hayo mabadiliko kwa manufaa ya siasa zao uchwara.

Mnapinga maendeleo ya vijana wa Arusha ili iweje??

Shame on you ufipa boys
 
Sisi kama mvua ikiamua kunyesha inanyesha nchi nzima na hawana mpango wa kugawa kwa upendeleo na pia ni kazi nzuri ya Mkuu wa mkoa wa Arusha.

Naamini CHADEMA haiwez kugawa maeneo ambayo hajachaguliwa.
Kwani Chadema inakusanya kodi igawe pikipiki.
 
Serikali ikifanya majukumu yake mnasema rushwa.....dah binadamu kazi sana.Zirudisheni basi basi kama mnaona ni rushwa.

Kipi kilipaswa kuwa kipaombele cha serekali hii kwa sasa kati ya wahanga wa tetemeko kagera na pikipiki kwa wakazi wa Arusha? Serekali inahubiri viwanda, vimewashinda sasa wanagawa pikipiki badala ya kujenga viwanda. unaweza kutuambia pikipiki inazalisha nini? Kuwa mtu mweusi nimeamini ni laana.
 
Tatizo la misukule wa ufipa ni wavivu wa kufuatilia habari yote, pia wana wivu uliopitiliza.

Wanaahidi alafu Wanakuja kuyapinga tena hayo mabadiliko kwa manufaa ya siasa zao uchwara.

Mnapinga maendeleo ya vijana wa Arusha ili iweje??

Shame on you ufipa boys
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom